Je hili ni tatizo la client ama contractor?Nashindwa kuweka post kwa sababu bado naona kuwa huu ni wizi tu na sijui ni nani alaumiwe; $1.2m ni nyingi sana kwa ujenzi wa nyumba hizo nilizoona sehemu mbalimbali. Tatizo la nchi yetu ni kuwa watu hangalia bei za nyumba huko Marekani na kuzitumia kupanga bei za hapa Tanzania!!
Hapo juu nimekufahamu...
Nimekufahamu kuwa tatizo hapa ni Ndulu na sio gharama za ujenzi. Kama ndio hivyo basi sina swali lingine unless otherwise kama hukubaliani na gharama za ujenzi huo.
Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.
Sawa sawa kamanda, pamoja na mfano wako mzuri ambao unaonyesha jinsi gani usanii unaweza kufanyika. Nilichokifahamu ni ushiriki wa Nduli tokea mwanzo wa project hiyo. Hata hivyo hii haina maana kuwa gharama hizo sio sahihi.Sasa mzee mie sikufahamu unataka kutwambia nini mie nimejaribu kukupambanulia kuwa huo ndio usanii wenyewe umesema hauoni. Hembu chukulia mfano wewe unateuliwa kuwa rais wa kampuni, halafu wewe ndio mhasibu wa kampuni halafu wewe ndio msimamizi wa kampuni who will held who accountable for his/her action??? Ukijibu swali hili nadhani utaelewa kwanini watu wanalalamikia 1.4 Billion otherwise inawezekana tunakipigia gitaa but wewe mwenyewe umeziba masikio
Ningependa kuuliza kaswali kama kuna wajenzi humu ukumbini. Hivi leo nikitaka kujenga nyumba ya kisasa pale Tanzania, yenye vyumba vitano, sebule mbili, jiko ya kisasa, ikiwa na air conditioning na matenki ya maji safi itanigharimu kiasi gani? Achilia mbali bwawa la kuogelea kwa sababu tupo karibu na pwani nitaogelea pale Coco Beach. Tuseme viwanja Oyster Bay na Masaki havipatikani, basi kule Boko.
Sawa sawa kamanda, pamoja na mfano wako mzuri ambao unaonyesha jinsi gani usanii unaweza kufanyika. Nilichokifahamu ni ushiriki wa Nduli tokea mwanzo wa project hiyo. Hata hivyo hii haina maana kuwa gharama hizo sio sahihi.
Taarifa hiyo imeweka bayana jinsi project hiyo ilivyoondesha tokea hatua za awali hadi kupatikana kwa mjenzi. Iwapo gharama za ujenzi huo zitakuwa zimepangwa na BOT wenyewe na sio Wazabuni, basi hapo kuna ulazima wa kulalamikia hizo bilioni. Iwapo gharama za ujenzi zilipangwa na Wazabuni na kukubalika na client sioni kama kuna tatizo hapo.
Hilo ni neno jipya kwangu, una maana ya Quantity Surveyor?Mkuu, wazabuni hata siku moja hawapangi gharama. Gharama zinapangwa na mshitiri pamoja na washauri wake.
Fundi M.. hivi kuwawekea vyumba vya wageni kwenye nyumba za watumishi ni kwanini? Hivi Dar-es-Salaam hakuna hoteli za kufikia wageni? au ni wageni gani hawa ambao Benki Kuu inawafikiria kufikia kwa Gavana wao..?
Ndio maana nasema "ngojeni" kwani wamefanya kosa lile lile lakini Nguba kujibu kwa kutoa takwimu!
Hilo ni neno jipya kwangu, una maana ya Quantity Surveyor?
Kuna tofauti yoyote na ile mikataba ya awali ya viongozi hao?Kwa mujibu wa mikataba yao.
Swala Je, kwa gharama gani?Tunaambiwa iliamuriwa kujengwa
Jamani hizi nyumba kweli zilikuwa magofu? Salaleee tena zilikuwa huko Osterbay?Nyumba zilizokuwa huko zilikuwa ni magofu yaliyopigwa marufuku kuishi binadamu
Nyie ngojeni tu..
Tumeshangoja sana - ngoja ngoja huumiza matumbo!
Na wabunge wako wapi kwenye hili? Kuna hata mmoja aliyelitolea tamko? kupeleka bungeni kujadiliwa? and is this outrage only on the internet? what about on the ground?
Mwanakijiji,Fundi M.. hivi kuwawekea vyumba vya wageni kwenye nyumba za watumishi ni kwanini? Hivi Dar-es-Salaam hakuna hoteli za kufikia wageni? au ni wageni gani hawa ambao Benki Kuu inawafikiria kufikia kwa Gavana wao..?
Ndio maana nasema "ngojeni" kwani wamefanya kosa lile lile lakini Nguba kujibu kwa kutoa takwimu!