Majibizano ya Rais Samia na Spika yanaweza kuleta Anarchy!

Majibizano ya Rais Samia na Spika yanaweza kuleta Anarchy!

Wanaosema hii ni ngoma ambayo ccm wanaipiga ili wananchi tuicheze—- you are totally wrong!

Ukisoma Body language ya ndugai he was real not a joke, jamaa anaongea hadi anataka kutoa chozi.

Lakini Majibu ya Rais sasa [emoji23][emoji23][emoji23]

So tusilete mizaha hapa kama taifa...

Mimi ni mwana Ccm na ninachojua taifa Siyo mali ya Mtu ijapokua vijana wa Ccm wachumia Tumbo hujifanya kuimilikisha nchi kwa rais aliyepo madarakani.
Unapendekeza nini Mkuu...
 
Ni kweli watu hawajamwelewa Ndugai! Ni wapuuzi, wangekuwa wajinga wangeelimishwa na wakaelewa!, ni wapuuzi
Shida ni kwamba ndugai na bunge lake ndio wapuuzi wa kutupwa..

Atuambie tu anataka nini!?? Leo hii!!?
 
Jambo lililo wazi ni kwamba,iko shida kubwa uko ndani.Inaonekana kuna vuta nikuvute ya makundi yanayosigana na yakakosa pakupumulia.Kumekua na kauli za hapa na pale zisizoashiria jambo zuri.Ngoja tuone muda utasemaje.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Bunge ni Mhimili huru ilipaswa kuwa hivyo siku zote na siyo kujikomba kwa serikali.

Ayoub ameonesha nguvu ya Uhuru wa mhimili wa bunge kwa msimamo wake juu ya deni la Taifa kuzidi kupaa
 
Bunge ni Mhimili huru ilipaswa kuwa hivyo siku zote na siyo kujikomba kwa serikali.

Ayoub ameonesha nguvu ya Uhuru wa mhimili wa bunge kwa msimamo wake juu ya deni la Taifa kuzidi kupaa
Huo uhuru ndo umeanza leo!???
 
Huu ni muda muafaka covid 19 kusepa huko kwa wagonga meza wanakula kido zetu bure
 
Kuna mtu alishauri umuhimu PPP kwenye hii miradi akajibiwa kihuni sana ila setup ya hii mradi ilikuwa na mapungufu maana zilikuwa ni fikra za mtu mmoja tu!

ulianza vizuri, ila umefika mahali unajianika!!!

unataka kusema miradi ni wazo la JPM sio??? jinga wewe!!! miradi yote ilianza kabla, yake, ilipembuliwa kabla yake, alikuja kusimamia tu!!! ebu ukiwa unachamba uujue huu ukweli

pia umeingia kwenue record ya watanzania wajinga ambao hawajui spika kaongelea wapi na rais kaonglea wapi wanaona wanabishana!!!! huu umbumbumbu ndio umewafanya hatwa wenye degree na PhD KUDHARAULIKA NCHI hii

mzee umeingiaje huku??
 
Matusi mengi kwenye ujumbe mfupi..
Anyway, matusi aside, aliyefanya upembuzi wa Stiegler's ni nani?
Business plan ya kufufua shirika la ndege iliandaliwa lini?
ulianza vizuri, ila umefika mahali unajianika!!!

unataka kusema miradi ni wazo la JPM sio??? jinga wewe!!! miradi yote ilianza kabla, yake, ilipembuliwa kabla yake, alikuja kusimamia tu!!! ebu ukiwa unachamba uujue huu ukweli

pia umeingia kwenue record ya watanzania wajinga ambao hawajui spika kaongelea wapi na rais kaonglea wapi wanaona wanabishana!!!! huu umbumbumbu ndio umewafanya hatwa wenye degree na PhD KUDHARAULIKA NCHI hii

mzee umeingiaje huku??
 
Kazi ya bunge ni kutunga sheria, kuishauri serikali na kuisimamia serikali..
Sio kujibizana na serikali..

Majibizano ni ishara kwamba serikali haishauriki .. na hili sio jambo jema
Serikali isiyoshaurika ni ipi, Ile ya Jiwe iliyokopa matrillion zaidi ya 30 ndani ya miaka 5 kwa riba za muda mfupi na za kikomesho, au hii ambayo haina hata mwaka ambayo inakopa kwa riba nafuu ya muda mrefu?
 
Kwanza kabisa walaumiwe walioliharibu Bunge...hapa list ni ndefu ila Spika Ndugai hawezi kukwepa hizi lawama, pamoja na Polepole, Bashiru, Mwendazake, n.k
Hawa wamesababisha majadiliano yaliyopaswa kufanyika bungeni yafanyike mtaania...
Na hili ni tatizo maana mijadala ya mitaani ni unguided, uninformed na endless...

Nimeligusa hilo hapo juu kidogo maana kimsingi ndio lililozalisha huu mjadala wa 'mikopo na nchi kupigwa mnada' kati ya Rais Samia na Spika - Ndugai.
Nitagusia kidogo huu mjadala kisha nitamalizia na athari zake kwa imani ya wananchi juu ya watu wanaowaongoza.

1. Deni letu la taifa lina usiri mkubwa sana. Hapa Nape aliwahi kusema kuna haja ya kulifanyia 'audit' na kutafuta thamani ya fedha kwenye miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea. Hoja hii ikawa chungu kuliko 'mbilimbi' na mara moja ikazalisha timu ya 'wahuni' na 'viroboto'. Kama kawaida hoja ikageuka kioja na baadae ikafa kifo cha kawaida..japo umuhimu wa hoja yenyewe utaendelea kuwa hai.

2. Mama Samia ameongelea 'concession loans' zitakazoanza kulipwa baada ya miaka 20. Ukweli ni kwamba;
● Baada ya hiyo miaka 20 mama hatakuwa madarakani na hivyo sio yeye atakayelipa hayo madeni. Najua pia na yeye analipa madeni ya nyuma...HAPA...hapa ni pakiangalia sana. Utaratibu wa kiongozi kutengeneza tatizo leo litakalokuja kuonyesha makali wakati hayupo madarakani sio utaratibu mzuri kwasababu haya matatizo yatakua juu ya wananchi na vizazi vyao.
● Rais atakayekuwepo baada ya miaka 20 atahitaji pia kufanya miradi ya maendeleo kutokana na uhitaji wa jamii wakati huo, je itakuwaje? Miradi inayotegemewa kulipa hii mikopo ni pamoja na Ule wa umeme wa bwawa la Nyerere ambao kwakweli nina mashaka nao sana.. mvua ikigoma pale tutavuna tu kambale ambao sidhani kama watalipa deni. Kuna ule mwingine wa Shirika la Ndege ulioanza kuingiza hasara kabla hata haujaanza..big doubt!

3. Kauli ya Ndugai kwamba hii nchi itapigwa mnada.. hii ni alert kubwa sana kutoka kwa kiongozi wa mhimili wa bunge. Hii ni kengele ya hatari.
Ila kama kuna viongozi wa ajabu nchi hii nadhani Ndugai amewazidi wote.. yeye binafsi ameitia nchi hasara, misimamo yake imekuwa ikitegemea hali ya hewa ya siku hiyo. Huyu ameshiriki kugeuza bunge kuwa kituko na kutengeneza msingi wa maamuzi mabovu mengi ambayo mwendazake aliyafanya. Wakati wote deni linakuwa alikuwa akiangalia na kukaa kimya... leo miradi iko katikati ya utekelezaji na uchumi ukiwa umeyumba vibaya, anataka wananchi watozwe ili kuikamilisha... sasa sijui watatozwa nini??

Yote kwa pamoja, majibizano ya 'titi for tati' kati ya rais na spika wa bunge hayana afya kwa ustawi wa taifa...
Haya majibizano yanapeleka ujumbe kwa wananchi kuwa jikoni mambo sio mazuri. Eee..na sio mazuri kweli.. kama wapishi wanasema chakula kimeungua, basi yawezekana kweli kimeungua..
Mitaani watu wanachagua upande.. kuna wale wanaomsupport mama na kuna wagalilaya walio upande wa mwenzao..
Mwisho wa haya mabishano mtaani ni kufa kwa imani ya wananchi dhidi ya viongozi wao...hence..Anarchy!!
Hizi factions za ruling elites in public sio healthy zinakuwa cascaded mpaka katika taasisi nyeti quick realignment inahitajika haraka sana
 
Majibizano ya Spika (Bunge) na Serikali ndio inaonyesha Bunge linafanya kazi yake..., Kwahio majibizano haya na yaendeleee (kwa facts bila mipasho)
Je majibazano kati ya upinzani na serikali?
 
Ndugai tangu aseme kuwa Yesu ana mke huwa naona dish limeyumba vibaya sana
Alivyo mcharaza mwenzie na runguuu ndipo dishi liliyumbaa,alivyo ongeza huo uwendawazimu wake ndio mambo yakawa babaya zaidi kichwani kwake
 
Back
Top Bottom