Gavana Tutuba: Maisha Hayajawahi Kuwa Rahisi tangu mwanadamu alipoumbwa, fanyeni Kazi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Emmanuel Tutuba amewataka watu wanaodai maisha ni magumu wafanye kazi kwani hakuna mwaka maisha yamewahi kuwa rahisi.

Gavana Tutuba ameelezea kwamba Hali ya Uchumi wa Nchi ni nzuri na inaendelea na Ukuaji mzuri.

My Take
Ambao wamewahi kuwa na maisha Mepesi waje watuletee ushuhuda.

===
Alichokisema Gavana,

"Hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri, kama mnavyofahamu kwenye robo tatu zilizopita uchumi ulikua kwa wastani wa kama 5.2%. Tunatarajia takwimu rasmi zitakapotoka kwa hii robo ya mwisho, tunaamini lile lengo la 5.3% linawezekana likawa limefikiwa kabisa. Na kama mnavyojua mfumuko wa bei umeendelea kuwa wa chini wa around 3% ambayo bado ni asilimia inayoruhusu ukuaji mzuri wa uchumi. Na unaendelea kuweka mfumo wa kutunza thamani ya fedha kuwa nzuri.

Sasa kinachotakiwa ni kila mmoja kutumia fursa hiyo katika kufanya kazi. Na wengine nimewasikia wakisema maisha yamekuwa magumu. Kimsingi maisha hayajawahi kuwa rahisi. Tangu Mungu alivyoumba dunia, alivyomuumba mwanadamu alisema nenda kale kwa jasho, kwa hiyo hakuna siku maisha yalikuwa rahisi. Kinachofanyika ni serikali kuweka fursa zinazomuwezesha kila mmoja atumie fursa hizo kwa namna yake yeye mwenyewe ili aweze kufanya maisha yake yawe rahisi. Kwanza kwa kufanya kazi halali ili apate kipato halali. Kikiwa kipato kikubwa, kitamuwezesha yeye kufanya shughuli zake. Maana katika uchumi huwa tuna cartegorize watu katika yale makundi manne.

Kuna wale watu ambao kipato chao ni kidogo kuliko matumizi yao, yaani total income inakuwa ni less than total consumption. Maana yake anaishi chini ya ule mstari wa umasikini. Na ya pili ni ile total income inakuwa sawa na total consumption. Sasa yale ni makundi ambayo mapato yao ni madogo kuliko matumizi. Sasa wao pia wanatakiwa kuangalia, fursa zinazowazunguka maana sisi kama Benki Kuu kupitia sera ya fedha tunachofanya zaidi ni kuweka mfumko wa bei uwe wa chini, kuhakikisha mzunguko wa fedha uendelee kuwa mzuri. Kuhakikisha pawepo ujazi wa fedha wa kutosha kwenye uchumi, kuhakikisha kama ni mabenki na watoaji wa mikopo wengine wawe na hizo fedha ili kutoa mikopo yenyewe. Ili kuwezesha wenye nguvu na utashi wa kufanya kazi, akafanye kazi.

Lakini kuna wale ambao tunaenda kwenye level ya tatu ambao, inakuwa total income ni sawa na total consumption plus savings. Ile ni ngazi ambayo wakidhi huduma na kuwawezesha kuishi, na aweze kupata akiba yaani savings. Sasa hao wana fursa zaidi ya kuendelea kupata faida kwasababu yeye anafanya vitu hayuko kwenye pressure, anachofanya ni kuangalia fursa ili atumie ile fursa kupata faida zaidi. Na kuna wale wengine ambao total income ni sawa na total consumption plus savings plus investments/reinvestments. Hao sasa ni wale matajiri ambao hao bado kwa serikali hii ya mama Samia ya Awamu ya sita, tunaona imerahisisha mazingira ya ufanyaji biashara lakini imeweka mazingira wezeshi ya kila fursa ya kiuchumi...."

Theories, Kuna jamaa namjua, graduate wa chuo kama 5 years, alikuwa na kazi ya mkataba ikaisha, kazungusha cv, mpaka kachoka, alikuwa anataka kufungua Saloon, ana mke anapambana.

Jamaa wa watu akaja anataka mkopo wa 5m, nikamwambia naweza na wala sitamdai riba, ila aniweke kwenye kadi ya gari yake na alipaki, akileta hela, nampa gari.

Jamaa alipambana kweli, akawa anarejesha, baada ya mda, umeme shida, na majukumu, akashindwa kabisa kulipa kodi na deni.

Mwishowe, kaomba auze gari, anirudishie hela, nikampa gari kauza kwa hasara, kaweza rudisha 4m, nikashukuru angalau imerudi, nikamsitiri.

Alibakiwa na 2m, nayo kaimaliza yote, yupo huko anafanya kazi kiwandani ya dhoruba analipwa 250,000 a month, na 5000 overtime hata kama atatoka saa 6 usiku.

Nashangaa sana mtu akisema swala la kufanya kazi kwa bidii, kuna watu wanafanya sana kwa bidii ila maisha yamewagomea katu katu.
 
Kweli kabisa hata wakati wa Kikwete walisema maisha magumu kuna ufisadi mwingi...alipotoka Tu ndo wakasema vyuma vimekaza...kumbe wakati wa Kikwete vyuma havikuwa vimekaza??...hata sasa ndo hivyo hivyo akitoka Samia ndo utasikia kipindi cha Mama...maisha yalikuwa nafuu sana
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Emmanuel Tutuba amewataka watu wanaodai maisha ni magumu wafanye kazi kwani hakuna mwaka maisha yamewahi kuwa rahisi.

Gavana Tutuba ameelezea kwamba Hali ya Uchumi wa Nchi ni nzuri na inaendelea na Ukuaji mzuri.

My Take
Ambao wamewahi kuwa na maisha Mepesi waje watuletee ushuhuda.
Amesema kweli. Pamoja na mapungufu yalipo upande wa Serikali kushindwa kutengeneza fursa za kutosha, ila nchi yenyewe ina fursa nyingi sana hiyo. Imagine nchi kama Tanzania kuwa na uhaba wa Nyanya, vitunguu nk halafu watu wanalalamika maisha magumu, kweli?
 
Kweli kabisa hata wakati wa Kikwete walisema maisha magumu kuna ufisadi mwingi...alipotoka Tu ndo wakasema vyuma vimekaza...kumbe wakati wa Kikwete vyuma havikuwa vimekaza??...hata sasa ndo hivyo hivyo akitoka Samia ndo utasikia kipindi cha Mama...maisha yalikuwa nafuu sana
Exactly
 
Mifumo ya maisha haikubali kwa kila mtu.

Siku fulani nilikuwa ofisi moja nasubiria huduma, akapita Rostam Aziz bila salamu. Kaingia ofisi ile ile ambayo mimi nasubiria kuingia maana kulikuwa na mtu mwingine kwa wakati huo. Bwana Rostam akaambiwa asubiri, akaja kukaa pale nilipokuwa nimekaa, akasalimia 😆 nikaitikia kisha nikamwambia lakini nilikusalimia wakati unanipita kuelekea ofisini haukunijibu.........akaomba radhi kisha akasema daaah! Maisha magumu mno brother~hela ngumu inapatikana kwa taabu mno!

Sikumjibu lolote zaidi ya kuguna huku nikijisemea moyoni ,kama Rostam anasema maisha magumu akina sisi tusemeje?

Ni kupambana tu hakuna kukata tamaa. Gavana yupo sahihi
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Emmanuel Tutuba amewataka watu wanaodai maisha ni magumu wafanye kazi kwani hakuna mwaka maisha yamewahi kuwa rahisi.

Gavana Tutuba ameelezea kwamba Hali ya Uchumi wa Nchi ni nzuri na inaendelea na Ukuaji mzuri.

View: https://www.instagram.com/reel/C4vZDbeuPwI/?igsh=MWlyMW41dnYyaHc4ag==

My Take
Ambao wamewahi kuwa na maisha Mepesi waje watuletee ushuhuda.

Mwambie Gavana atuoneshe zilipo dolla
IMG_2081.jpeg
 
Kweli kabisa hata wakati wa Kikwete walisema maisha magumu kuna ufisadi mwingi...alipotoka Tu ndo wakasema vyuma vimekaza...kumbe wakati wa Kikwete vyuma havikuwa vimekaza??...hata sasa ndo hivyo hivyo akitoka Samia ndo utasikia kipindi cha Mama...maisha yalikuwa nafuu sana
Hata kipindi cha Magu mlisema hivyo hivyo,nimegundua kitu kuhusu wewe jamaa,chuki yako kwa yule jamaa ni udini tu
 
Back
Top Bottom