Nimempa ujauzito mpenzi wa rafiki yangu

Maloso

Member
Aug 10, 2020
17
8
Nimekuwa nikila uroda na demu wa rafiki wangu kwa muda sasa. Hili limekuwa likifanyika kila rafiki wangu anapoingia zamu ya usiku pale kazini pao.

Huyu demu wake hupenda pesa na anasa. Nilianza kumtongoza kisirisiri usiku mmoja tulipokuwa katika kilabu fulani mjini tukilewa. Katika zile harakati za kulewa, rafiki wangu akaenda msalani nikabaki na yule demu wake. Mimi kwa ulevi wangu nikamwomba namba yake ya simu akanipa (rafiki wangu hakujua). Tokea hapo yule binti akawa yuanisumbua sumbua eti yuataka nimpeleke out kulewa n.k.

Kwa utani nikamwambia aje kwangu kuna pombe nyingi ambayo hatoweza kuimaliza. Demu akasema atapitia jioni mpenziwe akienda kazini. Amini usiamini yule binti alikuja nikamnywesha pombe na hatimaye nikala uroda naye kavu kavu. Hili likawa jambo la kawaida kati yangu naye japo kwa usiri mkubwa.

Sasa jana ameniambia kuwa ana ujauzito na ile mimba nilimpachika mimi. Wadau, kama kweli ile mimba ni yangu nitajikwamuaje katika hali hii? Leteni mawaidha tafadhali. Nafikiria nibadilishe namba yangu ya simu na kuhamia mtaa mwingine lakini sijui kama hii hatua itakuwa suluhu kamili.
 
Wameingia cha kike, alisikika mwanamziki mmoja
emoji28.png
emoji28.png
emoji1739.png
 
Shukuru umepona UKIMWI na Corona.

Shukuru umepata kiumbe na hatimaye atazaliwa mtoto.

Mtunze mzazi na kiumbe chake tumboni.

Hujazaa na ndugu yako.

Huo urafiki ungeweza kuiasha hata kwa sababu nyingine.

Kama unaweza fanya uhakiki ikibidi ili kuthibitisha kwamba hiyo mimba ni yako.

Vumilia tu, ila usijaribu kumdhuru mtoto kwa lolote. Kuwa kawaida ila kuwa mwangalifu tu usifanyiwe ubaya.

Mlinde huyo mdada asifanyiwe hujuma na jamaa.

Kitanda hakizai haramu
 
Jamaa akienda zamu usiku, wewe unajivinjari. Wewe usipokuwepo, jamaa akiwa zamu, kuna mlevi mwingine pia anafanya yake, si pombe ndo umesema imewaunganisha sio?

Sasa uhakika wa kuwa huo mzigo wa dhambi ni wako unautoa wapi?
 
kama jamaa yako alikua hapigi show si ndio ataonekana kidume piga kimya amwambie jamaa kuwa ndi kampa mimba kwani hatari kitu gani
 
Back
Top Bottom