Kete Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 6,661
- 6,910
Binafsi kila ninapofanya jambo huwa natafuta hatari/hasara zaidi kuliko faida, faida huja yenyewe baada ya kuepuka hasara. Unapotembea kwa miguu, chombo cha moto au hata baiskel ni muhimu zaidi kuitafuta hatari na kuikabili kabla haijakamilika au kuanza, lazima uwatizame wenye chombo kama chako na wale waendao kwa miguu, jiamini mwenyewe na usimuamini mtu kirahisi, lolote popote laweza kutokea ikikosekana tahadhari. Ktk makosa ambayo huwagharimu watu wengi ni kumuamini mtu kirahisi, hii sio nzuri kwa afya yako chukua tahadhari.