Majibu ya awali ya tume ya kuchunguza sababu za kufeli vijana wa form4 ( 2012)

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,698
1,395
nimeicopy kutoka sehemu......
TUME YA MH. PINDA INATIA WASIWASI Jana Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa
Sifuni Mchome alidokeza baadhi ya
sababu zilizotolewa kwa wingi na wadau
wa elimu waliihojiwa mpaka sasa. Sababu hizo ni ukosefu wa walimu,
upungufu wa vitabu na mazingira duni ya
kujifunzia. Mwanzo huu sio mzuri hata
kidogo. Hizo sababu zinajulikana siku
zote, walimu wote wanazijua, na wizara
inazitambua. Istoshe hizo ni baadhi ya sababu zinazoathiri ufundishaji na
ujifunzaji shuleni. Je, hizo ndizo sababu
kuu za wanafunzi kufeli kwa wingi kiasi
hiki? Wakiendelea hivi; watajikuta wanarudia
yale yale ambayo walishaambiwa miaka
nenda-miaka rudi na kukataa, ama
kupuuza. Hivyo ni muhimu kwa Tume
hiyo kuja na maelezo ya kina na
uchambuzi utakaosaidia Taifa hili. Sababu hizo walizoanza kuzitaja,
zinapatikana kwenye kitabu cha takwimu
za elimu (BEST)-wala haikuwepo haja ya
kwenda kuziuliza kwa wananchi na
wadau wa elimu. Ni heri waendelee
kuchambua-ili wadau waje wapate ripoti kamili kuliko kuanza kutoa hizi taarifa
zisizojitosheleza.
 
Ndugu sasa wewe unataka majibu gani??

kama wao wameenda kufanya utafiti na wamepata majibu hayo unataka wafanyenini? wayabadilishe? eti kwa sababu yamezoeleka?? au unataka waweke majibu unayoyadhania wewe kama 'NECTA waliwafelisha wanafunzi???

acha kuanza kulaumu, ni kweli hizo ni sababu za muda mrefu zinazofanya elimu yetu kuwa duni, je zimefanyiwa kazi??? kama hazijafanyiwa kazi basi matokeo yatakuwa mabaya zaidi na zaidi? na tutaishia kupoteza hela kwenye kuunda tume za uchunguzi

binafsi naamini kama hayo ndio majibu ya tume basi tujipange upya, we unfikiri kama mazingira ya kufundishia na vifaa vitakuwa vizuri unafikiri wanafunzi watafeli??/
 
Siasa tupu. Dharau za Serikali, Jamii dhidi ya Walimu ndo imetufikisha hapa kwa kiwango kikubwa ingawa zipo changamoto zingine.
 
Ndugu sasa wewe unataka majibu gani??

kama wao wameenda kufanya utafiti na wamepata majibu hayo unataka wafanyenini? wayabadilishe? eti kwa sababu yamezoeleka?? au unataka waweke majibu unayoyadhania wewe kama 'NECTA waliwafelisha wanafunzi???

acha kuanza kulaumu, ni kweli hizo ni sababu za muda mrefu zinazofanya elimu yetu kuwa duni, je zimefanyiwa kazi??? kama hazijafanyiwa kazi basi matokeo yatakuwa mabaya zaidi na zaidi? na tutaishia kupoteza hela kwenye kuunda tume za uchunguzi

binafsi naamini kama hayo ndio majibu ya tume basi tujipange upya, we unfikiri kama mazingira ya kufundishia na vifaa vitakuwa vizuri unafikiri wanafunzi watafeli??/

mkuu gango2 hapo juu nimekuandikia kabisa ''NIMEICOPY KUTOKA SEHEMU" so usinitolee povu mimi....
Nimeipaste hapa ili sisi kama wadau wa elimu tujadili na si vinginevyo...
 
Last edited by a moderator:
HII tume siikubali kwa kuwa, hata haya majibu ya awali, tunayajua. Nasubiri, kama kuna, majibu mapya.
 
tume = pesa
zingine mbwebwe tu
ukitarajia majibu kutoka kwenye tume tena ambayo si ya bunge, utakufa kwa presha tu.
chuku chako mapema.
 
Back
Top Bottom