Majangili waliotungua Chopa, wahukumiwa miaka 60

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,662
Watuhumiwa wanne kati ya tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye pori la akiba la Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kumuua rubani wake, wamehukumiwa kifungo kwenda jela miaka 70.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo katika mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa kesi ya tatu inayowakabili watuhumiwa saba ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyokuwa chini ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Mary Mrio.

Baada ya maelezo ya wakili huyo mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akitoa hukumu mbele ya watuhumiwa Hakimu huyo alisema kuwa katika kosa la kwanza, pili pamoja na kosa la nne kwa watuhumiwa wote wanne mahakama imewahukumu kifungo cha maika mitano (5) kila mmoja kwenda jela.

Hata hivyo Hakimu Mrio alieleza kuwa katika kosa la tatu ambalo watuhumiwa wawili kati ya hao saba walikiri kutenda, mahakama imewahukumu kifungo cha miaka mitano (5) jela kila mmoja au kulipa faini ya shilingi Milioni 10.

Kwa pamoja watuhumiwa wote wanne watatakiwa kutumikia kifungo jela miaka 70, huku baadhi yao wakitumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wengine kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Katika kesi hiyo Njile Gunga ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo atatumikia kifungo cha miaka 20, huku akiwa anakabiliwa na kesi mbili ikiwemo ya mauaji pamoja na uhujumu uhumi ambazo mahakama hiyo haina uwezo wa kuzisikiliza.
 
du...kitu hakijacheleweshwa...hivi ndo inatakiwa siyo kesi inakaa miaka 10 inapigwa tarehe tu!
 
Hichi ndicho alichoomba Magufuli kifanyike, kesi kutoshelewesha kwa sababu zisizo na msingi, zikipigwa cases tano kama hizi, watu watakuwa wanajifikiria mara mbili mbili kabla ya kwenda kufanya tukio.
 
Miaka ishirini na bado kesi mbili za mauaji na uhujumu uchumi (kwa jinsi nilivyoelewa taarifa kwa mtuhumiwa husika ) safi, itatoa funzo!
 
Ntaomba kesi ya yona na mramba isikilizwe upya na kutolewa hukumu maana naona kama pesa iliishika mahakama macho.
 
Break newz majagili miaka sabini jera
Watuhumiwa wanne kati ya tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye pori la akiba la Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kumuua rubani wake, wamehukumiwa kifungo kwenda jela miaka 70.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo katika mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa kesi ya tatu inayowakabili watuhumiwa saba ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyokuwa chini ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Mary Mrio.

Baada ya maelezo ya wakili huyo mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo.
Hata hivyo wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akitoa hukumu mbele ya watuhumiwa Hakimu huyo alisema kuwa katika kosa la kwanza, pili pamoja na kosa la nne kwa watuhumiwa wote wanne mahakama imewahukumu kifungo cha maika mitano (5) kila mmoja kwenda jela.

Hata hivyo Hakimu Mrio alieleza kuwa katika kosa la tatu ambalo watuhumiwa wawili kati ya hao saba walikiri kutenda, mahakama imewahukumu kifungo cha miaka mitano (5) jela kila mmoja au kulipa faini ya shilingi Milioni 10.
Kwa pamoja watuhumiwa wote wanne watatakiwa kutumikia kifungo jela miaka 70, huku baadhi yao wakitumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wengine kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Katika kesi hiyo Njile Gunga ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo atatumikia kifungo cha miaka 20, huku akiwa anakabiliwa na kesi mbili ikiwemo ya mauaji pamoja na uhujumu uhumi ambazo mahakama hiyo haina uwezo wa kuzisikiliza.
Mbona hawajasema na kazi ngumu?
 
Nadhani hii kesi inaweza kua ndio kesi iliyoendeshwa haraka sana na hukumu kutolewa katika historia ya mahakama nchini Tanganyika..
Raia wa Uingereza ameuawa hiyo ndio sababu. ingekua ni Msukuma mwenzangu isingeandikwa hata kwenye magazeti achilia mbali kutolewa hukumu.
 
Kama kesi zote zingesikilizwa kwa speed hii (na weledi pia) naamini mahabusu zingepumua. Na wale ambao wanawekwa ndani mda mrefu kwa milolongo mingi ya kuahirisha kesi wangepata afueni
 
Tuanze kutumia sheria za Uarabuni ikiwezekana. Haiwezekani mtu aue kwa kukusudia halafu afungwe tu!
 
Back
Top Bottom