Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

Nchi yetu inageuzwa Animal Farm. Mbaya zaidi, Mzee Mwanakijiji haya matumizi yanatumika kununua second/third rate stuff kutoka majuu. Sisi tunachotaka ni kuwa kitu kimeagizwa kutoka nje bila kujali au kujua quality!

Amandla......

mbona tayari nchi yetu animal farm longi tu.
ingawaje sasa hivi ndio idadi ya wananchi wanaotambua
hali hiyo inazidi kuongezaka
 
Mbona NHC wanauza nyumba mpya wanazojenga nzuri tu na kwa bei poa. Kwa nini wasinunue hizo kama kweli wana shida.

MB1.V.jpg
MB2.V.jpg

http://www.nhctz.com/construction.htm
 
Swali jingine ambalo tungependa tuwaongezee kwa vile wao wamelileta ni hili: Ni watumishi wangapi wa BoT ambao kwa mikataba yao wanatakiwa wapewe nyumba? Impression waliyoiacha ni kana kwamba katika BoT ni hao watatu tu ndio wanatakiwa kupewa nyumba. Since they opened up the box.. let's look inside!
 
Reverend,

Why do you want to swallow your own vomit? Few days ago, you adamantly defended BOT's decision to build those houses solely because it's not tax payers' money. Now, you want to turn around and accuse them of the same thing you did defend them before. This is simply the zenith of hypocrisy. ......Sorry Reverend, you can't have both ways.

Those were not taxpayers money! Hiki ni kichekesho cha hali ya juu. Hebu tuambie mwenzetu ni lini BoT wameanza kuwa na shamba la kuvuna mapesa yao wenyewe badala ya kuendeshwa na pesa za walipa kodi? ili na sisi tukavune katika hilo shamba la bibi.

Nchi hii imeoza kuanzia Ikulu na taasisi zote nyingine muhimu TAKUKURU, Mawizara yote na kinachosikitisha zaidi ni kwamba pamoja na kuoza kwa nchi yetu bado kuna watu wanataka kutetea uozo uliokithiri kila mahali na kuona eti Kikwete anastahili miaka mingine mitano ya kuisambaratisha zaidi nchi.
 
Reverend,

Why do you want to swallow your own vomit? Few days ago, you adamantly defended BOT's decision to build those houses solely because it's not tax payers' money. Now, you want to turn around and accuse them of the same thing you did defend them before. This is simply the zenith of hypocrisy. ......Sorry Reverend, you can't have both ways.

Alikuwa anatania huyo. Kama ulimsoma vizuri teh teh teh
 
Swali jingine ambalo tungependa tuwaongezee kwa vile wao wamelileta ni hili: Ni watumishi wangapi wa BoT ambao kwa mikataba yao wanatakiwa wapewe nyumba? Impression waliyoiacha ni kana kwamba katika BoT ni hao watatu tu ndio wanatakiwa kupewa nyumba. Since they opened up the box.. let's look inside!

Waweke mkataba wa ajira ya Ndullu na hao manaibu wengine hadharani tuone kama kuna kipengele cha kupewa nyumba zenye thamani ya $1,000,000.

Hawa watu wanajisahau kama wanaishi Tanzania wanataka kuishi maisha ya fahari kubwa wakati asilimia kubwa ya Watanzania wako hoi bin taabani kwa maisha ya dhiki yanayosababishwa na sera na Viongozi wabovu kila kukicha. Ufujaji wa pesa kuanzia Ikulu na kila kila taasisi ya serikali na hiyo CCM chama twawala.
 
Tanzania ni gari bovu kweli kweli, hatuwezi hata kumwajibisha kiongozi yeyote hata akifurunda vipi.

Inawezekana kabisa kuwa Mheshimwa Ndulu (siyo profesa kwa sababu hafundishi chuo kikuu) hana makosa, hata hivyo ni lazima akubali kuwa kuna makosa yalifanyika na kama kuna mtu mwingine aliyefanya makosa hayo basi amwajibishe.

Hii bla bla ya mikataba, tenda na upumbavu mwingine havisadii kutujengea imani kwa taasisi hii inayotunza mapesa mengi sana ya walipa kodi na imekuwa inakumbwa na kashfa nyingi tu za matumizi mabaya ya mapesa hayo.
 
Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Hii inatisha kweli. Benki Kuu wanakuwa na nyumba ambayo wanaiachia hadi inakuwa gofu! Ni magofu mengine mangapi ambayo bado wanayo?
Na hayo magofu yanatumika na watu au yako matupu? Na ni hatua gani walichukuliwa wale walioachia nyumba za Taasisi hii muhimu zifikie hatua ya kuwa condemned? Au walinunua condemned buildings kwa zile dola 400000 tulizoelezwa awali?

Majibu ya haraka haraka yana matatizo yake.

Amandla......

Reverend,

Why do you want to swallow your own vomit? Few days ago, you adamantly defended BOT's decision to build those houses solely because it's not tax payers' money. Now, you want to turn around and accuse them of the same thing you did defend them before. This is simply the zenith of hypocrisy. ......Sorry Reverend, you can't have both ways.

Rufiji,

On my posting before defending BOT descision, I had asked the same question! Suala si kula matapishi, bali ni watu kushindwa kujenga hoja na wewe kama si Wacha au yule jamaa mwingine mkadai najifanya machinoo!

Mimi nilisema, ni haki kwa BOT kujijengea nyumba, kutokana na bajeti yake, lakini hapo hapo nikauliza kwa ujumla, kwa nini mfumuko huu wa bei haudhibitiwi?

I am not a hypocrit, and I wish you extend an apology.

Go back and read the whole thread on BOT and see what I stated before kuniita mnafiki!
 
Hii inatisha kweli. Benki Kuu wanakuwa na nyumba ambayo wanaiachia hadi inakuwa gofu! Ni magofu mengine mangapi ambayo bado wanayo? [/FONT]Na hayo magofu yanatumika na watu au yako matupu? Na ni hatua gani walichukuliwa wale walioachia nyumba za Taasisi hii muhimu zifikie hatua ya kuwa condemned? Au walinunua condemned buildings kwa zile dola 400000 tulizoelezwa awali?

Majibu ya haraka haraka yana matatizo yake.

Amandla......

ndio maana binafsi mimi ningependa sana kujua hivyo viwanja vilivyokuwa na condemned buildings vilikuwa vya shemeji yake na nani?
 
Nani kakwambia BOT walinunua kiwanja ? Hivi viwanja vilikuwa mali ya BOT . Hizo shilingi bilioni 2.5 ni za kujenga nyumba mbili tuu !

Rufiji,

Sizungumzii kuhusu viwanja vya Benki Kuu, nazungumzia soko la viwanja na ardhi Tanzania nzima! Nilishasoma BOT walichosema kuwa ni viwanja magofu.

Kama unakumbuka, niliuliza kwenye ile thread ingine, gharama za ujenzi Tanzania na eneo lilipojengwa nyumba hizi!
 
two issues

From spinning point of view BOT wamechelewa kwani issue ishapita zaidi ya 5 working days hivyo tayari ishafika stage ambayo ni ngumu kuireverse

From the response point of view naona BOT hawakujua kuwa their target should have been JF members ambao if anything huwa wanawarahishia waandishi wetu uchwara kazi ya kutafuta maswali ya kuwauliza kwani Kishoka et al washawafanyia .

If anything majibu ya hawa BOT hayajitoshelezi kwani hawajasema :

kwenye Pre-qualification hao waliokuwa shortlisted walikuwa shortlisted kwa vigezo vipi na waliokosa walikosa kwa vigezo vipi

Ingekuwa si vibaya wakaweka wazi BOQ original na sio lile lililokuwa linabadilishwa siku ya Jumamosi

Mwisho naona its about time waka outsource hii kazi ya PR kwa private companies kwani naona ma spin doctors wao bado wako enzi za 'CHEKOS---SLAVIKIA'...kwani huwezi ukawa na DISASTER prone institute kama BOT ambayo if anything maskendo yake yamekaa ki 21st Century halafu unataka kuleta solutions za 20th Century.

This wont work...considering NDULU alivyoingia kwa mikwara ya kutokaa kwenye ofisi na ile pethous iliyojengwa na Balali au kuwapakiza wafanya kazi kwenye MINI BUS kwenda Dodoma kisa? eti kuonyesha he's different from Marehemu Balali!

Haya kiko wapi?
 
ndio maana binafsi mimi ningependa sana kujua hivyo viwanja vilivyokuwa na condemned buildings vilikuwa vya shemeji yake na nani?

Wameishasema kuwa vilikuwa ni mali yao. Sasa kwa vile BOT hawana mandate ya kufanya biashara ya makazi, nyumba zao zote ni kwa ajili ya matumizi yao na si kufanyia biashara. Kwa hali hiyo basi yale magofu yalikuwa yanatumika kama makazi ya watendaji wao. Hii ina maana waliyaacha bila matengenezo hadi yakifikia hali ya kuwa condemned ( bila kutuambia nani aliyetoa hukumu hii. Manispaa ya Kinondoni?) kama makazi. Kwa vile bila shaka BOT ina nyumba nyingine basi ingekuwa vizuri kama wakitufahamisha zina hali gani maana haiwezekani kuwa ni hizi chache tu zilizoachiwa zifikie hali hiyo! Inabidi tujue taratibu zao na bajeti yao kwa ajili ya matengenezo maana hata hizi zisipofanyiwa maintenance hazitakawia kuwa magofu na itabidi wauziwe wanaozitumia kwa bei ya kutupa!

Amandla.......
 
Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Mimi siko kabisa kwenye gharama ya ujenzi maana nimeshindwa hata kushangaa karibu 1.5Bil kwa nyumba si mchezo, nipo kwenye yanayoitwa magofu, wao wanayaita magofu sisi tunaziita nyumba, ni kufuru kupita kiasi.
Sikatai Gavana kuwa na nyumba nzuri ila napinga zile nyumba zilizobomolewa kuitwa magofu, kwa maana hiyo asilimia 90 ya watanzania tunaishi kwenye magofu maana ni wengi hatuna nyumba kama zilizobomolewa, ningekuwa na picha zake kabla ya kubomolewa ningewawekea.
 
You must have something wrong in your brain kufikiri kwamba a 1 million dollar (US $) house ni kitu cha kawaida kwa mtumishi wa serikali especially in TZ. In reality hata president wa Tanzania hastahili nyumba yenye gharama hiyo.

Hiyo reply ya BOT inataka kutuaminisha kwamba contractors ndio waliopanga bei, na wao wakachagua yule wa chini. Hivi yule wa chini angekuwa $5 mil. angepewa tu kwa sababu ni chini?

Halafu kwa mtu yeyote anayefahamu taratibu za tendering in TZ na tena huko huko BOT sio rahisi kuamini maelezo yao kwamba hakukuwa na michezo michafu.

Maswali ya kizushi,

1. Hii kampuni Eletrics International Co. Limited mbona imekaa kimazabemazabe well labda wadau mnaoifahamu lakini kwa sababu ni bongo si vibaya kujiuliza nio kampuni ya nani, imewahi kufanya miradi gani mingine, na hapo BOT imewahi kufanya kazi ngapi? Inaweza kuonekana ni kupersonalize the issue lakini history tells me kuna haja ya kujua.

2. Ndulu ameshahamia kwenye nyumba hiyo? Na kabla ya hapo alikuwa anakaa wapi?

3. Liyumba anayedaiwa kwamba aliidhinisha majengo pacha, hakuhusika na hii isije mwishoni mambo yakiwa moto karushiwa tena Liyumba. Mind you mradi wa karibu $450mn jamaa wamemmbebesha Liyumba wht about this $1ml?
 
Mimi siko kabisa kwenye gharama ya ujenzi maana nimeshindwa hata kushangaa karibu 1.5Bil kwa nyumba si mchezo, nipo kwenye yanayoitwa magofu, wao wanayaita magofu sisi tunaziita nyumba, ni kufuru kupita kiasi.
Sikatai Gavana kuwa na nyumba nzuri ila napinga zile nyumba zilizobomolewa kuitwa magofu, kwa maana hiyo asilimia 90 ya watanzania tunaishi kwenye magofu maana ni wengi hatuna nyumba kama zilizobomolewa, ningekuwa na picha zake kabla ya kubomolewa ningewawekea.

Nishasema katika Thread nyengine kuwa Professor Mervin King anakaa katika nyumba ina thamani ya £420,000, Professor Ben Benarke $549,000 Professor wetu anakaa nyumba ya $1.2 Million unadhani huyu jamaa akienda na rais kuomba pesa watampa kweli, unafikiri hawa jamaa mabalozi wao hawasomi magazeti!!!!
 
Unajua, Mkuu, tunajidanganya kuwa dola moja hapa kwetu ni sawa na shilingi moja. Dola milioni moja kwa hiyo ni sawa na shilingi milioni moja! Lakini nje, dola ni dola! Kwa hiyo Benarke anakaa kwenye nyumba ya milioni zaidi ya 600 na hii ya kwetu ni kamilioni kamoja!

Amandla.......
 
Mie natamani aje ofisa uhusiano wa BOT humu JF tutete nae au ikiwezekana aje Ndulu mwenyewe tuzungumze nae maana hii haijakaa sawa. Wasitutolee matangazo ya vitisho na jeuri wakifikiri vichwa wako BOT tu bongo sasa hivi Masters za economics kibao tena za vyuo vya kimataifa, PhD nazo zinaongezeka kila siku sasa watutolee matangazo yaliyoenda shule na sio kutishana tishana na mikwala kibao!!!!
 
Back
Top Bottom