Majeshi yetu yanahitaji kujengewa uwezo juu ya Demokrasia

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa majeshi yetu toka turudi kwenye mfumo wa vyama vingi, cha kushangaza pamoja na kwamba tuna takribani miaka 28 toka mfumo wa vyama vingi uwepo majeshi yetu yamekuwa stagnant, yaani hawaendi na muda na matakwa ya wakati.

Jeshi letu JWTZ linaitwa Jeshi la Wananchi - ni jina zuri sana ingawa halijihusishi sana na mabo ya kiraia lakini wakati wa chaguzi huko nyuma tumewahi kushuhudia kiongozi wa jeshi akitishia watu.

Jeshi la polisi hili ndo worse kabisa, sijajua huko CCP mitaala yao ikoje natamani ningeiona, sijui kama mitaala yao wanafundishwa namna ya jeshi ku-behave in multiparty environment.

Nadhani bado wanatoa mafunzo yao kwa kutumia mitaala waliyokuwa wakitumia wakati wa mfumo wa chama kimoja. Wanaviona vyama vingine ni traitor kumbe vipo kisheria ni kihalali.

Hata leo nimemsikiliza IGP akitoa statement leo juu ya "TUMEJIPANGA" na uchaguzi mkuu, ile kauli ukiisikiliza ukaisoma between lines utagundua "wamejipaga" kufanya nini.

Jeshi la magereza nalo limeingia katika mtego huu kwa kujigeuza kuwa chamber ya kutoa mateso kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani huku CCM wakiingia na mayuniform yao na Ma-VX ndani ya gereza.

Kwa matukio hayo nashauri majeshi yetu yajengewe uwezo - CAPACITY BUILDING ili wapate ufahamu namna ya kufanya shughuli zao ndani ya mfumo wa vyama vingi ili waweze kujiondoa kwenye aibu ya kuonekana ni magenge ya chama tawala na yasiyo na weledi.

Nawasilisha
 
CCM wanawaogopa chadema kuliko corona na Ebola, hata ukitaka wazuie Ndege toka china zinazomimina wagongwa kila siku hao Dsm watangazie kuwa hao Wachina wote ni wafadhili wa chadema
 
Majeshi yetu yanaamuliwa na wenye mamlaka

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo ndo shida ilipo, mi naona jeshi la polisi ni moja ya kikwazo kikubwa cha demkrasia nchini, hawa watu kwa bahati mbaya wanatekeleza maagizo ya wakuu wa wilaya au mkoa bila kujali ni halali au haramu. Hawa wakuu wa wilaya ni makada wa ccm, bila shaka wameagizwa kuvinyongonyesha vyama vingine katika maeneo wanayoyaongoza. Kwa mtindo huu inabidi tubadili katiba hivi vyeo vifutwe au tufanye mabadiliko ambapo polisi atakuwa hapokei amri haramu za hawa watawala.
 
Back
Top Bottom