masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Leo kuna kituuko cha nguo kuchanika pale Mwenge kwa Majembe.
Nani asiyeifahamu kampuni ya Majembe Auction Mart, kampuni ya udalali wa kunadi mali za wadaiwa sugu nchini.
Mwosha huoshwa, na vivyo mnadi kanadiwa leo.
Inasemekana Majembe alikuwa na deni la mtu aliyemkamata kimakosa na hatimaye kuharibu gari lake.
Mwenye gari alienda kwa pilato kudai haki yake, na akapewa tuzo ya kulipwa milioni 5 miaka minane iliyopita.
Majembe akaamua kumpuuza na kupiga chenga hukumu.
Deni na riba mara likafika milioni 300, na mdai akarudi kwa pilato kukazia hukumu.
Akapatikaba dalali chap chap na Majembe akanadiwa fasta.
Sasa leo ilikuwa mkaza hukumu, Polisi wenye silaha zaidi ya 40 walifika Mwenge kumwondoa mdaiwa Majembe katika eneo lake ambalo sasa si lake tena.
Na ilikuwa furugu, siyo vurugu bali furugu tupu
Ama kweli mwosha huoshwa!
Pole Majembe.

Last edited: