Majibizano ya Rais Samia na Spika yanaweza kuleta Anarchy!

Kwanza kabisa walaumiwe walioliharibu Bunge...hapa list ni ndefu ila Spika Ndugai hawezi kukwepa hizi lawama, pamoja na Polepole, Bashiru, Mwendazake, n.k
Hawa wamesababisha majadiliano yaliyopaswa kufanyika bungeni yafanyike mtaania...
Na hili ni tatizo maana mijadala ya mitaani ni unguided, uninformed na endless...

Nimeligusa hilo hapo juu kidogo maana kimsingi ndio lililozalisha huu mjadala wa 'mikopo na nchi kupigwa mnada' kati ya Rais Samia na Spika - Ndugai.
Nitagusia kidogo huu mjadala kisha nitamalizia na athari zake kwa imani ya wananchi juu ya watu wanaowaongoza.

1. Deni letu la taifa lina usiri mkubwa sana. Hapa Nape aliwahi kusema kuna haja ya kulifanyia 'audit' na kutafuta thamani ya fedha kwenye miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea. Hoja hii ikawa chungu kuliko 'mbilimbi' na mara moja ikazalisha timu ya 'wahuni' na 'viroboto'. Kama kawaida hoja ikageuka kioja na baadae ikafa kifo cha kawaida..japo umuhimu wa hoja yenyewe utaendelea kuwa hai.

2. Mama Samia ameongelea 'concession loans' zitakazoanza kulipwa baada ya miaka 20. Ukweli ni kwamba;
● Baada ya hiyo miaka 20 mama hatakuwa madarakani na hivyo sio yeye atakayelipa hayo madeni. Najua pia na yeye analipa madeni ya nyuma...HAPA...hapa ni pakiangalia sana. Utaratibu wa kiongozi kutengeneza tatizo leo litakalokuja kuonyesha makali wakati hayupo madarakani sio utaratibu mzuri kwasababu haya matatizo yatakua juu ya wananchi na vizazi vyao.
● Rais atakayekuwepo baada ya miaka 20 atahitaji pia kufanya miradi ya maendeleo kutokana na uhitaji wa jamii wakati huo, je itakuwaje? Miradi inayotegemewa kulipa hii mikopo ni pamoja na Ule wa umeme wa bwawa la Nyerere ambao kwakweli nina mashaka nao sana.. mvua ikigoma pale tutavuna tu kambale ambao sidhani kama watalipa deni. Kuna ule mwingine wa Shirika la Ndege ulioanza kuingiza hasara kabla hata haujaanza..big doubt!

3. Kauli ya Ndugai kwamba hii nchi itapigwa mnada.. hii ni alert kubwa sana kutoka kwa kiongozi wa mhimili wa bunge. Hii ni kengele ya hatari.
Ila kama kuna viongozi wa ajabu nchi hii nadhani Ndugai amewazidi wote.. yeye binafsi ameitia nchi hasara, misimamo yake imekuwa ikitegemea hali ya hewa ya siku hiyo. Huyu ameshiriki kugeuza bunge kuwa kituko na kutengeneza msingi wa maamuzi mabovu mengi ambayo mwendazake aliyafanya. Wakati wote deni linakuwa alikuwa akiangalia na kukaa kimya... leo miradi iko katikati ya utekelezaji na uchumi ukiwa umeyumba vibaya, anataka wananchi watozwe ili kuikamilisha... sasa sijui watatozwa nini??

Yote kwa pamoja, majibizano ya 'titi for tati' kati ya rais na spika wa bunge hayana afya kwa ustawi wa taifa...
Haya majibizano yanapeleka ujumbe kwa wananchi kuwa jikoni mambo sio mazuri. Eee..na sio mazuri kweli.. kama wapishi wanasema chakula kimeungua, basi yawezekana kweli kimeungua..
Mitaani watu wanachagua upande.. kuna wale wanaomsupport mama na kuna wagalilaya walio upande wa mwenzao..
Mwisho wa haya mabishano mtaani ni kufa kwa imani ya wananchi dhidi ya viongozi wao...hence..Anarchy!!
Katika nchi hii sheria zinawahusu wananchi, wenye nchi haziwahusu. Wenye nchi wanaingia mikataba ya ajabu, wamejitungia sheria hakuna wa kuwagusa, au kuwahoji. Mwingira kalalamikia serikali, polisi wanamtafuta kwa uchochezi. Ndugai kasema ya jikoni, yupo na kiti chake.
 
Nionyeshe mwanaume anaetembea kwa kuburuza miguu chini na kichwani yupo 'smart' nami nitakuonyesha dereva wa lori mwenye mwanamke mmoja tu.
 
Kati ya mama na Ndugai mimi nachagua mama.
Mama ana vijimambo vyake lakini she is not corrupt, kama hao wa bungeni. Nia yake ni njema, mikopo tutalipa, la muhimu ni je hiyo mikopo inafanya nini.
 
Wote mnaokomalia huu mjadala ni wapumbavu kwasababu mnajadili kitu ambacho Ndugai hakumaanisha.

Mjadala umejikita kwenye UPUUZI
Oya bro! Ndugai halisi au mwakilishi wake?
Anyway! Tuliambiwa tozo ni kwa ajili ya madarasa, maji, vituo vya afya, au sio bro?
All in all: Waambieni wakopaji, kuna uhaba mkubwa wa chakula unalinyemelea taifa 2022/2023, hivyo wasikope mpaka 'bar', tusijepata aibu kuwasimulia wajukuu kuwa mlima K'njaro, L. Viktoria, n.k vilikuwa vyetu.
 
Ukiambiwa na nani?

Kwahiyo kama Tozo ni kwaajili ya madarasa, ukipata pesa sehemu nyingine hazitakiwi kujenga madarasa tena?
All in all: Waambieni wakopaji, kuna uhaba mkubwa wa chakula unalinyemelea taifa 2022/2023, hivyo wasikope mpaka 'bar', tusijepata aibu kuwasimulia wajukuu kuwa mlima K'njaro, L. Viktoria, n.k vilikuwa vyetu.
Hukulima ?

Kwahiyo unataka serikali ije kulima nyumbani kwako ?

Jishughulishe, utafirwa mjini hapa kwasababu ya njaa.

Serikali haina shamba, shamba pekee ka serikali ni watu.

Kitu pekee ambachonserikali inatakiwa kufanya ni kuwa na akiba ya chakula (NFRA) ili kupunguza majanga na siyo kugawia kila Tom, Jerry na Msukule.
 
Kwanza kabisa walaumiwe walioliharibu Bunge...hapa list ni ndefu ila Spika Ndugai hawezi kukwepa hizi lawama, pamoja na Polepole, Bashiru, Mwendazake, n.k
Hawa wamesababisha majadiliano yaliyopaswa kufanyika bungeni yafanyike mtaania...
Na hili ni tatizo maana mijadala ya mitaani ni unguided, uninformed na endless...

Nimeligusa hilo hapo juu kidogo maana kimsingi ndio lililozalisha huu mjadala wa 'mikopo na nchi kupigwa mnada' kati ya Rais Samia na Spika - Ndugai.
Nitagusia kidogo huu mjadala kisha nitamalizia na athari zake kwa imani ya wananchi juu ya watu wanaowaongoza.

1. Deni letu la taifa lina usiri mkubwa sana. Hapa Nape aliwahi kusema kuna haja ya kulifanyia 'audit' na kutafuta thamani ya fedha kwenye miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea. Hoja hii ikawa chungu kuliko 'mbilimbi' na mara moja ikazalisha timu ya 'wahuni' na 'viroboto'. Kama kawaida hoja ikageuka kioja na baadae ikafa kifo cha kawaida..japo umuhimu wa hoja yenyewe utaendelea kuwa hai.

2. Mama Samia ameongelea 'concession loans' zitakazoanza kulipwa baada ya miaka 20. Ukweli ni kwamba;
● Baada ya hiyo miaka 20 mama hatakuwa madarakani na hivyo sio yeye atakayelipa hayo madeni. Najua pia na yeye analipa madeni ya nyuma...HAPA...hapa ni pakiangalia sana. Utaratibu wa kiongozi kutengeneza tatizo leo litakalokuja kuonyesha makali wakati hayupo madarakani sio utaratibu mzuri kwasababu haya matatizo yatakua juu ya wananchi na vizazi vyao.
● Rais atakayekuwepo baada ya miaka 20 atahitaji pia kufanya miradi ya maendeleo kutokana na uhitaji wa jamii wakati huo, je itakuwaje? Miradi inayotegemewa kulipa hii mikopo ni pamoja na Ule wa umeme wa bwawa la Nyerere ambao kwakweli nina mashaka nao sana.. mvua ikigoma pale tutavuna tu kambale ambao sidhani kama watalipa deni. Kuna ule mwingine wa Shirika la Ndege ulioanza kuingiza hasara kabla hata haujaanza..big doubt!

3. Kauli ya Ndugai kwamba hii nchi itapigwa mnada.. hii ni alert kubwa sana kutoka kwa kiongozi wa mhimili wa bunge. Hii ni kengele ya hatari.
Ila kama kuna viongozi wa ajabu nchi hii nadhani Ndugai amewazidi wote.. yeye binafsi ameitia nchi hasara, misimamo yake imekuwa ikitegemea hali ya hewa ya siku hiyo. Huyu ameshiriki kugeuza bunge kuwa kituko na kutengeneza msingi wa maamuzi mabovu mengi ambayo mwendazake aliyafanya. Wakati wote deni linakuwa alikuwa akiangalia na kukaa kimya... leo miradi iko katikati ya utekelezaji na uchumi ukiwa umeyumba vibaya, anataka wananchi watozwe ili kuikamilisha... sasa sijui watatozwa nini??

Yote kwa pamoja, majibizano ya 'titi for tati' kati ya rais na spika wa bunge hayana afya kwa ustawi wa taifa...
Haya majibizano yanapeleka ujumbe kwa wananchi kuwa jikoni mambo sio mazuri. Eee..na sio mazuri kweli.. kama wapishi wanasema chakula kimeungua, basi yawezekana kweli kimeungua..
Mitaani watu wanachagua upande.. kuna wale wanaomsupport mama na kuna wagalilaya walio upande wa mwenzao..
Mwisho wa haya mabishano mtaani ni kufa kwa imani ya wananchi dhidi ya viongozi wao...hence..Anarchy!!
Cha kushangaza Gavana wa BOT amesema leo Clouds Power breakfast kuwa kama nchi hatujafikia hata 50% ya lending limit yetu ina maana Spika hakupata taarifa kwa wataalam kabla ya kuongea public mambo nyeti kama haya
 
Mihimili mikubwa ka hii inavyobisha hadharani kama mimi nunavyokuwa na wanywa K Vant wenzangu huku mtaani ni aibu kubwa...

Ikumbukwe taifa saizi lilishakata tamaa...sasa watu wanaotegemewa wanaongea hovyohovyo hiviii ni hatari kuubwaa saanaa...

This situation need to be taken care of ASAP..... hili si la kuvumilia hata kidogo.
 
Jambo la Msingi hapa ni kuhakikisha kuwa kama kuna haja ya kukopa basi iwe hivyo kwa mambo ambayo kweli tumeshindwa na tunahitaji mkopo ila sio kila jambo tunakopa kopa tu.
 
Ndo kashakopa sasa..
 
Wanaosema hii ni ngoma ambayo ccm wanaipiga ili wananchi tuicheze—- you are totally wrong!

Ukisoma Body language ya ndugai he was real not a joke, jamaa anaongea hadi anataka kutoa chozi.

Lakini Majibu ya Rais sasa [emoji23][emoji23][emoji23]

So tusilete mizaha hapa kama taifa...

Mimi ni mwana Ccm na ninachojua taifa Siyo mali ya Mtu ijapokua vijana wa Ccm wachumia Tumbo hujifanya kuimilikisha nchi kwa rais aliyepo madarakani.
 
Wote mnaokomalia huu mjadala ni wapumbavu kwasababu mnajadili kitu ambacho Ndugai hakumaanisha.

Mjadala umejikita kwenye UPUUZI
Ni kweli watu hawajamwelewa Ndugai! Ni wapuuzi, wangekuwa wajinga wangeelimishwa na wakaelewa!, ni wapuuzi
 
Back
Top Bottom