Majeshi ya Tanzania na huduma za dezo

Majeshi ya Tanzania na huduma za dezo

Askari yeyote(jwtz, magereza, polisi,jkt) akiwa ktk gwanda popote awapo tatizo ama uhalifu ukitokea raia wote tutategemea muongozo na msaada wake, Hawa viumbe WaPo kazini 24/7 na wamejitoa kwaajili ya usalama wetu.

Mbona ufahamu wetu uko chini kiasi hicho jamani!!!!!!!!!!
Tangu lini jwtz wakashughulika na uhalifu mtaani? Anajua hata kuandika mashtaka? wakihusika ni sawa na wewe unavyofanya kama raia mwema na unaweza kuamua kumchoma moto tu. Polisi peke yao ndo wamefundishwa kudhibiti uhalifu ndani ya nchi. Ndiyo maana wanashitakiwa kwa matumizi ya nguvu kuliko kiasi. JWTZ na magereza hawana mafunzo hayo ila ni tabia mbovu ya utawala kudhani kwamba askari wa JWTZ anaweza kamata mtu mtaani.
 
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
.

thread hii sio mimi nimetuma...
 
Kipato kidogo hakiwezi kuhalalisha upate huduma ya kudhulumu biashara za wenzako. Kitendo cha kupata huduma bila malipo ni kitendo cha dhuluma au ni ketendo cha wizi. Hakuna tofauti yoyote na mhalifu au kibaka anayechukua mali ya mtu na kutokomea nayo. Ni kwanini basi kama ni watu wanaositahili kupewa huduma za dezo, lakini wakiwa mahotelini, sokoni, maduka ya dawa na kwenginepo wanalipa? Tatizo ni kuwa wenye magari ya kusafirisha abiria (daladala) hawana umoja. Kwa sababu kama wakiamua kung’ang’ana na maaskari wasiolipa hadi mahakamani ndipo kitaeleweka kuwa kitendo wanachikifanya ni haki yao au ni kitendo cha wizi. Je kitendo cha askari barabarani kushika magari na kudai rushwa pia ni sawa kwa sababu mishahara yao ni midogo. Ni lazima askari waishi kwa kipato chao wanachokipata. Kwa sasa askari wa JWTZ mishahara yao ni mizuri na yalifanyika marekebisho ya pension zao wakati wa awamu ya tatu, kila askari anayestaafu analipwa asilimia 50 ya mshahara wa cheo alichokuwa nacho, kama kutakuwepo na ongezeko la mishahara ya ngazi aliyokuwa nayo. Ongezeko hili pia litakwenda sambamba na pension yake kuongezeka kwa kiwango cha mshahara unaolipwa kwa wakati huo.
.

thread hii sio mimi nimetuma... ni mdukuzi
 
Mkuu hivyo vijisenti watu ndo ugali wao,wewe si unakula kupitia kujua kushika SMG/Ak 47!!!

jitahd kuelewa mtu anapo post, suala la kula kwa smg ni pana vingnevyo eleza unamaana gani na utetez wa maisha ya mtu kupitia dhamana ya kutulinda kwa smg yaani kurisk maisha yake for us haviendan think big au una ajenda nyingne
 
acheni discussion za ajabu jamani wanajeshhi wapate huduma hizo wala sio kudhulumu....jeshi is a core organuiization......tusitake siasa tuzipeleke jeshini......mi kama ningekuwa raisi nasema iwe ivo hivo....wapande bure wanastahili heshima yao hao.
 
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
wacha wanajeshi wetu wajinafasi watu wanauza roho kwa ajili ya nchi au ww unafikir hiyo laki 6 wanayolipwa inafanana na maisha yao wanayoweka rehani
 
Makonda wenyewe hawadai....alafu wastani wa hawa wanausalama ni kama askari wawili (max) kwa daladala moja(hiyo ni 800~1200 ), safari za mikoani 90% wanalipa nauli... Unamtaka konda aDai nauli kwa traffic officer ilihali gari ni bovu,konda na dereva hawana uniform,bima ime-expire,ndo kwanza gari limejaza kuzidi inavyotakiwa! Haa kifuatacho atakijua mwenyewe!!
 
je ipo sheria yeyote inayompa askari polisi, jkt, magereza, jwtz, na ffu furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
mkubwa siku zote mtu akishiba anaweza kuongea chochote kile na wewe umeshiba amani ndio maana unaanzisha mada ambayo ni matokeo ya shibe ya amani, kwanza kaa ukijua kuwa wanachopewa wanajeshi ni danganya toto tu wao wanaitaji zaidi ya kupanda bure katika mabasi wewe ukifanya kazi zaidi ya muda unapewa overtime yeye kazi yake masaa 24, wewe unakadi ya bima mwenzako akiumwa mpaka akatibiwe lugalo tu je waliombali nalugalo inakuwaje, kazi yao inausika na roho zao maana yake nini wakati wa vita wao ni kufa na kupona wakati wewe unakuwa mkimbizi katika nchi ya watu ukisubiri kuwe na amani ndio uweze kurudi nchini kwako, tujadili mengine ndugu yangu lakini sio jeshi letu ambalo ni tiifu kwa wananchi wake. Sema utakachoweza kwani umeshiba amani tujadili siasa zetu ambazo zimetushinda na tujadili jinsi tutakavyoweza kujikwamua na wimbi la asomi wetu kukosa kazi na wao kutokujituma hata wakiwezeshwa wanashindwa kusimamia miradi waliyoanzisha lakini sio jeshi letu kupanda mabasi bule hiyo sio hoja ya kutuondolea umaskini.
 
Makonda wenyewe hawadai....alafu wastani wa hawa wanausalama ni kama askari wawili (max) kwa daladala moja(hiyo ni 800~1200 ), safari za mikoani 90% wanalipa nauli... Unamtaka konda aDai nauli kwa traffic officer ilihali gari ni bovu,konda na dereva hawana uniform,bima ime-expire,ndo kwanza gari limejaza kuzidi inavyotakiwa! Haa kifuatacho atakijua mwenyewe!!
 
Hapa umesema kweli GT. Asilimia kubwa ta hawa wanajeshi na mapolisi wetu wana kipato kidogo sana, na wanaishi na kufanya kazi kwenye mazingira ya tabu mno. Yaani ni afadhali hata basi wanaweza pata usafiri wa bure maana othewise labda wangekuwa wanatembea kwa miguu. Tuwaonee huruma.

Mkuu sekta ya usafirishaji inaathirika kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu ya watumishi hawa. Natambua umuhimu na unyeti wa kazi maaskari wa majeshi yetu lakini umefika wakati sasa waanze kulipa kwa kuwa na wao wanalipwa mishahara tena ni mizuri kuzidi hata baadhi ya watumishi wengine nchini
 
Tatizo la msingi ni askari wetu kuishi mitaani na raia wengine. Si jambo la kawaida kwani askari katika nchi zote huishi katika maeneo yao maalum yakiwemo makambi. Wakiwa kambini hawalazimiki kutafuta usafiri kwenda kazini!
 
mkubwa siku zote mtu akishiba anaweza kuongea chochote kile na wewe umeshiba amani ndio maana unaanzisha mada ambayo ni matokeo ya shibe ya amani, kwanza kaa ukijua kuwa wanachopewa wanajeshi ni danganya toto tu wao wanaitaji zaidi ya kupanda bure katika mabasi wewe ukifanya kazi zaidi ya muda unapewa overtime yeye kazi yake masaa 24, wewe unakadi ya bima mwenzako akiumwa mpaka akatibiwe lugalo tu je waliombali nalugalo inakuwaje, kazi yao inausika na roho zao maana yake nini wakati wa vita wao ni kufa na kupona wakati wewe unakuwa mkimbizi katika nchi ya watu ukisubiri kuwe na amani ndio uweze kurudi nchini kwako, tujadili mengine ndugu yangu lakini sio jeshi letu ambalo ni tiifu kwa wananchi wake. Sema utakachoweza kwani umeshiba amani tujadili siasa zetu ambazo zimetushinda na tujadili jinsi tutakavyoweza kujikwamua na wimbi la asomi wetu kukosa kazi na wao kutokujituma hata wakiwezeshwa wanashindwa kusimamia miradi waliyoanzisha lakini sio jeshi letu kupanda mabasi bule hiyo sio hoja ya kutuondolea umaskini.

Nashukuru sana na hongera kwa majibu mujarabu kabisa. Naomba niongeze kuwa kama ni muwekezaji wa kweli, hakuna athari anayoipata kwa hawa ndugu zetu kupanda magari yao bure. Athari pekee ni ya ''kuumia'' roho kama mleta mada anavyoumia sasa.
 
Wewe utakuwa na tatizo la kisaikolojia haswa linaloendana na ubishani ama ushindani. Serekali kupitia JWTZ imewahi kutoa tamko rasmi kwamba wanajeshi walipe nauli. Kilichotokea ni makubaliano kati ya wenye mabasi na askari hao... kwa mapenzi yao kwa jeshi lao wakawa teyari kuwabeba bure kwa safari za ndani ya mkoa kwani wanauthamini mchango wao katika kuhatarisha maisha yao kulinda mipaka ya nchi na maadui wa Taifa letu wa ndani na nje ya nchi

Si kweli kwamba askari hao wanapanda kwa makundi kama unavyosema kwani makubaliano ya wenye daladala hizo na wanajeshi/askari hao ni askari wasiozidi wawili kwa daladala moja na askari wanapopanda na kujitambua wamezidi idadi hiyo huwa wanashuka ama kujitolea kulipa kutokana na hali iliyopo.
Na mara zote askari hao huwa ndani ya Uniform na huwa wakienda makazini wakati wa asubuhi na kurejea jioni.
Mifano mizuri ya mahusiano bora kati ya Askari na Raia wao ni mongi sana ila nitakuachia mtoa mada uijaze hapa kwa kurekebisha ama kuifuta mada yako tenye chuki kwa walinda amani wa nchi. HUWEZI LINGANISHA PESA KWA HATARI WANAYOJITOLEA KUIKABILI ASKARI WETU.. THE DANGER THEY FACE HAS NO MONETARY VALUE MY BRETHRENS
MWISHO KABISA NAPENDA KUWATAHADHARISHA WATANZANIA KUWA MAKINI SANA NA WIMBI LA WATU WALIOTUMWA NA WASIOITAKIA AMANI NCHI TETU KUJENGA MAHUSIANO MABOVU KATI YA WANANCHI WASIOKUWA NA HATIA NA ASKARI WATII WA KATIBA YA NCHI...

MUNGU IBARIKI TANZANIA

well said mkuu uzur mmoja hata wao huchukua watu iwapo ikitokea magar yao kam mabasi
 
Hivi ile tabia ya kujichukulia sheria mikononi mwao wameacha au serikali ilisema nini kuhusu kuwacharaza wale wanaolipa kodi ili wao wawe jeshini?

Watanzania wengi wana tabia hii, unataka kusema wanaochoma wezi moto ni askari?

Unauhakika kuwa popote utakapoona watu wanazichapa ni askari anapigana?

Unadhani wote wanaopiga wake zao ni askari?

Hizo zote ni kujichukulia sheria mkononi,,,, tusiwaone kama ni watu tofauti sana na sisi,,,, wanaghafirika kama binadam mwingine yeyote.
 
Ww unayejiita baba "h" hujui ulisemalo..et wanajeshi hawana kazi!!..nani kakwambia?, ulinzi wa mipaka ya nchi nani anafanya??...kila mtu ktk sekta aliyopo ana umuhimu wake na sio kusema kaz ya flan ni bora kuliko flan..you better think propery kabla hujaanza kubwabwaja mambo usiyo na uhakika nayo..
 
Inategemea umepataje hizo pesa ulizonunulia daladala - kuna kulipa fadhila atiiii!
 
ngoja siku nchi ivamiwe ndio utajua umuhimu wao,fursa za wanajeshi haziko Tz ata nchi zilizoendelea.Wajeda ni watu muhimu sana kwenye nchi wako tayari kujitolea kufa ili wewe usalimike
 
ngoja siku nchi ivamiwe ndio utajua umuhimu wao,fursa za wanajeshi haziko Tz ata nchi zilizoendelea.Wajeda ni watu muhimu sana kwenye nchi wako tayari kujitolea kufa ili wewe usalimike

Yaani acha tu! Kuliko mafisadi kula hela zetu hawa askari ndiyo wanapaswa kupewa mishahara mikubwa na posho kubwa. Kazi yao ni ngumu na muhimu sana.
 
Back
Top Bottom