Makaburi ya Viongozi: Jeneza hugusana na udongo au ndani huwa kunakuwa na uwazi uliofunikwa na zege kwa juu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,375
Mwenye kujua atujuze kwani nafahamu ipo miili ambayo hukaushwa na kubaki kama ilivyo na mingine sujui huwekewa vioo watu watazame, n.k.

Kwa Tanzania yetu hii, viongozi majeneza yao hushindiliwa na udongo kama ya watu wa kawaida au wao huzikwa kwa namna tofauti majeneza yao hayakutani na udongo?

Na kama ni hivyo, wanapotupia udongo kwenye kaburi huwa ni kiasi kidogo tu kama ishara ya kumzika marehemu?
 
Mafundisho ya dini ya kiislam hakuna ubaguzi kwenye Ibada, Ispokuwa Hija na Zakkah.( Zakah na Hijja vitafanywa na wenye uwezo).

Na mazishi ni sehemu ya Ibada.

Kila mmoja anavalishwa sanda, anaswaliwa, anazikwa (analazwa kaburini kwa kulalia upande wa kulia, kisha anafunikwa na udongo.

Mazishi hayo yanawahusu Waislamu wote, Mashekh, Wafalme, Masultani, Marais, Mawaziri, Matajiri na wengine.
 
Wenzetu hapa mko sahihi sana.

Akilazwa tofauti, shida ni nini kwa mujibu wa imani yenu?
Maisha yote ya waislamu yana mwongozo.
Huo ndiyo mwongozo wa mazishi ya dini hiyo, kinyume chake ni upagani.
Labda kama kuna dharula
 
Ya Kikristo hayagusani lakini ya kiislamu yanagusana na udongo
Kila siku tunawafukia wenzetu wakirito kwa koleo masanduku yao ushushwa kwa kamba mpaka chini kisha ushindiliwa na udongo ss waisilamu atuziki mfu kwenye sanduku bali tuna mvilingisha kwenye nguo kisha tuna weka mbao juu yake au nyasi lakini mbao hizo azigusani na mfu kisha tuna fikia udongo habari inaishia hapo
 
Udongo mdogo sana ule wanaomwaga waombolezaji angalia la JPM na lowasa na mkapa naona ni zege tupu juu. Ndani pamesakafiwa saaafiii na vigae pembeni vimebandikwa poaaaa,chini vimawe mawe vya madoido au vigae
Kwahiyo makaburi yao huwa wanayaziba tu na zege?
 
Waislam hawaweki majeneza unaingia wewe kama wewe na sanda yako na unawekewa udongo kama kawaida
Kuna style ya ujenzi siku hizi kaburi likishajengwa kwa tofali baada tu ya usawa wa jeneza unawekwa mfuniko wa zege alafu baada ya hapo unawekwa udongo hadi juu.
 
Kuna style ya ujenzi siku hizi kaburi likishajengwa kwa tofali baada tu ya usawa wa jeneza unawekwa mfuniko wa zege alafu baada ya hapo unawekwa udongo hadi juu.
Hii ni style ya wakristo au waislam..
Maana Ujenzi wa makabuli wa waislam upo kwenge Sunna na kwenye Vitabu its all instructed
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom