Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Naweza kuonekana mwendawazimu kwa hii mada lakini wenye kuona mbali wataona mantiki yake!
Ni hili la majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga..Maisha yanaenda kasi sana na mabadiliko mengi yasiyotarajiwa yanatokea kwa kasi kubwa...
Miaka 30 nyuma ilikuwa ni ajabu kukuta jeneza likiwa limeshatengenezwa tayari likisubiri maiti.. Iliitwa uchuro... Jeneza lilitengenezwa baada ya mtu kufa.. Na haikuwa bidhaa ya kujiingizia kipato..
Miaka 30 nyuma sehemu za kuzikia zilitolewa bure na kwa wale ambao hawakuwa na ndugu ama walikufa na hawakujulikana asili yao wala ndugu zao walizikwa na manispaa kwenye makaburi ya serikali... Siku hizi hao ndugu ni dili.. Kuna watu wananunua misiba!
Nje ya hayo ya marehemu vitu kama harusi na sherehe mbalimbali havikuwa na michango ya lazima kama ilivyo leo hii.. Sehemu za wazi ndio zilitumika na kama kuna kumbi basi zilitolewa bure au kwa malipo kidogo
Hakukuwa na caterers
Hakukuwa na ma mc wa kukodi
Hakukuwa na wapambaji wa kukodi nk
Nguo za harusi pia zilikuwa rasmi kabisa za wahusika ..hazikikodishwa kama ilivyo leo hii.. Na hizo nguo za harusi zilitunzwa mpaka kifo cha mhusika.. Na ndio nguo atakazovishwa siku yake ya mwisho duniani
Sasa kwa dunia ya wenzetu tayari wako hatua tano mbele wao hawaziki tena.. Wanachoma moto na kukodi sehemu ya kuhifadhi majivu yaliyoko kwenye jeneza dogo la mkebe.. Mkataba ukiisha wanaweza ku renew ama kuhamisha...!
Sisi huku bado hatujafikia hatua hiyo na hata hivyo sio mila na tamaduni zetu kuchoma wapendwa wetu
Kwa tunakoelekea na kwa hizi gharama kubwa za mazishi kwasasa ni lazima sasa tuanze kuangalia option ya kuwa na majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga
Maisha yetu yamegawanyika katika sherehe kuu tatu 1. Kuzaliwa 2. Harusi 3. Kifo.. Kila mojawapo ya hizo ndugu jamaa na marafiki hujitahidi kulifanya tukio kubwa na la kukumbukwa kwa muda mrefu..
Sasa basi kwenye hili la kifo tuanze kujiandaa kuwa na majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga
Kila mtu anapenda kitu kizuri hivyo basi kuwepo na majeneza mazuri ya kukodi.. Haya mwisho wake ni pale makaburini ambapo wakati wa kuzika ..mwili utabadilishwa na kuwekwa kwenye jeneza la kawaida tuu..kuliko kutumia gharama kubwa kununua jeneza la gharama ambalo linaenda kuharibika ardhini...!
Kuhusu makaburi ya kupanga iko hivi... Unapata msiba wa ndugu yako, mwanao mke,mume nknk.. Lakini kipindi hicho mambo yako bado hayako kivile na huna kwako mwenyewe unaishi sehemu ya kupanga ...Kwenye situation kama hii ukipata msiba unaweza kwenda kuhifadhi mwili kwenye makaburi ya kupanga mpaka utakapopata sehemu yako mwenyewe...
Nitandelea