Hata ukimuuliza Chenge atajibu sera ya CCM ni ujamaa. Wenye akili ndogo wanadhani nchi hii ina tatizo la sera tu.
Chenge ni mjamaa kama MM wenu, Lowasa ni mjamaa kama MM wenu, Rugemalila ni mjamaa kama MM wenu
View attachment 245912 View attachment 245913
Kusema tu sera yangu ni ujamaa haijawahi kuwa tatizo kwa akina Chenge kama ambavyo sio tatizo kwa MM.
Kwahiyo unakiri kuwa hujui sera za chama chako na huihitaji kujua??
Ndicho nilichomwambia jamaa yangu hapa chini, wanachama wengi wa vyama vya siasa ata hawajui vyama hivyo vinasimamia nini, wanachojua ni majina ya watu na matukio, basi.
Kwa wale waliosomea mambo ya project management kuna kitu kinaitwa RAID. Pamoja na mambo mengine, project yoyote inakubidi kuidentify risk zinazoweza kuadhiri project yenyewe kuisha on time and within the budget. Kati ya risk kubwa nayoiona ndani ya ACT "WAZALENDO" ni kumtegemea ZZK kama kiongozi pekee mwenye mvuto na anayeweza kusikilizwa na kueleweka machoni mwa watanzania! Binafsi simuoni kiongozi yoyote ndani ya chama hichi anayeweza kusimama mwenyewe bila msaada au support. Hii ni risk kubwa kwa chama cha kisiasa kuwekeza kwa binadamu badala kutegemea sera na itikadi ya chama! Siombi jambo baya limtokee kwa ZZK, ZZK ni binadamu leo yupo kesho ametangulia mbele ya HAKI.
Nafikiri unaweza kuona hapo juu.Ni mfano halisi wa wanachama na ata viongozi wa vyama vingine hapa nchini.Sikuhizi siasa zimekuwa ni kama mipasho, mkutano mzima wa siasa ata uwe ni masaa mawili, huwezi kusikia suala la sera wala nini, ni majina ya watu na matukio mwanzo mwisho.
Ndio maana kwenye hili ACT wapo mbele ya vyama vingine vya upinzani.Kwenye mikutano ya ACT asilimia walau 50 za hotuba zao ni sera na aina ya nchi wanayotaka kuijenga.Lakini ukienda mikutano ya Chadema kwa mfano asilimia 99.9% za hotuba zao ni majina ya watu na matukio.