MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,977
- 777
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.