Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
i156_1262250542nyumbayagavanawabot.jpg

Nyumba ya Gavana Ndulu iliyoibua utata

MASWALI YA LULA WA NDALI (RAIA MWEMA)

KULA MLE KUULIZA TUSIWAULIZE?

BENKI Kuu wanataka kula tena; wanataka kula bila kuulizwa na yeyote; wanataka kula huku tukiwatazama. Si huku tunawatazama tu bali wanataka wale huku tukiwapigia makofi kwa jinsi gani wanakula vizuri.

Habari kuwa Benki Kuu imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu kujenga upya nyumba ya gavana wake ni habari za ulaji mwingine kwenye taasisi hiyo ulaji ambao walaji wake hawataki waulizwe!

Habari hizi zilizoripotiwa na gazeti moja la kila siku nchini zinadokeza kuwa Benki Kuu imetumia fedha hizo katika kumpatia Gavana wa Benki hiyo Profesa Benno Ndulu jumba la uhakika linaloendana na hadhi ya Gavana (wa Tanzania). Ingawa habari hizo zilidai kuwa fedha hizo zilitumika katika ukarabati siku chache baadaye gavana mwenyewe alijitokeza na kudai kuwa fedha hizo (au zaidi) hazikutumika katika ukarabati kama gazeti hilo lilivyodai bali zilitumika katika ujenzi mpya wa jumba la Gavana.

Ndullu alinukuliwa kudai kuwa "Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema" na hivyo kuhalalisha matumizi hayo ya fedha. Lakini zaidi alionekana kuchukizwa kwa kupatikana kwa habari hiyo akidai kuwa "Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli, kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu kizuri na kujengwa taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi. Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa".

Gavana Ndulu hakutaka kusema gharama halisi ya ujenzi wa jumba hilo ni kiasi gani na ni kwa nini ni kiasi hicho. Katika kufikiria suala hilo nimejikuta tena napigwa na bumbuazi la aibu; bumbuazi lililoniacha na maswali mengi kuliko majibu yake. Nilikuwa ninaamini kuwa mambo haya yalikuwa yanatokea wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa lakini sasa tunayashuhudia katika utawala wa Jakaya Kikwete na sitashangaa mwaka huu mmoja uliosalia tutaona mambo makubwa sana ya "ukarabati" hadi tunyofoe nywele zetu!

Ninajiuliza:

  1. Profesa Ndulu amesema kuwa walichofanya si ukarabati bali ni ujenzi wa jumba jipya kabisa. Ningependa kujua kabla ya ujenzi wa jumba hilo eneo hilo lilikuwa na nyumba ya aina gani na kwa nini ililazimika kuvunjwa? Jibu hili ni muhimu kwani tusipoangalia wakuu wa taasisi mbalimbali watakapopewa majumba ya waliowatangulia nao watataka kujenga majumba mapya. Hivyo, ningependa kupewa jibu kwa nini Gavana wa BoT alihitaji jumba jipya?
  2. Kwa vile jumba hili linadaiwa kugharibu zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu Gavana Ndulu anaweza kutupatia mchakato wa gharama za ujenzi wa jumba hili kiasi cha kuhalalisha matumizi makubwa ya fedha kiasi hicho?
  3. Fedha zilizotumika zimetokana na mfuko gani? Swali hili ni muhimu kwani tangu habari hizi zimevuja kumekuwa na mjadala mkubwa wa fedha zilizotumika ni za walipa kodi au ni za Benki Kuu wenyewe na haziko katika usimamizi wa umma? Kama jawabu ni kuwa ni fedha za walipa kodi ni utaratibu gani ulitumiwa kuhalalisha hasa tukizingatia kuwa Gavana wa Benki Kuu ndiye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo? Na kama ni fedha za "benki kuu" kama baadhi ya watu wanavyoamini tunajuaje kuwa mchakato wa matumizi yake hauna mazingira ya kifisadi?
  4. Kutokana na swali hilo hapo juu, hatuna budi kujiuliza kama Benki Kuu yetu ilivyo sasa haina tofauti na Benki Kuu ya Dk. Daudi Ballali? Mojawapo ya matatizo tuliyoyashuhudia wakati wa Gavana Ballali ni uwezo wa Gavana yule kuhalalisha malipo na matumizi makubwa ndani ya benki hiyo kwenda kwa makampuni hewa na hivyo kuwa sehemu ya ufisadi mkubwa. Je, Gavana Ndulu kwa kuhalalisha matumizi haya anaweza kuelezea kuwa yanaendana na thamani kweli ya ujenzi wa jumba hilo na kwamba uchunguzi huru ukifanyika utahalalisha matumizi hayo?
  5. Je, Gavana Ndulu yuko tayari kufungua vitabu vya Benki Kuu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) au mkaguzi wa nje atakayeteuliwa na CAG kupitia mahesabu ya mapato na matumizi, hususan kwenye suala hili la ujenzi?
  6. Katika kufanya hilo hapo juu, je, Gavana Ndulu anaweza kutuambia kuwa ujenzi huu wa hili jumba ulifanywa na kampuni gani iliyofanya hivyo kwa kushinda tenda gani iliyotangazwa lini na yenye vigezo gani?
  7. Je, Benki Kuu inaweza kutuambia kuwa jumba hilo lililojengwa kwa fedha za Watanzania (ziwe zinazotokana na kodi yao au mtaji wao kwenye benki hiyo) lilitumia kiasi gani cha vifaa, ufundi, utaalamu, samani n.k kutoka ndani ya nchi yetu au ni yale yale ambapo hadi vitasa tunaagiza nje, mazuria nje, madirisha nje, makochi na vitambaa vya makochi kutoka nje?
  8. Swali la mwisho ambalo ningependa kujua jibu lake ni kwa Gavana Ndulu kutuhalalishia kwa nini Gavana wa Tanzania akae kwenye jumba lenye gharama inayoshinda jumba la Gavana wa Benki Kuu ya Marekani, taifa kubwa zaidi lenye uchumi mkubwa na lenye matatizo ya kiuchumi ya kutosha tu?
  9. Nina uhakika yapo maswali mengine lakini ningependa tuanze na haya. Napendekeza katika kuonyesha uongozi bora Waziri wa Fedha amwombe CAG kufanya ukaguzi wa haraka wa Benki Kuu hasa kwenye matumizi ya ujenzi na ukarabati wa majumba yao yote na kuona kama taratibu zimefuata na gharama inaendana na kile kilichofanyika au kudaiwa kufanyika (value for money).
  10. Ndugu zangu Benki Kuu haina rekodi nzuri inapokuja kwenye masuala ya matumizi ya fedha zetu; imekuwa ni sehemu ya mtandao wa kifisadi na hadi hivi sasa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuisafisha isipokuwa kubadilisha mapambo tu ya utendaji wa Benki hiyo. Tusipoangalia fedha za Uchaguzi Mkuu kwa chama kimoja nchini zitapatikana tena kwa mtindo huu huu wa ulaghai
Ninachosema ni kuwa mkila tutawauliza, kama hamtaki tuwaulize…

--------------------------------------

MAJIBU YA HOJA ZA LULA KUTOKA BENKI KUU

TAARIFA KWA UMMA

BOTgoldLogo10.jpg

TAARIFA KUHUSU UJENZI WA MAKAZI YA VIONGOZI WAKUU WA BENKI KUU YA TANZANIA

GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008. Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
 
ni break down nzuri na imekaa KITAALAMU!lakini kwanin irushwe leo?
 
Hakuna kitu hapo, bado hayo ni matumizi makubwa mno kwa ajili ya nyumba ya kiongozi mmoja tu kwenye nchi kama Tanzania.

Unaweza kujenga nyumba kama hiyo kwa gharama chini ya bilioni moja.
 
Ikiwa Ben Bernanke mwenye cheo kama cha Ndullu US, nchi mabayo ina uchumi mkubwa sana kulinganisha na Tanzania na pia ni nchi tajiri sana, anajilipia gharama za matengenezo mbali mbali ya nyumba yake kutoka mfukoni mwake badala ya kuwabebesha mzigo huo walipa iwa Marekani, kwanini Ndullu na manaibu wake wasijilipie wenyewe gharama hizo? Kuna mtu aliweka hapa kwamba mshahara wa Ndullu ni mkubwa kuliko hata wa Bernanke. Huu nao ni ufisadi wa aina yake.
 
Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price)

1,274,295,025.26 + 1,272,348,512.00 = ?
nyumba 2 tu, mwee twaliwa.
 
1,274,295,025.26 + 1,272,348,512.00 = ?
nyumba 2 tu, mwee twaliwa.
HELA YA KAWAIDA SANA HIYO!hebu kasome specifications na requirements,EBO!

why are you guys interested in figures?labda mngeshauri wabadilishe DESIGN
 
ni break down nzuri na imekaa KITAALAMU!lakini kwanin irushwe leo?

Ha ha ha mkuu. Si unajua mambo mengi yapo kwenye mafaili mpaka itokee mtu wa kuchoma utambi ndipo yanawekwa wazi?? si unajua tena EPA ilikuwa hivyo hivyo ila ubaya hawakutoa Press Release mapema jambo ambalo lilimfanya kila kiongozi kupayuka kivyake na kuharibu zaidi.

Ila jamani mbona pesa ni nyingi sana hizo?? Nina wasi wasi, hebu wataalam mtusaidie, au tuseme ina bullet and bomb proof, untouchable with mafuriko ya sunami maana itaelea au kuna kipi hapo?? Mbona watu wawili watumia pesa ya kutosha kujenga zahanati, shule na kupatia vitanda au madawati. Sikatai viongozi kuishi nyumba zenye hadhi, bali pia tuangalie hali ya uchumi na umaskini wa watanzania. Pesa yangu ya PAYE na kodi za vitega uchumi vyangu inaniuma kwa namna inavyotumika.
 
Yaani hii ripoti inaumiza kichwa sana, ni kweli uamuzi ulichukuliwa 2006 but the contract to build those two houses were signed in 2008, and according to my recollection Balali was long gone at that time. Therefore, Ndulu was the one who spearheaded this spending spree!

Another thing that is worth mentioning is the total cost of these two projects which is not 1 billion shiling but rather almost 2.6 billions shilings ! At the same time, we are calling ourselves poor .
 
Hili ni la Tangazo kwa ajili ya Zabuni ya Nyumba ya Kiwanja 12 Tumbawe Road

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008. Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Lakini hii mbona imekaa ki ujumla jumla sana

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo
 
i1339_Page1.jpg

GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008. Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA

That is wrong mkataba wa kuteuliwa kiongozi especially Bank of Tanzania haukuguarantee wewe lazima upewe nyumba unataka kunambia magavana wa marekani wote wanapewa nyumba??? Pili si lazima yeye kukaa humo anaweza kukaa kwake akalipwa allowance, na hata kama upo je kwani Ndulu hawezi kukarabatiwa nyumba aliyokuwa akikaa Rashidi au Balali lazima ijengwe mpya.

Tatu gharama hizi hazijustify uhalali wa Billioni 1.4 tumeshawaeleza magavana wa US na UK nyumba zao hazinukii hata $1 Millioni, sasa gavana wa nchi ya 10 toka mwisho katika umaskini anajengewa nyumba ya $1 million basi bora wangelimnunulia nyumba Malibu, Marekani maana atakaa kwa amani.

Tuje katika gharama za ujenzi macontractor wa bongo wanakulaga dili na hao hao wanene BOT tuambieni je kuna independent team ya wapinzani walipitia hiyo estimates. Tutajua vp kama hizo estimates haziko inflated??? Msitufanye wajinga Tanzania ni karne ya 21 tuko makini mkitaka tusiwaandame iteni wabunge wa upinzani wapitie hayo makisio venginevyo huu ni ufisadi mtupu hamna zaidi.
 
Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Sawasawa.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008

Wakati huu Gavana wa Benki Kuu akiwa Prof. Benno Ndulu.

Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni. Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Gavana akiwa Prof. Benno Ndulu

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008. Mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited, gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26 (zaidi ya dola milioni moja )

Masikini Tanzania - Shamba la bibi !

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (zaidi ya dola milioni moja)

Hizi gharama ! Na hapo bado zile za ukarabati wa nyumba zingine tatu achilia mbali mikopo ambayo ilikuwa wagawane kama njugu !

My first task is to get rid of the tarnished image of the institution and nation
Those are the words Prof. Benno Ndulu uttered in his first interview after being appointed Governor in January, 2008. The bottom line is that all this has taken place under his watch. Prof., here you have failed us miserably.

According to BOT Act of 2006
"There shall be appointed by the President a Governor who shall, unless he dies or resigns or vacates or is removed from his office for good cause or is disqualified, hold office for a period of five years and shall be eligible for a re-appointment.
(2) No person shall qualify to be appointed as a Governor unless he–
(a) holds a university degree;
(b) has not less than fifteen years experience in the fields of economics, banking, accountancy or finance or law;
(c) has been in senior managerial positions in the government departments or institutions, private institutions or international organizations; and
(d) has not been appointed and served as the Governor for two Consecutive term.
(3) There shall be appointed by the President three Deputy Governors who shall, unless one dies, resigns, vacates or is removed from office for good cause or is disqualified, hold office for a period of five years and be eligible for re-appointment for a further term of five years only.
(4) The appointment of the Deputy Governors shall be made on the basis that at least one of the appointees hails from either side of the United Republic."

Mtuongezee katika kipengele hichi na nyumba pia ya kuishi apewe akimaliza aiache tubilioni tuwingi ati!!!!
 
My first task is to get rid of the tarnished image of the institution and nation

Ndullu is just like Ballali. He was there during EPA scandal and Twin Towers scandal. It was a big mistake to appoint him as a new Governor. He has failed miserably.
 
According to BOT Act 2006,
14.–(1) The salaries and allowances including retirement allowances
of the Governor and the Deputy Governors shall be determined by the
President.
(2) The fees, allowances and other terms of service of the members
of the Board shall be determined by the Board on approval by the Minister.
(3) The salaries, allowances, fees and other terms of services offered
under subsections (1) and (2) shall not be reduced or otherwise diminished

Sasa basi mtuambie rais anafahamu kuhusiana na tubilioni tunusu iliyotumika kujenga hekalu ya mzee au aliona akamezea. maana 2010 iko around the corner.
 
14.–(1) The salaries and allowances including retirement allowances
of the Governor and the Deputy Governors shall be determined by the
President.
(2) The fees, allowances and other terms of service of the members
of the Board shall be determined by the Board on approval by the Minister.
(3) The salaries, allowances, fees and other terms of services offered
under subsections (1) and (2) shall not be reduced or otherwise diminished

Sasa basi mtuambie rais anafahamu kuhusiana na tubilioni tunusu iliyotumika kujenga hekalu ya mzee au aliona akamezea.

Rais hahusiki kabisa na hii gharama ya ujenzi wa nyumba ya Gavana. Msimuingize kabisa Rais katika swala hili. Haya ndiyo yatakayokuwa maneno ya Salva kama ataulizwa kuhusu kasheshe hii.
 
HELA YA KAWAIDA SANA HIYO!hebu kasome specifications na requirements,EBO!

why are you guys interested in figures?labda mngeshauri wabadilishe DESIGN
Na wapitie BQ ili kuona mtiririko mzima...
 
Na wapitie BOQ ili kuona mtiririko mzima...
yap!
watu ningewaona wa maana kama wangeachana na siasa,wajdiliane kitu REAL!
-wahoji DESIGN SPECIFICATIONS
-wahoji DESIGN REQUIREMENTS
-waombe B.O.Q wakague rates zilivyo

then wajue sehemu ambayo the figures are INFLATED
 
Du! Tanzania safari ndefu...sasa hamjaelewa nini? kwenye ripoti mumeambiwa hivi, mkaguzi wenu atafika na kukagua hayo mahesabu kama sheria inavyotaka.

Si msubiri hapo basi ndio mseme wapi kuna tatizo?

Hivi Ndulu amefika kampuni zimeshapewa tender mlitaka akatishe hizo tenda mwajua gharama yake?
 
yap!
watu ningewaona wa maana kama wangeachana na siasa,wajdiliane kitu REAL!
-wahoji DESIGN SPECIFICATIONS
-wahoji DESIGN REQUIREMENTS
-waombe B.O.Q wakague rates zilivyo

then wajue sehemu ambayo the figures are INFLATED

Kuomba B.O.Q hakusaidii especially baada ya kuambiwa kwamba aliyepewa tenda ni yule mwenye bei ya chini!!! So BOQ itakusaidia nini? Tunajadili nini hapa? Mbona siwaelewi?
 
Back
Top Bottom