Majibu ya mke wangu haya hapa

Majibu ya mke wangu haya hapa

Buzi Maarufu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2019
Posts
422
Reaction score
330
Alishaapa kamwe hatanisaliti,lakini Kila nikifanya uchunguzi naona hamaanishi anachokisema.

Mwezi huu anaenda kwao kusherehekea krismasi na mwaka mpya, leo hii katika stori za hapa na pale nikachomekea neno, Mke wangu unaenda kwenu utakaa mwezi mzima, Ma Ex wako wawili ninaowafahamu wapo kule chondechonde usiende kuwapa tunda,amejibu...Sitatoka nyumbani mpaka siku nitakaporudi huku, Kwahiyo sitoweza kuonana nao, nikauliza,Je haiwezi ikatokea bahati mbaya mkaonana?

Akajibu hapana haiwezekani, nikamwambia wao wanaweza wakakuona wakamtuma mtu kwako au kuomba namba ya simu, akajibu.,..hapana hawawezi kufanya hivyo, Baada ya majibu haya nikagundua mke wangu ni dhaifu sana hana msimamo ndio maana ananiambia atakaa nyumbani tu ili asionane na hao watu, tafsiri yake ni kwamba akionana nao wakamuomba uporo hawatawanyima, baada ya majibu hayo nimemsisitiza sana ikitokea akaonana nao na wakamuomba tunda basi ajitahidi asije akacheka mechi pekupeku.

Sasa yeye kakasirika eti simwamini nahisi yeye ni malaya Kwahiyo hataenda kwao,tusaidieni katika hili jamani Nani mwenye kosa kati yetu?nilitarajia ataniambia anajiamini na hata akionana nao hatakuwa na muda nao lakini majibu yamekuwa kinyume na matarajio yangu.
 
Back
Top Bottom