Watanzania hatuna chuki binafsi na Zito bali tuna chuki kubwa kwa yale aliyotufanyia. Mengi yamesemwa juu yake lakini hajawahi kuyajibu kwa vielelezo. Hajawahi kueleza kwa ukamilifu hela aliyokuwa akiipokea toka CCM (kwa kupitia maofisa wa TISS) ilikuwa ya nini? Hajawaeleza Watanzania ukaribu wake mkubwa na mawasiliano yake na maofisa wa juu wa TISS yamekuwa yanahusu nini hasa. Mawasiliano na maofisa wa TISS yalioneshwa kwa vilelezo, na hasa yalikuwa wakati wa kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi.
Leo anapotaka kushirikiana na UKAWA, Watanzania watakuwa na uhakika gani kuwa nia yake kubwa siyo kutaka kujua mipango na mbinu za UKAWA kwa manufaa ya wale ambao amekuwa akiwatumikia siku zote, CCM?
Kipindi anapokea hizi hela alikuwa ni kiongozi na Mwanachama wa Chadema. Ni katika kikao gani cha Chama mlishawahi kumuita na kumhoji?
Utatofautishaje skendo hiyo na Ile ya Lema na wizi wa Magari? Au ilishawahi tolewa Ufafanuzi? Tatizi mnachagua watu wa kuwawajibisha, Mngekuwa serious kweli na hizi kashfa, Mngehoji Mbowe na Ununuz wa piki piki za chama, mngehoji kuhusu Ruzuku kukopeshwa kwa viongozi wa Juu.
Kuna Madudu kibao, Ila mko busy na Zitto kutwa nzima. Keshatoka kwenu, lakini bado Mko nae tuu, as if Uraisi kura zinapigwa na Chadema tuu.
Mtajidili mtu mpaka lini? Wananchi ndio wenye Maamuzi ya Mwisho.
Zitto ana madhaifu Mengi tuu. Lakini ktk viongozi, yeye ana afadhali compared to the rest. Siku zote, hata maofisini, ukisimama ktk misingi ya sheria, utaitwa majina yote, utachukiwa ili mradi tuu, ukatetamaa, au ubwage manyanga, wanaokula, waendelee kula, wanao lala njaa waendelee kufa njaa.
Dini na siasa ni Bangi inayolewesha sana.