Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Majibu ya baadhi ya maswali yenu

Joined
Apr 20, 2013
Posts
15
Reaction score
424
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).

  1. Private messages ya TAYADI, tarehe 11 Juni
Kazi unaweza saaana!,, lakini Kwa hili la GHOROFA, Mafisadi wameiweka serikali pamoja na mama Tibaijuka MFUKONI. Hakuna anayefurukuta. Jengo litaendelea kuwepo tu!

Jibu. Asante kuona naweza ila nikuhakikishie sijawekwa mfukoni na mtu. Ila mwenye jengo kaenda mahakamani na kapewa injunction. Kesi ipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, Miscellaneous Land Application No. 42 of 2013. Tarehe 31 Mei, 2013, Mhe Jaji J.S. Mgeta alitoa amri ya kulinda status quo baada ya Bw. Mashauri, Mwanasheria wa Halmashauri ya Ilala (ambayo imeshitakiwa), kutopinga ombi la Bi. Rachel, Mwanasheria wa Mwekezaji (Ali Raza Investments Ltd), kwamba wakati kesi kuu ikisikilizwa jengo lilindwe. Mchakato wa kisheria unaendelea tukipata maamuzi tutawajulisha. Mbali ya taarifa hiyo, kwa mujibu wa sheria, siwezi kujadili zaidi jambo lililo Mahakamani. Tusubiri.


  1. Private Message ya Amani Ndoyella, ya 11 Juni, 2013
Ujumbe wako kuhusu Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mrefu ila kwa ufupi, unalalamika kuwa wananchi hawashirikishwi katika maamuzi, watendaji wamenipotosha, fidia ya Shs milioni 141 kwa ekari ni ndogo wakati unadai mwekezaji atalipa Shs milioni 300 kwa eka, unataka wananchi mmojammoja waingie ubia, unalalamika sijwawahi kufika Kigamboni kukutana na wananchi kwa hiyo niliyoyasema Bungeni siyo sahihi. Unakiri nilikutana na Kamati yenu lakini pia unadai hamsikilizwi, Mwisho unailalamika kamati yenyewe, nkd.

Jibu: Kupanga miji ni kazi ngumu, inahitaji uzalendo. Ni changamoto na kero kwa wahusika wote. Ushirikishwaji umekuwepo tangu mradi ulipoanza mwaka 2008 ila tukubali umechelewa na hii ni changamoto. Mimi binafsi nimefanya mikutano mikubwa ya hadhara Kigamboni miwili, mbali na kukutana na Kamati ya Madiwani, Wabunge, na hata Kamati huru kama ile ya kwenu. Wananchi wamechagua wawawikilishi wao katika KDA, wakala wa Serikali kuu itakayoendesha mradi. Ofisi za KDA ziko huko huko Kigamboni. Mkurugenzi wake Bw. Vincent Shauri anapatikana hukohuko kujibu hoja zenu. Tunatambua usumbufu lakini na sisi tunajitahidi kutekeleza kazi hii kwa manufaa ya umma hasa vizazi vijavyo. Miji yetu ikiharibika hata na uchumi na maisha haviwezi kuwa bora.
Niliporejea kutoka Singapore, kwenye ziara ya Mhe. Rais, nilileta kwenye mtandao huu Master Plan ya mji mpya wa Singapore. Wengine hawakuelelwa mantiki ya post hiyo, hata wakadiriki kukebei kwa nini ninawasumbua?. Nilitaka kuonyesha kwamba adha za upangaji miji siyo Dar es Salaam tu, hata haya majiji yalioyoendelea sana kama Singapore yanapangwa upya kadri ya maendeleo yanavyosonga mbele (urban renewal programs). Utamaduni wa kulalamika hausaidii sana lakini utamaduni wa kujadili ni mzuri na ndiyo umuhimu wa jukwaa hili la JF. Kwa hiyo kuhusu Kigamboni nifafanue tu kwamba fidia tuliyotaja ni endelevu na mchakato wa kutoa malipo kwa wananchi wa Kibada unaendelea. Madai ya Shs milioni 300 kwa ekari ni uongo, na mwenye ushahidi mwambie akuonyeshe. Niliyoyasema Bungeni ni sahihi, ninakushukuru kwa kufuatilia.
Mwisho amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa hiyo tuilinde. Tujiepushe na kauli za kutishia uvunjifu wa amani, hazina tija. Hoja tu ndiyo jambo la msingi.
 
Ahsante
mama japo umejibu kwa bla bla,suala la kubomoa ghorofa halihitaji
usubiri hukumu ya mahakama we unatakiwa ufanye kazi zako kwa kufuata
sheria.kiujumla serikali imelemewa na mafisadi mmebaki kuwaonea na kuwagandamiza wananchi wa chini wasio na feha.mama kwakuwa we ni mjumbe wa cc ya ccm utakapokuja kujibu maswali mengine nami naomba utueleze chama kina mpango gani wa kuwawajibisha mwigulu,Nape,na wasira kwa kuendesha siasa za kimafia na kibaguzi nchini.
 
umejibu maswali mawili tu tena uliyotumiwa kwa PM,
zingatia sheria za JF mtu anapokutumia private msg.
 
Ahsante mama japo umejibu kwa bla bla,suala la kubomoa ghorofa halihitaji usubiri hukumu ya mahakama we unatakiwa ufanye kazi zako kwa kufuata sheria

Mimi siyo mwanasheria. Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mimi siyo mwanasheria.
Hivi angeweza kuendelea kubomoa kama yule kafungua kesi hata kama
alijenga kwa kukiuka sheria ya ujenzi pamoja na kibali alichokuwa
amepewa cha ghorofa kumi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

naamini mpaka alipofikia uamuzi wa kubomoa aliona zipo sheria na kanuni alizoona zimekiukwa na hazikufuatwa ambazo yeye kama waziri anatakiwa azisimamie.court injunction kwa issue kama hii hamzuii yeye kuendelea kufanya kazi zake.
 
Mukaile kilinjwi hukujibu vizuri swali la Kigamboni. Tunaomba kujuzwa picha inakamilika lini, ili tujue hatima yetu?
 
Wanamtandao

Ninawashukuru wote ambao kwa mda mmeelekeza masuala na matukio mbalimbali kwangu. Niombe radhi kuchelewa kujibu kwa sababu ya shughuli zilizokuwa zinatukabili. Sasa nimepata nafasi kidogo, nitajibu baadhi ya mambo ambayo naona ni ya haraka zaidi, na yanafaa kujadiliwa hadharani. Private messages nyingine nitazijibu moja kwa moja (bilaterally).
Mheshimiwa waziri;
Hivi hakuna sheria za ku-deal na mambo ya dharura na hatari kama hili la jengo? Nauliza kwa sababu INASEMEKANA hilo jengo lilijengwa chini ya viwango na kwa kukiuka vibali kama lile lililobomoka! Sasa kweli tuhatarishe maisha ya watu kwa sababu ya kusubiri kesi iliyofunguliwa mahakakamani, tena mfunguaji mwenyewe ni mtu huyo huyo ambaye ameshaua watu kwa uzembe anaotetea?
 
Mheshimiwa waziri ukipata nafasi naomba unijibu hili.
Mheshimiwa mbunge mwenzenu kada wa CCM, Bwana JUMA NKAMIA alisema kwenye mahojiano na televisheni ya Taifa TBC1 kuwa mtandao wa JF ufutwe kwani ni mtandao ambao hauna sifa ya kuitwa mtandao wa kijamii kwani unaandika uwongo na mambo ya kufikirika na utashi wa mtu.
Mheshimiwa wewe ni member wa JF, unafikiri alichosema kada huyo ni sahihi? nini ushauri wako kweke?
 
Mi nakupongeza sana kuithamini JF na hivyo kuja kutolea majibi yako hapa. Ila nisisitize tu kitu kimoja, kwamba wwnanchi wengi wanakosa subira na maneno matupu. wanataka kuona mambo dhahiri shahiri. Harakisheni kigamboni watu tujue hatma yetu ya maisha kwani kwa miaka yote hii hatufanyi maendeleo kule kwasababu yenu.
 
kwahiyo hiyo mahakama itazuia gorofa kuporomoka?
maana kusudio la kuvunja ni kwasababu lipo chini ya kiwango. Tuache siasa

kabisa,yeye kama waziri anatakiwa afanye kazi zake ili kuepusha maafa ya baadae.
 
Mheshimiwa,

Naomba niulize swali moja dogo tu kupanga miji kisheria na kuweka utaratibu wa kutaka activities fulani zifanyike na zengine zifanyike kule kunahitaji gharama kiasi gani? Mfano jiji la Dar-es-Salaam ambalo halina plan ya msingi mnashindwa kweli kuwaambia wakaazi wa kariakoo mfano kufanya biashara zao maeneo ya ilala na magomeni kuondoa foleni mjini. Mkaishinikiza serikali ofisi zake za mawaziri na taasisi zengine isipokuwa TRA, Bandari na Benki Kuu zikabakia mjini nyengine zote zikahamia maeneo ya mwenge, ubungo na manzese kusambaza vitega uchumi maeneo hayo? Finally mjini kukabadilishwa na kuwa na taasisi za kifedha, mahoteli, shopping malls tu ili kupunguza foleni na vile vile kuleta urban tourism.

Kama ni ngumu sana basi tuajiri sie tukushauri vp ufanye ili kuleta faida ya taifa letu na maendeleo kwa ujumla.
 
Mama Anna Tibaijuka mambo niaje! Majibu uliyoto inaonesha unaheshimu sana Rule of Law, Nakupongeza kwa hilo. Mh waziri mkuu, ambaye ni msomi wa sheria, amesema "kama wanakataa kutii sheria wapigeni"? Tunafahamu Police wameruhusiwa kutumia reasonable force to control situation, Mama najua umeishi sana nje, umeshuhudia case nyingi za police brutality ambazo zinaongeza uhasama katika jamii na kuwapa mwanya wahalifu. Nini msimamo wako kuhusu kauli ya Mh Pinda? Je huu ndio utawala wa sharia? Je hauoni aibu kuwa mmoja ya viongozi katika serikali inayoongoza kimabavu?
 
Tatizo la viongozi wa nchi hii na wasomi wetu hawaishi kulalama je tutafika kwa mtindo huu
 
Tunashukuru Mama Anna Tibaijuka kwa kutujuza yale yanayoendelea kuhusiana na AMRI uliyoitoa ili jengo libomolewe.

Hii ndiyo nguvu ya mawasiliano katika dunia ya sasa ambapo sentensi ya mistari SITA inayochukua less than two minutes kuiandika imeondoa SINTONFAHAMU iliyokuwa inaelea hewani kwa muda kuhusiana kile kilichoko nyuma ya jengo kutobomolewa.

Jaribu kuwashauri na watendaji wengine wa chama na serikali hasa mawaziri kujiunga na Jamiiforums ( JF) ili wasogee karibu kwa wananchi katika kupashana habari na kuelimishana.
 
Mheshimiwa waziri;
Hivi hakuna sheria za ku-deal na mambo ya dharura na hatari kama hili la jengo? Nauliza kwa sababu INASEMEKANA hilo jengo lilijengwa chini ya viwango na kwa kukiuka vibali kama lile lililobomoka! Sasa kweli tuhatarishe maisha ya watu kwa sababu ya kusubiri kesi iliyofunguliwa mahakakamani, tena mfunguaji mwenyewe ni mtu huyo huyo ambaye ameshaua watu kwa uzembe anaotetea?
mmhh!!!! hapana jamaa angu mama kaeleza vizuri sheria zetu hizi tunazitunga wenyewe na kuzisimamia, jengo lilindwe kwa maana lisilete madhara , mimi ningeshauri tu wakati wanalilinda walitegue kidogo kuonyesha soon litaleta madhara . kingine ni kwa nini ichukue muda sana labda kama unavyodai sheria ya dharura. inatkiwa hawa mahakama watambue wanacheza na uhai wa watu. wa kulaumu ni hawa watu wa mahakama kama wamehongwa ndiyo issue sasa
 
Ikitokea jengo hilo likaanguka (Mungu aepushe mbali) serikali tuiweke upande gani? Hili jengo ni la siku nyingi,mlishindwa vp kupeleka mswada wa kuirekebisha hyo sheria kipind cha bunge la bajet?
 
Vyema sana prof tibaijuka. Umefanya jambo jema wakati muafaka
 
Mama Tibaijuka, kidumu chama cha mapinduzi. Nikupe ongera kwa ujasili wako wa kuja kutolea majibu humu jukwaani, ukizingatia kwa vuguvugu la ushindani lilivyo kwa sasa, nikupe hongera.

Lakini kuhusu jengo pale mtaa wa Indra Gadhi, Posta. Sidhani kama pingamizi lililo tolewa lina tija, ukizingatia hali ya usalama kwa wakazi wa eneo husika bado si shwari, watu hawana amani na wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru.

Mimi nadhani jengo livunjwe haraka iwezekanavyo, harafu mahakama kuu kama chombo cha kusimamia na kutoa haki, tuone itahamua nini. Haya ni maisha ya watanzania tunayangelea hapa, hatuwezi kuendelea kuyahatarisha kwa pingamizi la mtu mmoja au kikundi cha watu kwa kulinda maslahi yao.
 
Back
Top Bottom