Majembe Auction Mart washapewa UBUNGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majembe Auction Mart washapewa UBUNGO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Nov 30, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  swali tangazo la hii tenda lilitolewa lini na SUMATRA na je mbona hatujaambiwa kama sheria za PPRA zilifuatwa na mchakato uliofanywa uliwapitisha akina nani mpaka akapatikana huyu Majembe?


  surely kwa issue controversial kama UBUNGO BUS stop ilitakiwa SUMATRA waonyeshe due to public interest Business plan yao nzima na malengo gani wanayo katika kufanya kile kituo kiwe user friendly


  au tunakosea kuuliza?

  Halafu kwa nini PINDA hataki tuone first (original ) version ya ripoti ya CAG kuhusu UBUNGO?
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nchi ishauzwa hiyo! Wote niwaigizaji tu!
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  "Kuna watu zaidi ya laki moja wanatumia kituo hiki kila siku, hatuwezi kuhatarisha usalama wa taifa kwa kuweka ripoti hii hadharani"
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Usalama wa kulinda ufisadi ofcourse.
  Toa Fisadi weka Fisadi ndio mchezo wa kisasa ,nilimuona Mama Simba kama mpayukaji sasa nimeanza kumwamini kwa kumnukuu "Katika CCM hakuna asiye fisadi"nakubaliana naye kwa asilimia mia moja kabsaaa
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, in the name of commission everyone becomes a servants!!! i think some of decisions a better left unknown!!!
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa Usalama barabarani James Kombe akizungumza leo jijini Dar kuhusu utoaji huduma ya usafiri kupitia kampuni ya Majembe Auction Mart.

  SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
  Yaani Kuanzia Desemba 1, 2009 Kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART imekasimiwa kazi ya kusimamia, kufuatilia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni ya kusafirisha abiria katika jiji la Dar na kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo.

  Mbali na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.

  Wenye vyombo vya Usafiri, wafanyakazi wao, abiria na wananchi kwa ujumla wanaombwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuleta maboresho yenye manufaa kwa umma.
  Kama kawaida bongo mambo tambalale ukiwa mpiga deal mambo yako safi kila siku.Hawa majembe ni kampuni ya udalali na kudai madeni sugu yaliyoshindikana,sasa suala la kushughulikia usafiri wote wa Dar pamoja na mabasi yanayokwenda mikoani hapo ubungo yamekujaje?
  Wamebadilisha fani, na je leseni yao haina specification kwamba mwisho wa majukumu yao ni wapi?
  Na hawa SUMATRA ndio siwaelewi kabisa ubabaishaji mtupu. SUMATRA ndio Surface and Marine Transport Authority, sasa tena Majembe! Kama wananchi jamani tunatakiwa kuwahoji hawa watu,mwisho wa yote hata TRA watapewa majembe.
  TUENDAKO KAMA NCHI SINA UHAKIKA!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,694
  Trophy Points: 280
  Wa madhabahuni ale madhabahuni...kama aupo madhahabahuni usiulize wanakulaje...huo ni mstari kaka upo wapi check na google
   
 8. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #8
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Hivi inakuwaje watu ambao "profession" yao ni waendesha mnada/wakala wa mahakama, wanapewa kazi kubwa kama hiyo ya kusimamia utekelezaji wa masharti ya leseni za usafirishaji? Au ni kwa sababu Memorandum and Articles of Association inawaruhusu kufanya "kazi nyingine yoyote"? Jamani, tunakwenda wapi? SUMATRA inatupeleka PABAYA sana!

  ./Mwana wa Haki
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanzo mgumu, labda baadaye patakuwa na makampuni mengi ya ndani yanayoweza mambo yote.
   
 10. M

  Mchili JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35


  Ngoja nifafanue Mkuu, ni kwamba Majembe wamepewa uwakala wa kusimamia taratibu za leseni na uratibu wa utekelezaji wa wasafirishaji kwa niaba ya SUMATRA, sio kuendesha kituo cha Ubungo. Hata hivyo SUMATRA walitakiwa kutangaza hiyo tender hilo halina ubishi kama hawakutangaza.


  Kituo cha ubungo kiko chini ya City​
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  another crazy business
   
 12. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hapa ndipo ambapo pananitia hasira, mimi sioni sababu kwanini kazi ambazo serikali ina mamlaka maarumu za kusimamia na kuratibu zikabidhiwe third party, kama wanaona hawana uwezo basi si waongeze resources...huu ni ufisadi kwakuwa gharama wanazomlipa huyo wakara ni nyingi sana....ni mchezo mchafu tu...hawa trafiki na polisi wanafanya kazi gani, je hatuwaamini?? hatuamini ufanisi wao? hao ndio products ya system zetu na wanalipwa na serikali kwa nafasi zao, kumweka wakara afanye kazi hizo ni kuongeza gharama na kumkandamiza mhusika..demotivate...
  sasa utaona watakavyotunyima raha hao jamaa, wanahistoria ya vurugu, ubabe...
  kila siku sisi ni wakubebeshwa mizigo tu, kwanini shughuli kama hizi zenye maslahi ya jamii wadau wasihusishwe, leo tuna zigo la stika za fire....kule kinondoni kuna kampuni imepewa uwakara wa kukusanya kodi za matangazo, hata wakikuta umetangaza mlangoni kwako wanachaji...tena wanataka malipo ndani ya siku 7 bila hivyo wanatishia kukupeleka mbele ya sheria....hujakaa vizuri kuna wengine wanapita wanasema wanakusanya pesa za afya (takataka)...ukiangalia takataka zinakaa wiki2 hawajazoa.....
  mbona maisha yanafanywa magumu hivi.....ina maana wananchi hawana mamlaka ya kuamua au hata kushauri hatima ya mazingira yao......
  Tanzania wajanja ndio wanokula nchi hii....HIVI YONO NI YA NANI???
   
 13. L

  Lusyonja Member

  #13
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 21, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Suala zima naona lina utata hasa lengo kubwa likiwa ni kupunguza kero kwa wasafiri na wasafirishaji abiria.
  Kuna mambo ya msingi yameelezwa kuhusu kupewa tender yenyewe lakini pia 1.Hawa majembe watalipwa namna gani? kama watalipwa kutokana na faini za
  wakosaji na kwenda tofauti na leseni za usafirishaji , itakuwa vipi kama
  hakuna wakosaji hasa pale wote watakapo fuata sheria,
  2. je hawa majembe hawatabambikia makosa wasafiri na wasafirishaji.
  3. Je hawa majembe watatumia diplomasia gani kuwatimua wapiga debe
  vituoni mwetu na stand ya mkoa-dsm, nahisi kuna maafa yanakuja hapo!
  4.Alikuwepo Mwaibula na timu yake walifanya kazi ilionekena japo hapakosi
  mapungufu kwani wengi wao walikuwa wanafahamika, je hawa Majembe
  watafahamikaje kama sio loop hole ya wezi na matepeli.Hapa naamini watu
  watalia hasa kwa hii BONGO
  5.kwa upande ya wakatiza ruti hapo Majembe na ubabe wao watakomesha
  kabisa kama wakijipanga vizuri kama wakati askari wa FFU a.ka TIGO
  walipokuwa wanaanza kazi walikuwa moto!.
   
 14. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tenda waliyopewa niya kukusanya mapato kituo cha mabasi Ubungo au ni kudhibiti madereva wasiofuata sheria??


  [​IMG] Sumatra yaipa rungu rasmi kuanzia leo

  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), umeipa rungu kampuni ya mnada ya Majembe Auction Mart kusimamia shughuli zote za usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam.
  Kampuni hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa inawashughulikia madereva wachafu, wanaokatisha ruti, wanaopandisha nauli wakati wa usiku pamoja na kupita kwenye hifadhi ya barabara.
  Aidha, makosa mengine ambayo kampuni hiyo itayashughulikia ni pamoja kukamata magari yaliyotoboka chini, wanayotoa moshi na mambo mengine yote yanayovunja sheria za barabarani.
  Uamuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israeli Sekilasa, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
  Sekilasa alisema kampuni hiyo itafanya kazi sambamba na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa usafiri katika jiji la Dar es Salaam unaboreka.
  Alisema ubabaishaji katika shughuli za kuendesha biashara ya daladala umefikia mwisho na kwamba kampuni hiyo imepewa jukumu la kusimamia utendaji wa kila siku wa magari hayo jijini.
  Alifafanua kuwa kampuni hiyo itaanza kazi yake leo ambapo wafanyakazi wake watakaa katika maeneo mbalimbali kwenye barabara ili kusimamia mabasi hayo ili yaweze kufanya kazi vizuri.
  Sekilasa alisema dereva yeyote ambaye atakutwa na kosa ama gari lake, Majembe Action Mart itamwandikia faini na atatakiwa kuilipa ili aruhusiwe kuingia barabarani tena.
  Aliongeza kuwa usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umekuwa na matatizo mengi hasa wakati wa usiku.
  Alisema polisi wa usalama barabarani hawatoshi kuwadhibiti madereva wakorofi pamoja na wamiliki wanaokataa kutengeneza magari yao hivyo kuwepo kwa kampuni hiyo kutakomesha matatizo yote.
  Sekilasa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wasaidie kufichua utendaji wa kampuni hiyo ambayo mamlaka yake imeingia nayo mkataba wa mwaka mmoja.
  Kuhusu malipo kwa kampuni hiyo, alisema itajilipa yenyewe kupitia fedha itakazotoza daladala zenye makosa.
  Hata hivyo, alisema kama kampuni hiyo itashindwa kutatua matatizo ya usafiri jijini Dar es Salaam, Sumatra itavunja mkataba huo baada ya mwaka mmoja kumalizika.
  Kwa muda mrefu, usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umekuwa na matatizo hasa wakati wa usiku ambapo magari mengi hukataa kufika mwisho wa safari ama kupita njia ambazo haziruhusiwi.
  Aidha, wafanyakazi katika magari hayo wamekuwa na lugha za matusi na kuwanyanyasa abiria, mambo ambayo Sekilasa alisema Kampuni ya Majembe itayadhibiti.

  CHANZO: NIPASHE
   
 15. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huu ndiyo ukweli, msichanganye mambo
   
 16. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ufalme wa dunia hutekwa na wenye nguvu na wenye nguvu ni "MAFISADI" wimbo namba moja TANZANIA
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  I like the idea......brilliant!

  Operation za Usafiri zinatakiwa ziwe na control, kwenye mambo ya health and Safety, use of the facility/ies for the intended purposes, revenue collection mpaka ratiba za usafiri

  How the procurement exercise was conducted remained to be desired.....
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  labda SUMATRA watuambie valuation team yao imefanya kazi vipi mpaka ikafikia hapo iilipofikia
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kila tenda majembe,majembe.......tutacha lini kupeana shavu? hivi hakuna auction mart nyingine hapa Tanzania zaidi ya hawa Majembe? Tafadhali naomba mtu anieleze perfomance ya hawa jamaa na credibility yao.
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii Majembe Auction Mart ni ya Mh Nani? Ama Nachanganya Madawa hapa na Mh Yono Kevela, MP Njombe Magharibi?
   
Loading...