Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,348
Huwa nashindwa kuelewa nini hasa kinachomaanishwa ninapoona mjadala watu fulani hasa wanasiasa kwamba walisoma au waliendelea na masomo kupitia jina la mwanafunzi mwingine aliyefaulu.
Iliwezekanaje mtu kuchukua jina la mtu mwingine kwenda nalo sekondari akaliacha lake wakati wanafunzi huwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma na Passport wanaposajiliwa kuanza masomo ya sekondari?
Pia kwa wanaodaiwa waliokuwa wanachukua majina ya wanafunzia wengine si kuna wanafunzi ambao ulikiwa nao shule watakuwa wanakufamu kwa majina yako halisi ? Utajifichaje?!
Lakini pia miaka ya zamani wanafunzi wenye akili ambao inasemekana majina yao yalikuwa yanaibwa walikuwa wanaweza kufahamika hata wilaya nzima au shule kadhaa sasa iliwezekanaje utambulisho wao ukaibwa kirahisi hivyo bila watu kung'amua kuna mchezo mchafu?!
Na hao walioibiwa au waliochukuliwa majina yao wakiwa wanafunzi wadogo kwa nini huwa hawajitokezi hadharini kudai haki zao??