Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.
.
Mkuu kama umemsoma vizuri Zitto alichomtaka Mwandosya ni kuwaeleza WANANCHI juu ya tuhuma zile, badala ya Mwandosya kutoa maelezo kwa wananchi yeye aliichukulia kama Personal attack kwake! Na ukimsoma Mwandosya utaona kabisa kwamba alikuwa akitoa maelezo na majibu kumshusha Zitto kwanza, huku akijitenga na lawama zozote zinazohusiana na Ubinafsishaji ama kuanguka kwa mashirika hayo wakati hoja haikuwa Ubinafsishaji bali Usimamizi na Utekelezaji wa mashirika yale.
Mwandosya kama mgombea Urais hakutakiwa kabisa kujibizana na Zitto bali angeyachukulia maswali yale kama msingi wa kujisafisha ili arudishe imani ya wananchi.. Ndio maana nasema kuwa Profesa na Mwanasiasa ni mambo mawili tofauti maana mmoja ni mtaalam mwingine ni mtumishi wa watu. Mwanasiasa siku zote unawakilisha watu, Kila unalozungumza linawahusu wananchi na maslahi yao mbele ya kila kitu. Mtaalam unatazama vitu kisayansi kabla ya watu..
Zitto kasema ameridhika ili kuondoa wingu lilokuwepo na kumpa heshima yake Prof. Lakini wanaotakiwa kupima ni nyie wananchi kama majibu ya Mwandosya yanatosha au laa. Zitto sio hakimu wa kuwahukumu wagombea Urais bali ametoa hoja ambazo hawa wagombea kama wajanja wataanza kufanyia kazi majibu ili wakichaguliwa wataweza vipi kukabiliana na maswali hayo..
Duh mkuu wangu sijui kama umenielewa kwa sababu umeenda nje kabisa unapolihusisha Bunge maana mtu anapoelekeza swali kwa Speaker ni utaratibu ambao hauna maana mbunge hamuulizi Speaker swali vile vile. Zitto kataka maelezo ya mwandosya kuhusiana na tuhuma zinazosambaa na maswali kama haya huwa kawaida kabisa ktk uchaguzi.Umenishangaza sana kiongozi. Hoja yoyote inajibiwa kwa aidha maneno uite waandishi ama uitishe mkutano uongee kama alivyoonge Zitto. Namna ya pili ni kuandika , katika kuandika lazima maandishi yako uyaelekeze sehemu hasa kwa mwakilishi wa kundi.Kwa kuwa zitto ni Mwanachi katika hao wenye dukuduku anahaki ya kupelekewa ujumbe huo kwa niaba ya wengine kama tulivoupata mimi na wewe. Ukifuatilia bunge utasikia wanaelekeza kwa ndugu speaker, haina maana kuwa spika pekee ndio mwenye interest na hayo majibu
Duh mkuu wangu sijui kama umenielewa kwa sababu umeenda nje kabisa unapolihusisha Bunge maana mtu anapoelekeza swali kwa Speaker ni utaratibu ambao hauna maana mbunge hamuulizi Speaker swali vile vile. Zitto kataka maelezo ya mwandosya kuhusiana na tuhuma zinazosambaa na maswali kama haya huwa kawaida kabisa ktk uchaguzi.
Alichokifanya Mwandosya ni kujikosha yeye huku akimshusha Zitto hasa sehemu za mwisho kwa sababu Mwandosya anasahau kwamba yeye anagombea Urais alitakiwa kujibu tu maswali hayo kadri ya uwezo wake na anavyohusika maanake hizi ni kashfa na watu wanajiuliza. Unapogombea Urais hata kama unaulizwa na mtoto mdogo hutakiwi kumwambia wewe bado mdogo hujui kitu..Hizi ndizo dharau za kina Muhongo naona kama ni kawaida yenu kujikweza wenyewe badala ya kusubiri usifiwe..
pamoja na mwandosha kukanusha baadhi ya tuhuma ukweki ubinafsishaji wa ttcl uligubikwa na rushwa na utata mkubwa na gazeti la rai wakati huo chini ya kina ulimwengu ulionyesha mpaka invoice ambazo motto wa mwandosya alilipiwa na kampuni iliyonunua hisa za ttcl kwanini amechukua muda mrefu kukanusha mwandosya naye hana usafi wa kujiita yeye msafi
Mkandara kama umesoma vizuri utaona sehemu prof anelezea kuwa alishatolea majibu katika kipindi cha uchaguzi kama hiki na kufanikiwa kuingia tatu bora , alicholeta hapa ni summary , ndio maana akamshangaa kijana kwa kutochimba .Kuhusu lugha iliyotumika ni lugha ya sanaa ya majigambo , ukumbuke kuw Prof anamfahamu huyu na huyu anamfaham mwenzie na malengo yake ya kumharibia ndio maana ametumia hiyo lugha ili amtie hasira kama ana hoja aje -ni dhana ya kuonesha unavyojiamini-Isingekuwa busara prof ajishushe kwa kiumbe arrogant kama zzk
Kaka huyo dno Zitto, kaja na tuhuma za kusikia na kajibiwa kwa maneno rahisi naya kaelewa. Ndio Jembe hilo. Ila kama unafuatiloia kuna video yake akinadi chama chake cha ACT-Wazalendo alisema kama Lowassa anataka kuja kugombea urais kupitia ACT-Wazalendo anakaribishwa awaambie Watz kuhusu fedha zake. Usishangae sana huyo ndo Zitto anaitwa Jembe na baadhia ya mashabiki wake.Nimemshaangaa Zitto, pamoja na sifa anazopata humu kuwa ni jembe ..... binafsi nimekuwa nadoubt!!!
Yeye kama Supremo Leader anakujaje na hearsay kwenye mitandao na kuwatuhumu watu!!? Kama kweli ni jembe kama watu wanavyodai angekuja na concrete issues siyo ya hii oh walidai mtoto wako alisomeswa, au mashirika yalibinafsishwa ukiwa Waziri kwa njia za ufisadi, tueleze!!? Sasa Mwandosya katoa majibu bila hata lots of supporting evidences, Zitto anadai ameridhika.
Sasa Mwandosya kusema kuwa mtoto wake hakusomeshwa na shirika lilishatolea maelezo 2005, kunamrizishaje Zitto!!? Hakukuwa na haja ya Zitto kuja na hizi tuhuma bila kutaja kijana alisomeshwa wapi na malipo ya scholarship yake yalikuwaje!!? Kwa ujumla Zitto aliokoteza maneno ya mitaani na kuyaleta kwenye siasa. Inawezekana yana ukweli ndani yake ila yamekosa uzito!!
Mihemko...Unakosa kuwa objective kwa sababu tu inaonekana una shida/chuki na Zitto
Thubutu hawezi kutukana wakunga na uzazi ungalipo,Mwenye ushahidi zitto akisema lowasa fisadi auweke hapa
nakubaliana na ww rai walikuwa kwenye mtandao lakini zile document za malipo zlikuwa feki au halaliNinachokumbuka pia in kuwa Jenerali ulimwengu na gazeti lake la Rai alikuwa kwenye payroll ya MTANDAO uliomuweka mkulu madarakani. Ukumbuke kuwa Jenerali alitangazwa na serikali ya Mkapa kuwa ni FOREIGNER na wana mtandao wakamnunua KWA ahadi ya kumrudishia utanzania wake. Yeye na akina Salva wakawa busy kuwa-demonise watu wote waliokuwa wan auwezekano wa kupambana na Kikwete kwenye nomination. Kadhia hiyo ilimkumba pia JEMBE Salim Ahmed Salim. KWA hiyo gazeti la RAI was not that impartial and could not be relied on.
Prof. kumshauri huyu jamaa ni kazi kubwa, huwezi, anachoamini yeye ndicho hicho hicho kama huamini maneno yangu naomba mtafute Prof mwezio Lipumba atakupa mkanda mzima kwenye jambo hili. Si wewe tu ni wengi wamechemsha!!Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.
Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"
.
nakubaliana na ww rai walikuwa kwenye mtandao lakini zile document za malipo zlikuwa feki au halali
Mwandosya aendelee kujikalia kimya, strength yake iko kwenye kukaa kimya, sio kuropoka kama hawa wenye matamko kila baada ya nusu saa.
Kwa hali ya CCM ilikofikia, nikiambiwa nichague viongozi wa-3 wenye vigezo visivvyo na shaka hata kidogo vy akuiongoza hii nchi, Jina la Mwandosya halikosekani kwenye 2-bora. The guy is simply too good, too experienced and too damn wise.
Ukiwa na Raisi sampuli za huyu jamaa, you sleep at night knowing the country is in good hands, ila kuna ndugu zangu tia maji tia maji, kutwa kucha kuropoka, hawana substance, hawana akili, hawana weledi, hawana busara. Walischonacho ni Umaarufu tu, kwa ku-manage kuwa controversial long enough.
Mkuu sidhani kama swali letu sisi wananchi ni maamuzi ya kubinafsisha TTCL yalifanywa na nani? bali kina nani walishiriki katika mkataba wa kuwapa shirika la Malaysia kwa bei ya kutupa, maana kitendo cha maamuzi ya kubinafsisha chombo kile sio kibaya kama wangechukua maamuzi sahihi...YES, maamuzi ya kubinafsisha Ttcl yalifanyika kabla Prof hajateuliwa Waziri wa Mawasiliano.
..lakini Prof na mawaziri waliomfuatia ktk wizara hiyo hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kuilinda Ttcl na hujuma zilizofanyika baada ya kubinafsishwa.
cc Mkandara, Kimweri, makoye2009
Mkuu, hivi una akili timamu kweli?
umejibu vizuri kuwa mahakama ndio inajua ufeki au uhalali pia kama mwandosya angeona kakashifiwa angeenda mahakamani kujisafishaUfeki au uhalali ungeweza kuthibitishwa mahakamani. Mimi na wewe tunachoweza kuona ni nyaraka tu zinazowekwa na waandishi wa habari kwa sababu wanazozijua wao. Ninachoweza kusema ni kwamba, zilitumika kupandikiza negative perception kuhusu mhusika, na Rai (na wanamtandao) walifanikiwa kwa hilo.
Kwenye mambo ya propaganda, sometimes waandishi wanaweza wakatengeneza picha, risiti na nyaraka mbali mbali na kutengeneza stori za uongo kwa malengo wanayoyajua wao. Naamini utakuwa umewahi kusoma kwenye gazeti, habari ambazo si za kweli zikiwa front page, halafu,wakikanusha, wanaweka vimaneno kidogo kwenye ukurasa wa ndani, huku wakijua kuwa message ya kwanza ya kwenye front page imewafikia watu wengi zaidikuliko ile ya kukanusha. Ni mbinu chafu tu ambazo huwa zinatumika. Na kipindi kile zilitumika sana na wanamtandao.