Majangili waliotungua Chopa, wahukumiwa miaka 60

Majangili waliotungua Chopa, wahukumiwa miaka 60

Nadhani hii kesi inaweza kua ndio kesi iliyoendeshwa haraka sana na hukumu kutolewa katika historia ya mahakama nchini Tanganyika..
Hapana si kweli, kesi nyingi tu szimetolewa judgement promptly. Ukishakili kosa mahakamani kinachofuata ni hukumu, so wapo sahihi kabisa
 
Hotuba aliyoitoa Rais Magufuli siku ya Mahakama alisema kwamba ingawaje yeye siyo mwanasheria lkn anashangazwa na jinsi inavyofanya kazi kwa mfano mtu anashikwa na meno ya tembo inachukuwa miaka huku akifanyiwa uchunguzi sasa anachunguzwa nini mtu umeshika live?

Naaam, Mahakama yetu imeitikia wito wale majangili walioangusha Helikopta wamehukumiwa fasta miaka 70, hakuna kupotezeana muda tena, hukumu tayari fasta, hilo tumeshaliweka nyuma sasa tunahamia jambo linalofwata!


HAPA KAZI TU!​
 
Mkuu ukiwa mahakamani na ukakiri kosa hukumu haichelewi, ndio maana wale jamaa wamehukumiwa mapema, ila kuna baadhi ya wale majangili wamekana mashitaka na wamerudishwa rumande.
 
Tena Mahakama imewashukuru wahalifu hao kwa kukiri kosa na hivyo kupunguza gharama kubwa za kuendesha kesi yao. Hongera sana Magufuli aka Jembe
 
Mkuu ukiwa mahakamani na ukakiri kosa hukumu haichelewi, ndio maana wale jamaa wamehukumiwa mapema, ila kuna baadhi ya wale majangili wamekana mashitaka na wamerudishwa rumande.
Wepi hao waliorudishwa rumande? Na wao wanavutiwa kasi tu. lazima wanyooshwe
 
sasa hawa jamaa wazembe sana wewe unafanya tukio kama hilo porini huko msitu mkubwa kama huo alafu just a week unashikwa kirais namna hiyo alafu unakiri mahakamani umefanya upunguziwe adhabu.

Wamegarimu maisha yao kwa ujinga na uzembe wa hali ya juu
 
Hichi ndicho alichoomba Magufuli kifanyike, kesi kutoshelewesha kwa sababu zisizo na msingi, zikipigwa cases tano kama hizi, watu watakuwa wanajifikiria mara mbili mbili kabla ya kwenda kufanya tukio.
Wewe hujui mambo ya mahakama naona mkuu,hao watuhumiwa ni kuwa wamekiri kutenda kosa ndio maana wamehukumiwa haraka
 
Miaka ishirini na bado kesi mbili za mauaji na uhujumu uchumi (kwa jinsi nilivyoelewa taarifa kwa mtuhumiwa husika ) safi, itatoa funzo!
Mkuu kwa maisha ya mtanzania kwa sasa ukihukumiwa miaka 20 jela hiyo ni sawa na kifo maana uwezekano wa kurudi ni mdogo
 
Raia wa Uingereza ameuawa hiyo ndio sababu. ingekua ni Msukuma mwenzangu isingeandikwa hata kwenye magazeti achilia mbali kutolewa hukumu.
Wale ndio wanao endesha chumi nyingi za nchi za kiafrika mkuu
 
Mkuu Rais wetu mpendwa MAGUFURI, sio kesi za hao majangiri wavaa ndala tu,, tunataka kusikia hiyo miaka 20 kwa kinamasaki pia na genge lake?? Wale watu wa tra nao hiyo miaka 20 inawahusu..
 
Usanii mtupu. Vidagaa vitafungwa sana na kubomolewa nyumba.

JK anawajua majangili ampe Pombe majina yao awafunge. Kimama vipi?
 
Lost id,ni kweli hii itakuwa hukumu ya kwanza kutolewa faster baada ya watuhumiwa kukiri,nadhani huyu hakimu anasoma sana alama za nyakati hataki naye kuwekwa Mtu kati kuanza kuhojiwa na wakuu wake,tofauti na hapo mahakimu ni kama miungu watu wakiwa ktk mimbari,hakimu anaamua kuahirisha kesi bila kujali kwamba shahidi ameletwa toka mbali mno ili aje aeleze anachokijua kuhusu shitaka lililopo mahakamani,hakimu anaamua kumkingia kifua mshitakiwa aliyemwachia kwa kifungu kinachoruhusu mshitakiwa kukamatwa tena,kisa nduguze walishamuona kabla,aibu inakuja ni baada ya siku chache mshitakiwa aliyeachiliwa anauawa kwenye tukio la Uhalifu na wanachi.
 
Uchekewashaji wa kesi ni hasara kwa serikali na hata kwa wastakiwa. Kama hana kosa aachiliwe na kama ana kosa tumikie au alipe faini.
Inaoka muda.
 
Back
Top Bottom