Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

mimi
Mmetajiwa shule za msingi alizosoma na vyuo alivyopitia na uzuri picha zilibandikwa kwa kila aliyetahiniwa...maswali mengi yanajirudia rudia nendeni kwenye hizo shule muanzie hapo mtajua kama mkweli au sio mkweli...Mimi binafsi nimpongeze kujitokeza hapa kumbe viongozi wetu wamo humu!Mwisho tuangalie maswali mengine kama ataturuhusu kuhusu nje ya elimu na vyeti vyake hasa hili wimbi la panya road Mbagala watu hawana amani
nilisoma miaka hiyo 89-95 hakukuws na picha darasa la 4&7 akatulie arudi tena
 
Mkuu hapo hujajibu tuhuma, umetumia teknik ya ku-confuse watu.

Kwa mfano katika maelezo yako Jina la 'Nchemba' hujaeleza limetokea wapi

miaka ya 80 hadi 90 hivyo vyeti vyenye passport size au picha viliwezekana vp? hapo umetudanganya mh waziri
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,

Labda nikupongeze kwa kuja mbele kutoa ufafanuzi wa tuhuma zinazokukabili kuhudu uhalali wa majina yako, lakini maelezo yako bado yana ukakasi mkubwa. labda nikuulize majina ulioamua kuchukua ndio hayo hayo yaliomo katika cheti chako cha kuzaliwa? maana hiyo ndio hati ya kisheria ya utambulisho wa jina lako. Na kama hayamo ulikwenda mahakamani kupata "Poll Deed" ili uweze kutumia majina mapya kisheria na kwamba kula kiapo kwamba hubadilishi jina kwa kuwa jina la awali limehusihswa na uhalifu?

Aidha pia ungetupa ufafanuzi ni kwanini una tarehe mbili za kuzaliwa katika "document" rasmi za serikali kuthibitisha elimu yako? hapo chini?

Attachments

  • ZEC#HapaKaziTu#99#99#158#14#0.jpg
    ZEC#HapaKaziTu#99#99#158#14#0.jpg
    41.6 KB · Views: 46
  • ZEC#HapaKaziTu#99#99#158#14#1.jpg
    ZEC#HapaKaziTu#99#99#158#14#1.jpg
    32 KB · Views: 45
Wakati wanafuatilia ukweli wazingatie pia ukweli na halihalis ya wakati huo
nakubaliana na wewe kwani wengi waliteseka mno kwa mbinu hizi .hii ilitokana na maeneo yalivyo kijiografia ,jinsi kufika ,maisha ya watu wakati ule ,miundombinu ya mawasiliano Enzi zile uende posta upange foleni opereta akoroge simu wee .hadi jioni anakoroga .usafir wa vijiji vingi kufikika ilikuwa kazi .tuendelee tu na zoezi la uhakiki.
 
Nashkuru Mhe;kwakuclear hii doubt,na tuanze ukurasa mpya sasa,lakini ni vyema Watanzania wakajenga tabia ya kufocus mbele zaidi kwani tukifukua makaburi watakaopona ni wachache sana.
Wewe sasa unaenda kinyume na muheshimiwa

Kilichoko mezani ni kwamba ufafanuzi wake umewaacha watu na maswali mengi
Ki ufupi haukizi viwango

Ieleweke hivyo, ni bora angeweka hata kielelezo kimoja na sio historia ya majina
 
Nadhani kile wanachofanyiwa wafanyakazi wa umma kifanyiwe pia kwa viongozi,upanga ukate kotekote na sio kundi fulani tu.uhakiki usiwe biased tutawaelewa.
 
Kwani mhusika hana kwao? Kwanza tuanzie na jina halisi la wazazi wake na kijijini kwao mengine yatafuata. Alizaliwa kwao peke yake, hana wajomba shangazi etc Ukweli utamuweka huru! Tuanzie hapo!
 
Ama kweli mheshimiwa ameshikwa pabaya!! Watu wengine sijui mkoje, mnakuwa wafukunyuku sana, hadi mnaleaving certificate yake, mliitoa wapi?
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Sina hakika kama alirudia rudia shule au laah, nachokumbuka huyu Mwiguru Nchemba nimekutana nae mwaka 1999 akitokea Elboll shule ya vipaji maalumu akija Mazengo Secondary ( St. JOhn University kwa sasa) akisoma EGM mimi nikiwa PCM shule nyingine lakini tulikutana kwenye Tuition ya Hesabu kwa Mwl.Kavinuke pale Jamhuri Secondary School na ndipo nilimfahamu na nadhani alikuwa kiongozi wa wanafunzi pale Mazengo Secondary, mtu huyu anapenda Siasa sana tangu akiwa mashuleni mpaka vyuoni, naomba kusema kijana ni mkweli kabisa kwa alichokisema hapa.
 
Mkuu, vipi shule ulizosoma ni zipi?

Vipi ni utaratibu upi ulitumika kubadilisha jina uliporudi kuendelea na shule? Maana drs la kwanza hadi la tano jina jingine,, la tano na kuendelea jina jingine... Iliwezekanaje hii?
Sidhani kama swali la iliwezekanaje anatakiwa kulijibu yeye,namaanisha halimhusu.
 
Back
Top Bottom