Mkuu ni kawaida ya sisi waafirika kupenda vitu vya bure kwa hivo msimsimange mwacheyeni tu
Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!
big up kwa dereva anaejiamini mbele ya haki yake japo huyu MJEDA MPUMBAVU BADAE ALIPIGIA WENZAKE CM WATEKE GARI NJIANI KUA KAFANYIWA FUJO, bila hata kujua watu mle kwenye gari wana nyadhfa zao walikua wanangoja gari itekwe ili badae wawe mashahdi mahakamani isitoshe kulikua na majaji kama 2 waliokua washarekodi mkanda mzima wa tukio
RAI YANGU..msifanye fujo kwenye magari kabla hamjajua nyadhifa za watu waliopo ndani ya gari
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
Nahisi wewe ni askari unayejaribu kutetea muendelezo wa vya bure.
Mkuu ni wazi kabisa ujumbe wako umeuandika kishabiki. Ni lini ulishuhudia Mwanajeshi akipelekwa Mahakama za raia? au ni lini umemsikia au kumuona jaji yeyote au hakimu akienda MAHAKAMA ZA KIJESHI? So kubali kataa Jeshi hata raisi Lazima atumie BUSARA kutoa tamko kwa vyombo hivi coz 90% ya usalama wa raisi uko mikononi mwa JESHI (JWTZ)
Kama wanawajali sana serikali iwape magari wasitusumbue au walipe nauli.mwishowe mtadai mchukue na vitu bure madukani kwa kisingizio cha kulinda amani.
eti unaingia gari ya mkoa kwa kua una migwanda yako ukidaiwa nauli hulipi na kujibu jeuri, kuna 1 jana tulimkomalia akalipa nauli vingnevyo dereva asiondoe gari badae kwa aibu alipozidiwa na hoja alilipa nusu ya nauli akambiwa na konda kwa kua hakuonesha heshma nauli yake itakapoishia ndipo anashurhwa na dereva alifanya hvyo kweli
Chonde...mimi binafsi sina tatizo hata kidogo la wana uslama kutumia vyombo vya usafiri bure as long wanazo travel cards au kitu kama oyster cards za endapo watakuwa kwenye nguo za kiraia.
Kama kuna watu niko tayari kuwa wapendelewe basi ni wanajeshi kwani tutakapo hitaji huduma zao kama kujenga madaraja ya dharura wakati wa mafuriko huwa hawatuulizi pesa
So please spare wanajeshi wetu na nadhani mashambulizi yako ungeyapeleka kwa akina SALVA RWEYEMAMU kule ikulu ambako tangu aondoke Bush hawajatoa mchanganuao wa expenses walizozitumia
Mbona huulizi ile tenda ya Vitenge na Kanga alipewa nani?
mi binafsi daladala yangu nlishamwambia dereva kuwa Jwtz&Jkt wapande bure!!! hata kama wakiwa watano!
Ukitaka Kujua kwanini; nenda congo,sudan au somalia!!
Sio kweli hata kidogo GT
Kwa sababu hawa wanajeshi sio kwamba wanatoa huduma za kujenga madaraja bure, no hawa wanalipwa kila mwezi bila kazi yoyote wanayofanya, na ndo maana zikitokea kazi za dhalula wanafanya, unaweza kuniambia wanafanya kazi gani specific hawa jamaa, wakati wanalipwa kila mwezi
Na kama ndo hivyo kila mtu atataka kusafiri bure, nani kama Mwalimu aliyewafundisha watu, kwanini hasisafiri bure?, na Madaktari je wanaokoa Maisha ya watu, mbona nao hawasafiri bure?
Hakuna mantiki katika hili kuwa askari wasafiri bure kwa sababu zipi?
Kwanza askari wa Tanzania wengi hawana nidhamu na maadili hata kwa wananchi wao, wengi wamekuwa wakiwapiga na kuwaonea wananchi, pili kuna makundi makubwa sana ya ujambazi ambayo na Maaskari wanashiriki.
Hivyo basi mimi sioni kama wao ni muhimu sana kuliko watu wengi mpaka waweze kusafiri bure