Majeshi ya Tanzania na huduma za dezo

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Je ipo sheria yeyote inayompa askari Polisi, JKT, Magereza, JWTZ, na FFU furusa ya kupata huduma ya usafiri bure katika mabasi yanayofanya biashara katika nchi ya Tanzania? Tabia hii inakwaza wawekezaji wenye uwezo wa kuwekeza katika biashara ya usafirishaji, kama yupo mwenye ushahidi atusaidie tujue kiwango cha madhara ambayo Watanzania wanayapata na wataendelea kuyapata kwa ajili ya kundi la askari ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.Kama sheria haipo nini kifanyike sasa kukomesha tabia hii?.
 
Chonde...mimi binafsi sina tatizo hata kidogo la wana uslama kutumia vyombo vya usafiri bure as long wanazo travel cards au kitu kama oyster cards za endapo watakuwa kwenye nguo za kiraia.

Kama kuna watu niko tayari kuwa wapendelewe basi ni wanajeshi kwani tutakapo hitaji huduma zao kama kujenga madaraja ya dharura wakati wa mafuriko huwa hawatuulizi pesa

So please spare wanajeshi wetu na nadhani mashambulizi yako ungeyapeleka kwa akina SALVA RWEYEMAMU kule ikulu ambako tangu aondoke Bush hawajatoa mchanganuao wa expenses walizozitumia

Mbona huulizi ile tenda ya Vitenge na Kanga alipewa nani?
 
Sio kweli hata kidogo GT

Kwa sababu hawa wanajeshi sio kwamba wanatoa huduma za kujenga madaraja bure, no hawa wanalipwa kila mwezi bila kazi yoyote wanayofanya, na ndo maana zikitokea kazi za dhalula wanafanya, unaweza kuniambia wanafanya kazi gani specific hawa jamaa, wakati wanalipwa kila mwezi

Na kama ndo hivyo kila mtu atataka kusafiri bure, nani kama Mwalimu aliyewafundisha watu, kwanini hasisafiri bure?, na Madaktari je wanaokoa Maisha ya watu, mbona nao hawasafiri bure?
Hakuna mantiki katika hili kuwa askari wasafiri bure kwa sababu zipi?
Kwanza askari wa Tanzania wengi hawana nidhamu na maadili hata kwa wananchi wao, wengi wamekuwa wakiwapiga na kuwaonea wananchi, pili kuna makundi makubwa sana ya ujambazi ambayo na Maaskari wanashiriki.

Hivyo basi mimi sioni kama wao ni muhimu sana kuliko watu wengi mpaka waweze kusafiri bure

In short bado sitaki mwana usalama achelewe kazini kwa sababu hawezi kiupewa usafiri na issue iliopo hapa ni system iliopo ndio mbovu lakini kama ikiwekwa sawa then naamini tusingekuwa na huu mjadala humu

Nisichokipenda ni ma elitists ambao wamejikita kwenye media na sehemu zingine wanatabia za kuwadharau hawa watu ambao wakiambiwa waweke maisha yao onthe line kwa ajili yangu na wewe hawatoquestion hiyo order

suala la nidhani ni dogo sana...hili ni jambo la kutatuliwa kiusalama na mawasialano baina ya raia na wanajeshi lakini siyo mambo ya kuwatukana

Isije kuwa yale yale ya wanajeshi wa UK wanaorudi toka vitani wanatemewa mate na matusi wakivaa magwanda yao kwenye miji ya Peter borough na Leicester

we can do better than hizi cheap shots dhidi ya wanajeshi
 
Nafikiri suala ni kuelewa kama hio pesa ya wafanya biashara binafsi ni nani anaifidia.

Baba H na GT, ninyi lazima mfahamu kwamba Ulaya mfumo wa usafiri ni tofauti kabisa na bongo na hatutaweza kuifikia hata kwa miaka 50 ijayo.

Mimi nimewahi kufanza kazi ya customer service assistant nikiwa shule katika vituo vya treni za chini ya ardhi kwa miaka miwili mfululizo na pamoja na kufanza kazi humo nilikua nikipewa only discount na pesa ingine ya nauli ni mzee Livingstone Mayor ndie anafidia katika makato yake na wenye mabasi na wenye matreni mengine.

Rafiki yangu mmoja ambae alikwenda kufanza mafunzo ya kijeshi pale Sandhurst na baadae kuwa mwanajeshi sasa hivi anatumikia kule (Afghanistan) yeye wanapewa kadi maalum za kusafiri na MOD ya UK kwamba makato yanakuwa yamekwisha fanzika na wenye vyombo va usafiri.

Kwa hio mtu bila ya kujua au kujua ni kwamba system inafanza kazi na watu wanafanza biashara zao kama kawaida na ndio maana wazee na watoto chini ya miaka 11 wanasafiri bure ndani ya mabasi.

Sasa wanajeshi wa Tanzania hawawezi kuwaumiza watu wenye mabasi binafsi ambao wanatafuta fwedha yao ya kula kwa kujazana ndani ya basi moja kwa kisingizio cha kutaka kusafiri bure.

Uwezo wa kifwedha wa vyombo va ulinzi na usalama bongo zivielewi kwa undani ingawa mfano wa maisha ya askari kama pale mwenge tunaujua lakini ni mpaka pale mfumo mzuri wa biashara ya usafiri utapoimarika ndipo hawa walinzi wa Taifa wasafiri bure vinginevo Serikali lazima iwafidie wenye mabasi.
 
Hivi ile tabia ya kujichukulia sheria mikononi mwao wameacha au serikali ilisema nini kuhusu kuwacharaza wale wanaolipa kodi ili wao wawe jeshini?
 
In short bado sitaki mwana usalama achelewe kazini kwa sababu hawezi kiupewa usafiri na issue iliopo hapa ni system iliopo ndio mbovu lakini kama ikiwekwa sawa then naamini tusingekuwa na huu mjadala humu

Nisichokipenda ni ma elitists ambao wamejikita kwenye media na sehemu zingine wanatabia za kuwadharau hawa watu ambao wakiambiwa waweke maisha yao onthe line kwa ajili yangu na wewe hawatoquestion hiyo order

suala la nidhani ni dogo sana...hili ni jambo la kutatuliwa kiusalama na mawasialano baina ya raia na wanajeshi lakini siyo mambo ya kuwatukana

Isije kuwa yale yale ya wanajeshi wa UK wanaorudi toka vitani wanatemewa mate na matusi wakivaa magwanda yao kwenye miji ya Peter borough na Leicester

we can do better than hizi cheap shots dhidi ya wanajeshi

Hapa umesema kweli GT. Asilimia kubwa ta hawa wanajeshi na mapolisi wetu wana kipato kidogo sana, na wanaishi na kufanya kazi kwenye mazingira ya tabu mno. Yaani ni afadhali hata basi wanaweza pata usafiri wa bure maana othewise labda wangekuwa wanatembea kwa miguu. Tuwaonee huruma.
 
ambao kwa sasa ndio wanaolipwa vizuri kuliko watumishi wengine wa uma na bado wanataka huduma ya usafiri wa bure.

Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!
 
Hivi ile tabia ya kujichukulia sheria mikononi mwao wameacha au serikali ilisema nini kuhusu kuwacharaza wale wanaolipa kodi ili wao wawe jeshini?

Hii ni grief waliyonayo moyoni ambayo hawana pa kuitolea ndo maana wanapopata nafasi wanafanya uncounsciously ili kupeleka information kwenye society of their pain
 
Hii ni grief waliyonayo moyoni ambayo hawana pa kuitolea ndo maana wanapopata nafasi wanafanya uncounsciously ili kupeleka information kwenye society of their pain

Mi nafikiri katika trainings zao hawapati Military Ethics & professional conduct na ndio maana wanakuwa na tabia kama hizi za kuchukua sheria mikononi na kuwaumiza raia bila sababu za msingi!
Suala la kulipia huduma nafikiri hili linahitaji kufanyiwa marekebisho ili hata kama wanasafiri bure basi wenye vyombo hivi vya usafiri wapate relief fulani katika biashara zao. La sivyo basi wapewe transport allowance kila mwezi na watajua wenyewe kama wapande mabasi au watembee kwa miguu.

Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!

Mimi nafikiri hapa suala kubwa ni utawala na tusitake kuonyesha kwamba wanajeshi/polisi wanashida kuliko wafanya kazi wengine....hivi nani anajua jinsi walimu wanavyopata shida hasa vijijini??? huo mshahara hapo juu ni mkubwa kulinganisha na fani zingine e.g Engineering Graduate analipwa TGS E ambao ni karibu kabisa na mshahara wa Huyu askari wa ngazi ya chini 350,000/= kabla ya makati je nani anafanya kazi zaidi ya mwenzake na nani anastahili kilipwa zaidi!!

Mimi siamini kwamba wanajeshi/polisi/askari magereza wanaishi na kufanya kazi katika mazingira magumu kuliko fani zingine hapa Tanzania.
 
Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!

Inaweza kuwa kweli wanalipwa kidogo, but si kidogo kushinda mwalimu au mfanyakazi mwimgine tu wa serikali. Kinachouma hapa ni kwamba wakarti mtu analipwa 180,000 analipa nauli ya kwenda job, je huyo askari kwa ni i aslipe? Pia wanafuzi hata watoto wa std 1 wanalipa, mbona WAJESHI WASILIPE? Sioni mantiki kabisa
 
The argument ilikuwa kukanusha kwamba wanalipwa vizuri!! Suala la kulipa nauli ni la kimuundo na kiutawala. Doctrine zinataka mwanajeshi akae ndani ya kambi tu na kama ipo mbali na kikosi basi asafirishwe na serikali hadi kazini kwake. Tatizo linakuja palepale serikali haina pesa lakini kumbe zipo kwa ajili ya mafisadi. Distributioni mbaya ya resources, km bajeti ya vyombo vya usafiri badala ya kununua mabasi ya kutosha inanunuliwa ndege tena ilikuwa mbovu sana na hadi sasa na ile helikopta iliyodondoka kule Natron, wachache walikula cha juu wakaikodisha wakaweka mifukoni kwao, bahati mbaya ikawaumbua kuanguka

Uongozi ni mbovu kila mahali nchi hii, tatizo la rotten systems na jeshini ndio kwenye ufisadi wa kutisha kwa kujifanya auditing inafanyika then hatua hazichukuliwi. Kumlaumu askari anayepanda daladala bure ni kumuonea tu. Vigogo ndio wanaoharibu! Bahati nzuri bajeti ya jeshi huwa mara nyingi inapita yote, lakini planning na implementation bado za 47 bora ilivyokuwa wazee Musuguri na Kiaro wenye philosophy za jeshi la Uingereza waliloanza nao.
 
tatizo sana sana lipo kwa hao askari wa vyeo vya chini khali yao ndo mbaya zaidi kwa mfano mapolisi kuna vituo viko nje ya mji (outpost)ambako kituo chenyewe hakina usafiri wowote na hapo hapo anafika mwananchi akisema gari lililopita either basi lina muharifu WANGU kwa hivyo tulifuatilie au kuna mwizi aliyeniibia au hata kuna majambazi unafikiria ili hao mapolisi wawafuatilie watakodi gari kwa hela zao? huo ni upande mmoja issue nyingine ni kuhusu kupeleka washitakiwa mahakamani huko out post ndo kasheshe watuhumiwa wanatakiwa kupelekwa mahakamani AMBAKO NI MJINI YAANI NI UMBALI WA KILOMITA KADHAA lakini usafiri haupo na fungu la kuwapeleka mahakamani hao watuhumiwa either halipo au liliishia mjini je wakipelekwa mahakamani hao watuhumiwa na mapolisi na hakuna usafiri wowote wa polisi nani alipe nauli? polisi awalipie nauli hao watuhumiwa au mlalamikaji au WASIPELEKWE KABISA MAHAKAMANI(ISSUE NYINGINE YA MTUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI NDANI YA SAA 24 INA KUJA ) ULIZENI HUKO KWENYE OUT POST KAMA KUNA GARI LA SERIKALI/POLISI LINAFANYA HIYO KAZI LABDA MARA MOJA KWA MIEZI 4.SASA KAMA HUYO POLISI HAPANDI GARI BURE NANI ALIPE NAULI.KTK CASE KAMA HIZI?
 
Kipato kidogo hakiwezi kuhalalisha upate huduma ya kudhulumu biashara za wenzako. Kitendo cha kupata huduma bila malipo ni kitendo cha dhuluma au ni ketendo cha wizi. Hakuna tofauti yoyote na mhalifu au kibaka anayechukua mali ya mtu na kutokomea nayo. Ni kwanini basi kama ni watu wanaositahili kupewa huduma za dezo, lakini wakiwa mahotelini, sokoni, maduka ya dawa na kwenginepo wanalipa? Tatizo ni kuwa wenye magari ya kusafirisha abiria (daladala) hawana umoja. Kwa sababu kama wakiamua kung’ang’ana na maaskari wasiolipa hadi mahakamani ndipo kitaeleweka kuwa kitendo wanachikifanya ni haki yao au ni kitendo cha wizi. Je kitendo cha askari barabarani kushika magari na kudai rushwa pia ni sawa kwa sababu mishahara yao ni midogo. Ni lazima askari waishi kwa kipato chao wanachokipata. Kwa sasa askari wa JWTZ mishahara yao ni mizuri na yalifanyika marekebisho ya pension zao wakati wa awamu ya tatu, kila askari anayestaafu analipwa asilimia 50 ya mshahara wa cheo alichokuwa nacho, kama kutakuwepo na ongezeko la mishahara ya ngazi aliyokuwa nayo. Ongezeko hili pia litakwenda sambamba na pension yake kuongezeka kwa kiwango cha mshahara unaolipwa kwa wakati huo.
 
Ngoja siku moja nchi ivamiwe ndipo mtakapo jua umuhimu wa Jeshi letu!mna zungumza kwa kuwa mpo kwenye na amani!wengine mpo nje ya nchi hamjui hata umuhimu wa jeshi letu!Mie kana dala dala nawabeba bure tu hao sina tatizo!!
 
Unajua uci ongee tu na wewe uonekane umeongea.. Wewe sasa hivi unaongea hivyo kwa kua mambo ni shwari.. Na hao wafanya biashara wako unao watetea wanafanya hivyo ni AMAN tu.. Lakn umesahau kuna wa2 hawalali mipakani makambin mpaka wakati mwingine nchi jirani nazungumzia (mission) kwa ajili ya kuitafuta aman tena wanafanya hayo bila kuangalia mazingira ni magumu kiasi gani..
Sasa leo hii unamdhihak mwanajesh eti anasafiri BURE labda ni wakumbushe 1978 wakat wa vita vya kagera wakati AMINI alipo vamia Kagera... Magar yote ya serikali na binafsi yalikua na shughuli moja tu kuwasafirisha asakari kuwapeleka FRONT.
Watanzania wenzang tuciwe wanafk hivi kusafiri bure kwa wanajeshi wetu ni dhambi zaidi kuliko wanasiasa wanaojilimbikizia mali za walipa kodi ambao wana maisha duni .. Jaman tuwahurumie wanajeshi kwa sababu bila ya wao hata huu muda wakuandika maoni tusinge upata..
 
Mshahara wa askari private kabla ya kukatwa kodi ni Tshs 170,000 approx. Na allowance ya chakula kama Tshs 50,000 hivi kwa mwezi! Ofisa wa ngazi ya chini ni sh 350,000 kabla ya kodi!!! Huko ni kulipwa vizuri??? Na Jenerali ana 1.5M, gari + extra allowances whats the difference nafikiri mishahara mizuri ni ya wanasiasa sio wanajeshi. Hawasemi kwa vile ndio maadili yao lakini hawana amani hata kidogo na hawana wa kuwasemea, Hata wabunge wanakwenda maeneo ya wanajeshi wakati wa campaign tu then mbunge gani ulimsikia akitetea maslahi ya wanajeshi? Viongozi wao ni mabilionea, remember Mb..ma with meremeta na Tanzanite + Wa...tara ni mwenye pesa nyingi sana lakini wanajeshi sasa hata kuipata kombati unatoa rushwa!

Umemsahau aliyekuwa mwenyekiti wa CCM jeshini na mnadhimu mkuu aliyechota mabilioni, kwa sasa yuko China. Anakula bata mpaka kuku wanaona wivu, akina Mello na Mike walipiga filimbi wakaambiwa funga mdomo. Juzi Mello kaishia kusema Star Tv kuwa wizi mkubwa una mihuri ya siri
 
I believe in a strong military but not free-loading. This sense of entitlement is representative of despotic regimes and I'd like to believe ours is a democracy and my party is at the helm. Tatizo naona ni uelewa wa baadhi ya wapiganaji wanaodhani wako juu ya sheria na wana haki zaidi ya mwananchi wa kawaida. Hizi tabia za kupiga raia ni upuuzi na kukosa nidhamu. Askari mwenye maadili hawezi shambulia raia kwenye pombe au kufunga mtaa kwa ugomvi wa wanawake au mwenzi wao kuibiwa. Ni ubabe wa kijinga ambao naona siku hizi wananchi hawauchekei. Sifa ya kwanza kwa askari ni nidhamu. Suala la kusingizia mishahara midogo halina uzito. Ni watumishi wangapi wa umma wanalipwa vizuri? Si wengi.

Walimu, madaktari, wauguzi n.k kwangu naona ni huduma zenye uzito zaidi katika jamii. Ulinzi ni muhimu sana but not at the cost of liberty. Kuwa askari ni kama kazi nyingine tu. Kama silaha wengi tunazo and come war (God forbid) people will be drafted. Serikali iboreshe mazingira ya kazi ya wanamajeshi pamoja na sekta nyingine zenye kipato cha chini. But this free ride some people get just because of their profession is not right. Jiulize hao wenye mabasi yao nani anawafidia gharama za uendeshaji? Hii dhana ya kusema wanalindwa haina mashiko. These soldiers GET PAID to do their job. They are not doing anyone a favor. Hakuna drafting in Tanzania, military service is voluntary. Patriotism is larger than donning fatigues.
 
Kipato kidogo hakiwezi kuhalalisha upate huduma ya kudhulumu biashara za wenzako. Kitendo cha kupata huduma bila malipo ni kitendo cha dhuluma au ni ketendo cha wizi. Hakuna tofauti yoyote na mhalifu au kibaka anayechukua mali ya mtu na kutokomea nayo. Ni kwanini basi kama ni watu wanaositahili kupewa huduma za dezo, lakini wakiwa mahotelini, sokoni, maduka ya dawa na kwenginepo wanalipa? Tatizo ni kuwa wenye magari ya kusafirisha abiria (daladala) hawana umoja. Kwa sababu kama wakiamua kung'ang'ana na maaskari wasiolipa hadi mahakamani ndipo kitaeleweka kuwa kitendo wanachikifanya ni haki yao au ni kitendo cha wizi. Je kitendo cha askari barabarani kushika magari na kudai rushwa pia ni sawa kwa sababu mishahara yao ni midogo. Ni lazima askari waishi kwa kipato chao wanachokipata. Kwa sasa askari wa JWTZ mishahara yao ni mizuri na yalifanyika marekebisho ya pension zao wakati wa awamu ya tatu, kila askari anayestaafu analipwa asilimia 50 ya mshahara wa cheo alichokuwa nacho, kama kutakuwepo na ongezeko la mishahara ya ngazi aliyokuwa nayo. Ongezeko hili pia litakwenda sambamba na pension yake kuongezeka kwa kiwango cha mshahara unaolipwa kwa wakati huo.

Awali ya yote hili jambo umelikuza. Ni wanajeshi au askari gani uliwaona wanapanda mabasi bure toka Mtwara hadi Dar? au toka Bukoba hadi Mwanza?

Pili mbona husemi kuwa askari wanaobebwa na hizi daladala karibu wote huwa wanasimama (hawakalii seats) labda kama gari ilikuwa pia ina abiria kidogo sana?

Tatu mbona hutaji "ma-staff" ambao ni watu wanaojulikana kwenye hayo ma-daladala/mabasi ama kama madereva au makonda wa magari mengine na hawalipii huduma ya kusafiri tena hata jamaa zao hawatozwi?

Nne aliyekuzuia kubandika mlangoni mwa gari yako kuwa "Askari Shs......" nani?

Suala la mishahara wala pensheni za watu haliingii hapa. Suala muhimu ni kuwa jamii ya hapa TZ huu ni utaratibu unatumika na hajatokea mmliki wa mabasi kutoa takwimu kiasi cha faida aliyopoteza kwa hilo, potelea mbali wewe hulalamikii kutusimamisha kwenye daladala yako na kutupanga kama ndizi badala ya kutii sheria ya LEVEL SEATS.
 
Mfumo wa utawala wetu usiokuwa defined nadhani ndio unasababisha mikinzano ya kiitifaki kwenye makundi na taasisi za kiraia na kijamii ila kama nchi ingekuwa transparent kiuongozi mambo kama haya ni angalabu kuonekana...askari/mwanajeshi asingeonekana mzigo.
 
Back
Top Bottom