Majangili waliotungua Chopa, wahukumiwa miaka 60

Majangili waliotungua Chopa, wahukumiwa miaka 60

Mkuu kwakweli nawashangaa hawa mods kuwafuga hawa vijana wanao kashifu na kutukana watu hivi bila ya kuwachukulia hatua kwa kuwapiga ban
Humu kuna watu hawana adabu halafu wanaachwa watukane watu. Nashindwa kumwelewa hawa wanaowafuga
 
Huyo Njile Gunga aliyebaki anakabiliwa na kesi mbili ya mauwaji na uhujumu uchumi,nafikiri kesi iliyomkalia vibaya ni ya mauwaji tu,kuhusu uhujumu uchumi naomba haki itendeke ili naye ahukumiwe walau kufua nguo za wateja wa Hotel ya "kiburudisho cha papaa mukulu"
 
Wahujumu uchumi wanapewa mda wa kulipa kodi mbna wao wasihukumiwe fastafasta kma hao majangili
 
5+5+5+30 =/=70, ninyi wahandishi wa habari za mahakamani muache kutuchanganya hiyo sabini inakujaje...! Yaani mnadanganya kuwa washatakiwa wamefungwa vifungo vya muda mrefu kumbe siyo..!
 
Raia wa Uingereza ameuawa hiyo ndio sababu. ingekua ni Msukuma mwenzangu isingeandikwa hata kwenye magazeti achilia mbali kutolewa hukumu.
Kama vile kamanda Mawazo alivyouliwa na 'mazombie'! Ukishangaa ya Nkurlunziza, subiri uyaone ya Shein na Jecha!!
 
Raia wa Uingereza ameuawa hiyo ndio sababu. ingekua ni Msukuma mwenzangu isingeandikwa hata kwenye magazeti achilia mbali kutolewa hukumu.

Hapana! Tukio la kutungua ndege si jambo dogo hata kama ingeendeshwa na msukuma, bado ufuatiliaji ungekuwa mkubwa km ilivyotokea kwa rubani mzungu
 
Kwa kasi hii kesi nyingi zitasikilizwa. Hongereni idara ya Mahakama!
Usiwe mwepesi wa kupongeza, kama umekwenda shule kidogo hata kama huna taaluma ya sherias, , UNAJIULIZA UHARAKA HUU, TARATIBU ZA KISHERIA ZIMEFUATWA? HAKI IMETENDEKA? WALIKIRI KWA HIARI YAO? ETC
 
Mimi nilikuwa nataka wanyongwe kabisa manina zao kwanini hatujawauwa?
 
Hii hukumu imenishabgaza,Yani juzi tu ushahidi tayari na hukumu.Au tumemridhisha bwana mkubwa baada ya kumchezea sharubu.
 
Mkuu Kibo10 ebu funguka kidogo habari hii iko kwenye chanzo gani tukaifuatilie.

Ingekuwa kesi inaenda faster namna hii Wenzetu wenye ulemavu wa Albinism wangekuwa salama.
 
Hii hukumu imenishangaza,Yani juzi tu ushahidi tayari na hukumu.

Unashangaa nini? nchi za wenzetu hukumu yaweza chukua hata nusu saa ushahidi ukiwepo.Mfano umefumaniwa hapo hapo waweza pewa hukumu ya kukatwa kichwa au sheikh kukuoza hapo hapo ndoa ya mkeka.

Mahakama zikiwa na kasi hiyo uhalifu utapungua sababu watu hucheza na uozo wa mahakama kutokuwa na hofu ya kufanya makosa.Hukumu za haraka ndizo zimefanya nchi za uarabuni uhalifu uwe kiwango cha chini mno.Watu ni waoga hata kuokota hela iliyoanguka chini.Akiokota anapiga kelele nimeokota hela mwenye nayo nani na anaipeleka polisi anaogopa akiitia ndani kimya kimya hukumu ya mwizi kukatwa mkono haitachukua muda.
 
Back
Top Bottom