Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

Siamini kama kweli Tanzania ina wazalendo ( wazawa wenye nia njema) sishabikii mtu wala chama lakini blabla ni nyingi mno mbona mambo mengi yanafanyika lakini hawatoi essay ndefu kama hizi za kukemea mfano mdogo tu vurugu za Kusini kuhusu gas aundiyo waliokuwa wanafadhiri baada ya kunyimwa vitalu?
 
Mi nadhani Muhongo bado ana mtazamo wa Profe-to-student! Nadhani inawezekana Muhongo akawa na pointi ya kile akisemacho, ila akashindwa namna ya kukiwakilisha. Amesahau kuwa aliosema ni ukweli ambao anapaswa kutumia uprofesa wake kutekeleza mawazo ya Mengi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
kama mafisadi hawafi bhac lakini kama wanakufa malipo ni hapahapa duniani.
 
Historia nayoifahamu ni kwamba kiongozi wa unaposhindana na wawekezaji wa sampuli ya mzee Mengi inabidi ujiandae ...Muhongo inabidi amuulize Masilingi na Masha mziki wa watu kama hawa wanapoamua kukushughulikia unakuwaje . Namwonea huruma sana prof Muhongo kwa stement zake tokea Mtwara saga
Kuna watu wana "powers" kama ma Sharifu!. ukimtibua akakasirika, its a gone case!.
1. Alipoanzisha ITV akatishiwa na DTV. Mmiliki wa DTV Shabir Dewji aliswekwa 'ndani!'. Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani wakati huo, Silvanus Adel 'alimwaga unga!'.
2. Kwenye ule 'mchezo mchafu' wa Kilimanjaro hotel, Masilingi alipayuka sana!. Kapoteza ubunge na kapoteza uwaziri he is nobody now!.
3. Alipogombana na Masha, Masha kapoteza ubunge, kapoteza uwaziri, he is nobody now!.
4. Alipogombana na Rostam Aziz kwa kumuita 'Fisadi Papa!' na alipomjibu yeye ni 'fisadi nyangumi!', Rostam kapoteza ubunge, kapoteza biashara zote, kaikimbia nchi!. Kampuni zake zote zinapumulia mashine!.
5. Alipozozana na Yusuph Manji, Hivi sasa Manji anaelekea kufilusika!. Ameuza kila jengo limebaki jina tuu!.
6. Kile kipibdi cha 'Kiti Moto' kilikuwa OK kilipokuwa Channel Ten, Mzee akakinunua kwa dau kubwa na kukihamishia ITV . Alipotaka kuingilia 'contents', alitofautiana na mwendeshaji kipindi kilikufa mpaka leo mwendeshaji yuko juu ya mawe!.
7. Alipotofautiana na Tido kuhusu Kombe la Dunia na UK premier league!. Tido alipoteza kazi!.
8. Alipotofautiana na Mhariri Mkuu wa Guardian, Vumi Urasa, he lost his job and lost his life!.
9. Alipotofautiana na Mhariri Sunday Citizen, Sakina Datoo, Sakina lost her job and she is nobody now!.
10.Yule Mzungu Sarah Harmitage alimsema vibaya kumuunganisha katika sakata la 'Silvadale Farm', she has lost everthing and lost all the cases!.

Kuna watu ukiwatibua, utaishia ku loose!.
Mifano hai ipo!. Sasa ni zamu ya Prof. Muhongo!. Msubirieni tuu, siku zake zinahesabika!.
Pasco.
 
hivi Mengi sio CCM?
Ni kada wa CCM na tawi lake lilikuwa Kisutu kabla hajahamia Moshi. Ila pia dada yake toka nitoke ni mama mzazi wa kiongozi fulani wa siasa anayemuita mjomba!. Ni mfadhili mzuri wa CCM kwa mkono wa mbele ila pia humfadhili mjomba kwa mkono wa nyuma!. Ni kama Sabodo ila yeye sio kiwaziwazi!.
 
Kuna watu wa "powers" kama ma Sharifu!. ukimtibua akakasirika, its a gone case!.
1. Alipoanzisha ITV akatishiwa na DTV. Mmiliki wa DTV Shabir Dewji aliswekwa 'ndani!'. Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani wakati huo, Silvanus Adel 'alimwaga unga!'.
2. Kwenye ule 'mchezo mchafu' wa Kilimanjaro hotel, Masilingi alipayuka sana!. Kapoteza ubunge na kapoteza uwaziri he is nobody now!.
3. Alipogombana na Masha, Masha kapoteza ubunge, kapoteza uwaziri, he is nobody now!.
4. Alipogombana na Rostam Aziz kwa kumuita 'Fisadi Papa!' na alipomjibu yeye ni 'fisadi nyangumi!', Rostam kapoteza ubunge, kapoteza biashara zote, kaikimbia nchi!. Kampuni zake zote zinapumulia mashine!.
5. Alipozozana na Yusuph Manji, Hivi sasa Manji anaelekea kufilusika!. Ameuza kila jengo limebaki jina tuu!.
6. Kile kipibdi cha 'Kiti Moto' kilikuwa OK kilipokuwa Channel Ten, Mzee alinirubuni tukakihamishia ITV kwa 'dau kubwa!'. Alipotaka kuingilia 'contents', tulitofautiana!. Kipindi kilikufa mpaka leo niko juu ya mawe!.
7. Alipotofautiana na Tido kuhusu Kombe la Dunia na UK premier league!. Tido alipoteza kazi!.
8. Alipotofautiana na Mhariri Mkuu wa Guardian, Vumi Urasa, he lost his job and lost his life!.
9. Alipotofautiana na Mhariri Sunday Citizen, Sakina Datoo, Sakina lost her job and she is nobody now!.
10.Yule Mzungu Sarah Harmitage alimsema vibaya kumuunganisha katika sakata la 'Silvadale Farm', she has lost everthing and lost all the cases!.

Kuna watu ukiwatibua, utaishia ku loose!.
Mifano hai ipo!. Sasa ni zamu ya Prof. Muhongo!. Msubirieni tuu, siku zake zinahesabika!.
Pasco.

Hiyo namba 6 ungetumia lD yako ile ingine hii ya JF unawafumbua wabaya wako.
 
Kifupi mkuu wageni wanathaminiwa nchi hii zaidi ya wazawa
 
Pasco, Pasco, Pasco ha ha ha ha
Nimecheka saana, nami niongeze kidogo hapa
....alipomnyang'ang'anya kijana bint mrembo na kumzalisha kijana akalalama, kajikuta kawa wakala wa kusafirisha na kuuza SEMBE
 
Dk. Mengi (kwa madai yake) inabidi aache usanii wake wa kutumia neno uzalendo kwa ajili ya maslahi binafsi. Mzalendo ni yule anaedai haki kwa faida ya jamii na si haki binafsi na kujiita mzalendo. Wako watanzania luluki ambao wangependa kupewa hivyo vitalu vidogo vidogo vya madini lakini hawana deposit ya kufanya matakwa yao yawe uhalisia.

Hapo swala si kuwa serikali aina malengo na mtanzania isipokuwa ni huwezo wa kuwekeza tulio nao watanzania wengi, ndio sababu yeye kwa financial, connection and his status in the social kaweza kuwa na vitalu luluki vya madini bila ya kuviendeleza maana kuvi secure is one thing to utilize them is another (mpunga and the risk factor comes into play).

Kama kashindwa kuvitumia vitalu vyote vya madini yeye mwenyewe hataweza kweli kwenye gesi. Amna anaebisha ya kuwa anao huwezo wa kupata mkopo au kupata mmbia wakigeni lakini huko sasa tunatoka nje ya azma ya uzalendo na kufanya zoezi lote ni la opportunity and life chances ambazo mtu anaweza zipata kutokana na nafasi yake katika jamii. Kwa sababu si yeye tu bali vigogo wengi wa biashara can do the same but for their personal gain na si kwa sababu za kizalendo.

Unlike the government kuingia ubia na mwekezaji ambapo serikali uchukua large chunk of the business stake kupitia shares na taxes plus controlling the direction of the business strategy. Mwekezaji binafsi kutokana na huwezo wake mdogo especially kwenye gesi sidhani kama anaweza ingia ubia na kubaki na more than 30% of the stake kutokana na usawa wa capital invested na watafuta soko.

Kwa maana hiyo the so called mzalendo wa Dk. Mengi, will never make major decisions on the company na kuwapa nguvu wawekezaji namna ya kufanya biashara, sasa hapo kitalu atakuwa alipewa mtanzania au mgeni kupitia mgongo wa mtanzania ambae anafaidika yeye na familia yake tu huo ndio uzalendo kweli?
 
Tatizo ni kwamba wengi wetu tunakurupuka na kuwabeza watu kama Mengi. Mengi yuko TPSF, hakuchaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kuwa tu ni tajiri. La hasha! Kachaguliwa kwa kuwa anakubalika na kuheshimiwa na wafanyabiashara wenzake ambao ndio wanachama wa TPSF. Si haba!

Tatizo la watu wengi ni kutanguliza maslahi binafsi; hususan watendaji wakuu wa Serikali. Wanaona bora waje Wazungu, ambao kwa kweli ni madalali. Hata Zitto Kabwe ameshaliona hili na amelizungumzia kwa undani, jinsi hawa matapeli wanavyokuja, wanatumia pesa kidogo kupata leseni za utafutaji madini (Prospecting Licence), ambapo wakishazipata wanaziuza kwa bei mbaya. Mfano hai ni Sutton Resources, iliyotumia Dola za Kimarekani 20,000 kuipata P/L hiyo, ambayo baadaye ikaiuza kwa bei mbaya kwa Barrick Gold, kwa thamani ya Dola za Kimarekani 348 MILIONI! Kama si wizi wa mchana ni nini hiki?

Leo kwa kuwa mnamuona Mengi kuwa fisadi, ati anamiliki vitalu 49 vya madini (si mlete huo ushahidi?), mnaona ni bora waje hao wazungu-koko, wapewe mikopo, waanze biashara, huku wao wenyewe ni hohe-hahe kuliko sisi!

Tunapoambiwa Tanzania ni Shamba la Bibi, washamba ni sisi wenyewe, na Bibi ni yule Mzungu-koko anayekuja kuwekeza ilhali mfukoni hana hata shilingi!
 
Last edited by a moderator:
Ng'wamapalala hoja ya msingi hapa si watanzania kutomuelewa Prof. Muhongo kwakuwa wamezoea viongozi wanaofanya kazi kwa ufanisi wa chini. Muhongo ameshindwa ''ku-walk the talk'' kama alivyobainisha mzalendo Mzee Mengi kwamba sasa Prof. Muhongo anabugia matapishi yake, bila shaka ameshaonjeshwa unga wa ndele hadi amekengeuka ghafla kiasi hiki.

Nchi haina sera ya gesi asilia na ndio tupo kwenye mchakato wa kutengeneza sera hiyo sasa hii haraka ya Prof. Muhongo kugawa vitalu vingine vya gesi kabla hatujawa na sera ya gesi ni kudhihirisha kuwa uprofesa wake hauna faida wala manufaa yoyote kwa watanzania na nchi ya Tanzania kwa ujumla wake.

Prof. Muhongo amesha mess up sasa anachofanya ni kutumia uprofesa wake kutishia ubabe dhidi ya wananchi wanaojitambua na wanaojaribu kuhoji uzalendo wake ambao bila shaka uko mashakani kutokana na vitendo vyake na kauli zake.
 
Last edited by a moderator:
Dk. Mengi (kwa madai yake) inabidi aache usanii wake wa kutumia neno uzalendo kwa ajili ya maslahi binafsi. Mzalendo ni yule anaedai haki kwa faida ya jamii na si haki binafsi na kujiita mzalendo. Wako watanzania luluki ambao wangependa kupewa hivyo vitalu vidogo vidogo vya madini lakini hawana deposit ya kufanya matakwa yao yawe uhalisia.

Hapo swala si kuwa serikali aina malengo na mtanzania isipokuwa ni huwezo wa kuwekeza tulio nao watanzania wengi, ndio sababu yeye kwa financial, connection and his status in the social kaweza kuwa na vitalu luluki vya madini bila ya kuviendeleza maana kuvi secure is one thing to utilize them is another (mpunga and the risk factor comes into play).

Kama kashindwa kuvitumia vitalu vyote vya madini yeye mwenyewe hataweza kweli kwenye gesi. Amna anaebisha ya kuwa anao huwezo wa kupata mkopo au kupata mmbia wakigeni lakini huko sasa tunatoka nje ya azma ya uzalendo na kufanya zoezi lote ni la opportunity and life chances ambazo mtu anaweza zipata kutokana na nafasi yake katika jamii. Kwa sababu si yeye tu bali vigogo wengi wa biashara can do the same but for their personal gain na si kwa sababu za kizalendo.

Unlike the government kuingia ubia na mwekezaji ambapo serikali uchukua large chunk of the business stake kupitia shares na taxes plus controlling the direction of the business strategy. Mwekezaji binafsi kutokana na huwezo wake mdogo especially kwenye gesi sidhani kama anaweza ingia ubia na kubaki na more than 30% of the stake kutokana na usawa wa capital invested na watafuta soko.

Kwa maana hiyo the so called mzalendo wa Dk. Mengi, will never make major decisions on the company na kuwapa nguvu wawekezaji namna ya kufanya biashara, sasa hapo kitalu atakuwa alipewa mtanzania au mgeni kupitia mgongo wa mtanzania ambae anafaidika yeye na familia yake tu huo ndio uzalendo kweli?

Mkuu naona umeji contradict sana,labda urudie kuisoma post yako mara mbili tatu then utapata picha!hata hivyo je unajua nini hasa azma ya usiri wa mikataba mibovu ya gesi?unajua kua moja ya vyanzo vya mabilion yaliyofichwa Uswiss ni hii mikataba yenye usiri ya gesi?rejea kuna thread humu ilikua inaelezea ilo na ilichambuliwa kwa ufasaha na Zitto Kabwe
 
Kaka, ingesaidia kama ungenieleza where my contradiction lies. Halafu tuache tabia ya kujumlisha factors that could be eliminated when looking at matters of national interest. Gesi ina soko kubwa sana kwa nchi za europe kwenye matumizi ya "ndani ya nyumba" therefore kwa nchi kama tanzania na serikali ya sasa rushwa will play apart kwakuwa it is a commodity of high interest for those who wish to play part.

Hivyo tukichacharika hata kusema one of the opposition parties ndio wangekuwa madarakani, business decisions have to be made on our natural resources. Kwa sasa kutokana na huwezo wa serikali njia mbadala ya kuanza kutumia utajiri wetu ni kwa kutumia wawekezaji ambao wana mitaji, experience and established markets already. To me that is a sound argument as a strategy, namna mikataba inavyo kubaliwa na tunavyoingia is a matter of public scrutiny sibishi hoja hiyo na kuna haja ya uwazi if we are getting value for the exchange of external investment.

Kuhusu hoja ya wazalendo they will not do anything otherwise the government is not doing considering the nature of the sector. Isipokuwa hapa ni wao ndio watakao faidikia kwakuwa serikali in normal circusmtances faida yake ni yetu sote na hela urudi kwa jamii kwa namna moja au nyingine. On other hand kwa mwekezaji binafsi ni utajiri wake ambao kutoa ni kwa mapenzi yake, one thing for certain his bank account is bound to bulge. Kwa maana hiyo kwakuwa fulani ana huwezo na influence anataka to forsake our income for his gain in the name of uzalendo huko ndio kutufanya sisi wajinga (Dr. Mengi, is a one trick pony).

Nadhani tuachane na ushabiki hapa na tuangalie nyendo za hawa matajiri wetu, kusema eti Mozambique are doing ABC therefore it will also be good for us ni uzandiki, maana hatujui motive of their politicians. Hila the fact remain the same almost everywhere in africa natural resources walipopewa wazawa hawakufanya chochote tofauti na serikali, isipokuwa ndio chanzo cha mabillionare wetu kwa kushirikiana na wazungu as individuals. Si ndio maana Angola leo kuna matajiri wakubwa na wote wako serikalini kisa sera hizi hizi za uzalendo uchwara, who knows what Mozambique leaders are scheming.
 
Mkuu naona umeji contradict sana,labda urudie kuisoma post yako mara mbili tatu then utapata picha!hata hivyo je unajua nini hasa azma ya usiri wa mikataba mibovu ya gesi?unajua kua moja ya vyanzo vya mabilion yaliyofichwa Uswiss ni hii mikataba yenye usiri ya gesi?rejea kuna thread humu ilikua inaelezea ilo na ilichambuliwa kwa ufasaha na Zitto Kabwe

si hivyo tu, kunauwezekano mkubwa hao wanao kataa mikataba kuwekwa hazarani wakawa na hisa humo, wao wenyewe kwa majina yao au jamaa zao kwa kuwa wakilisha.
 
Mbona sijaona alipojibu tuhuma za vitalu 59 kama ni kweli alivichukua na hajaviendeleza, Aisee mwambieni meku kuwa kula chakula na walemavu haiwezi kumkingia ufisadi kama hata-come clean. Mwambieni atuelezee hivyo vitalu alivyohodhi ameviendelezaje? Huku kutlia kwake kutukumbusha kuwa anakulaga na walemavu sisi tutamuona kama msanii tu.

Miongoni mwakazi za serikali yoyote duniani baada ya kazi ya ukombozi wa utawala wa wakolono,halihii ya ukombozi imepitiwa karibu na nchi zote duniani,kazi kubwa na yamuda mrefu kwa serikali iliyopo madarakani ni kuwawezesha wananchi wake kiuchumi,kisiasa na kijamii halihii wananchi hawakuweza kuipata chini ya utawala wa wakoloni,suala lilinalozungumziwa ni hili la kiuchumi,serikali ya chama cha Tanu na badae chama cha mapinduzi ilifanyakazi kubwa na nzuri ya kuung'oa utawala wa kikoloni katika nchi hii,na kipindi kirefu cha zaidi ya miaka 50 imeshindwa kusimamia maendeleo ya watanzania kiuchumi,kero lukuki katika kiwango cha elimu yetu,kiwango duni cha matibabu,kipato cha mtanzani kisichotosha chini ya dola mmoja(Mhe Kinana akutana na mabango ya wananchi kudai maji) hizi ni dalili tosha za serikali kushindwa kusimamia uchumi wa watanzania.wawekezaji kutoka nje wamewezeshwa na nchi zao kauli kama za mhe profisa Muhongo hazikupewa nafasi katika nchi za jamii zinazo jali maendeleo ya raia wake,hivi nikweli viongozi wetu wanakerwa na umasikini wa watanzania.
 
Mengi amfyatua Muhongo
• ASEMA NI MWONGO, MPOTOSHAJI KUHUSU UWEKEZAJI WA GESI
na Mwandishi wetu
MWENYEKITI Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wameingia katika mzozo mzito kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi.
Katika mzozo huo, Mengi amemshambulia Waziri Muhongo kwa kumwita ni mwongo, mpotoshaji na mwenye lengo la kuwatoa Watanzania kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yao ya gesi.
Mengi alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini.
Mzozo wa vigogo hao ulianza wiki mbili zilizopita baada ya Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), kukutana na waandishi wa habari na kueleza msimamo wa taasisi hiyo katika suala la uwekezaji wa gesi nchini.
Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa majadiliano zaidi.
Baada ya ushauri huo, Waziri Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba uko palepale kama ulivyopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Prof. Muhongo pia alitamka bila kumng'unya maneno kwamba hana mpango wa kukutana na TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda, na kuongeza kuwa uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta ya gesi.
Septemba 7, mwaka huu, mzozo huo uliingia katika hatua mbaya zaidi baada ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la ‘CCM Tanzania', kusambaza taarifa kwa njia ya barua pepe kwa vyombo vyote vya habari na kumshambulia Mengi kwa kumwita fisadi, mbinafsi na mfitini wa maendeleo.
‘CCM Tanzania' kama anavyojiita, alidai katika barua pepe yake kuwa Mengi amepanga kuwatumia vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya kongamano lenye maudhui: ‘Rasilimali za nchi na manufaa kwa wazalendo.'
Alisema kongamano hilo limepangwa kupewa muda maalumu na Kituo cha Televisheni cha ITV kinachomilikiwa na Mengi na lengo lake ni kutaka kuionesha jamii kuwa Waziri Muhongo na watendaji wengine wa wizara hiyo hawajali masilahi ya wazawa na hawana utaifa wala uzalendo.
‘CCM Tanzania' alisema si mara ya kwanza kwa sekeseke la aina hii kuzuka ama kuzushwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mengi na mara zote amekuwa akitumia nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari anavyovimiliki katika kutafuta kuungwa mkono na hata kuonesha ubaya wa wabaya wake.
Akijibu tuhuma hizo kupitia taarifa yake jana, Mengi alisema Septemba 7, mwaka huu, alipokea barua pepe yenye kichwa cha habari kisemacho: "Ubinafsi/ufisadi wa Mengi na chuki/ fitna kwenye maendeleo."
Alisema aliyetuma barua pepe hiyo ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, alijitambulisha kama ‘CCM Tanzania' na aliisambaza kwa vyombo mbalimbali vya habari, wanasiasa na watu wengine wa kada mbalimbali.
"Kabla ya barua pepe hiyo, nilifowadiwa pia nakala ya ujumbe (sms) na watu ambao walitumiwa na Prof. Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na mbunge inayosema:
"Wambieni Watanzania: Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya madini vyenye ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km) amevishikilia, ameshindwa kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka vitalu vya gesi na mafuta. Je, huu ndio uzawa?
"Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya rasilimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu," alisema.
Mengi katika taarifa yake hiyo, aliendelea kusema kuwa mbali ya Waziri Muhongo kutuma ujumbe huo, vilevile Septemba 5, alijibu kwa dharau swali la mwandishi wa habari lililouliza:
"Waziri tunataka ufafanuzi kuhusu kauli yako ya hivi karibuni kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika uwekezaji wa gesi asilia. Kwanza, kauli hii ni kweli? Pili, kauli kwamba Watanzania wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya machungwa tu, huoni si kwamba unawavunja moyo bali unawadhalilisha wawekezaji wazalendo?"
Alisema kuwa Prof. Muhongo alijibu: "Kila mtu alitoa mawazo ya sera ya gesi wakiwamo TPSF. Mengi na wenzake wanataka vitalu wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta yetu. Tutatoa orodha ya vitalu vya madini vilivyoko mikononi mwa Mengi ambavyo anafanya ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na ulanguzi wa Mengi wa genge lake."
Mengi alisema ameona ni bora atumie haki yake ya kujibu na kuwaonya wanaohusika kusambaza taarifa hizo kuchafua jina lake, wajue kwamba atawachukulia hatua za kisheria.
Kuhusu kusingiziwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi, alisema huo ni upotoshaji na uongo wa hali ya juu wa Waziri Muhongo, wenye lengo la kuwatoa Watanzania kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yao ya gesi, kwani hajawahi kufanya udalali kwenye vitalu vya madini.
Alisema tamko la TPSF, lilitokana na kikao cha bodi ya taasisi hiyo cha Agosti 28 na baadaye kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Alisema mambo mengi yalizungumzwa katika kikao hicho, ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa Watanzania (Economic Empowerment) na mambo muhimu matatu yalijadiliwa na kutolewa mapendekezo.
Mengi aliyataja mambo hayo kuwa ni kuhusu manunuzi ya umma (public procurement), ardhi na uvuvi na tatu, ni suala la gesi asilia.
"Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mimi nikiwa Mwenyekiti wa TPSF, niliwasilisha maoni ya TPSF kuhusiana na manunuzi ya umma, wakati Makamu Mwenyekiti wangu, Salum Shamte, aliwasilisha maoni yetu kuhusiana na sekta ya ardhi na uvuvi na mwishoni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, aliwasilisha maoni ya TPSF kuhusiana na gesi asilia.
"Katika maoni yetu, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji wa vitalu vya gesi hadi hapo sera ya gesi itakapokuwa tayari. Mwisho, Bwana Simbeye alisema kwamba TPSF itaomba kukutana na Profesa Muhongo kuwasilisha mawazo na mapendekezo ya taasisi hiyo," alisema.
Kwa mujibu wa Mengi, matokeo yake Prof. Muhongo hajajibu hoja na badala yake alitoa majibu ya kumshambulia mwenyekiti huyo.
"Binafsi nilishitushwa na msimamo wa Prof. Muhongo, kwani Serikali ya Awamu ya Nne imepiga hatua kubwa katika kudhihirisha kuwa ni "serikali sikivu". Ingemgharimu nini Prof. Muhongo kukaa na kutusikiliza? Hakuna ambacho angepoteza zaidi ya dakika chache za muda wake.
"Jambo la pili ambalo lilitokea ni mimi binafsi kushambuliwa kana kwamba maoni yaliyotolewa kuhusiana na gesi ni maoni yangu binafsi na si ya TPSF. Mifano ya mashambulizi dhidi yangu ni kama nilivyoonyesha hapo juu katika email na ujumbe mfupi wa simu (sms)," alisema.
 
Back
Top Bottom