Majambazi yaua watu wanne Tanga

Majambazi yaua watu wanne Tanga

Niliwahi kusema wakuu,huu mchezo wa kuachia Silaha watu eti za kujilinda bado Janga
huko marekani walifanya kama sie ila leo ndio imekuwa jeneza lao,hawajui watokeje,eti leo sie ndio kwaanza tunahakikia upya.
La pili,Jengo hilo lina Cameras,cha kushangaza sana utaona Polisi wanaonyesha picha za waliojeruihiwa,bada ya kuonyesha Picha za Camera za waliovamia kama walivyofanya wenzao wa Kenya Kwenye ile Mall yao,ambapo ilisaidi haraka watu kujua wahusika.
Ila hapa utasikia polisi picha hizo wanakuambia zinafanyiwa uchunguzi,sasa mtafanyiaje uchunguzi wakati raia ndio rahisi saana kuwajua pindi mkirusha picha hewani?na ndio maana matukio kama haya kufanyia uchunguzi inaweza kufika hata miaka 5
 
Acha kabisa mkuu!
Jamaa walituamru tulale chini kuna "mwanaumme wa dar" kabla hajalala chini akawa anapandisha mlege kwanza... shabaash!! alichukua tatu za kifua.. pale pale na mzee mmoja wakati jamaa wanatoka eti akajitokeza kuchungulia kulikoni na gobole lake aisee nae walimmiminia njugu aka rip palepale!!
Acha kabisa mkuu, usiombee kushuhudia!!
Wapi huko yalikusibu haya?
 
Katika hali ya kusikitisha majambazi wamevamia kituo kimoja cha kuuza mikate na keki mkoani tanga almaarufu kama central bakery,nakuua wateja wa nne na mfanyakazi mmoja kituoni hapo hapo,na kujerui wawili siku ya 20/04/2016 saa moja na nusu,na kutoweka na fedha taslim zisizo pungua million 2,..
hilli ni moja ya tukio kubwa liliowahi kutokea mkoani hapo,
taarifa zaidi zitapatikana mepema kesho..
 
Jamani million mbili, kwa nini hawachukui hela bila kuua/jeruhi Watu! Hivi huu in ujambazi tu au kuna kitu nyuma ya pazia?
 
Hili la majambazi Tanga naliangalia kwa jicho la tatu!! Isiwe ikawa wakenya wanatubeep na bomba la mafuta hapa kwamba Tanga nako hakuna amani!! Ni jicho la tatu si vinginevyo!!
Kama tanga haitopewa ulinzi wa kutosha nadhani bomba tutalisikia tu
 
Acha kabisa mkuu!
Jamaa walituamru tulale chini kuna "mwanaumme wa dar" kabla hajalala chini akawa anapandisha mlege kwanza... shabaash!! alichukua tatu za kifua.. pale pale na mzee mmoja wakati jamaa wanatoka eti akajitokeza kuchungulia kulikoni na gobole lake aisee nae walimmiminia njugu aka rip palepale!!
Acha kabisa mkuu, usiombee kushuhudia!!
Duuuuuh noma sana aise!
Spati picha ulikua km huelewi kinachofanyika a.k.a kuparalaizi[emoji1]
 
Kwa tetesi inavosemekana kuna customers pia wameuwawa habari kamili bado.
 
Nadhani jamaa wa mapango ya Amboni wamerudi,wametumwa matumizi. Maduka mengi wamefunga kamera za siri,tusubiri upelelezi
 
Kwa kupata dira hivi hii bakery iko barabara ya ngapi au mtaa gani?
 
Kwa kweli hali ya kuvamiwa imekithiri sana mwaka huu sielewi tatizo ni nini au hali ngumu yani sielewi naskia watu wanauwawa tu kila siku hali ya amani na usalama inaanza kutoweka taratibu ktk nchi yetu.
Uchochezi. Hii inaonekna kuwa ni kauli iliyokusudiwa. ...wewe ni miongoni mwa wananjama hao?
 
Nikweli wacha tuone wale ma rc maana raid magufuli aliwaagiza kuthibiti ujambazi na uhalifu kwa ujumla
Utapambanaje na ujambazi kwa kutoa matamko kwa wakuu wa mikoa wapya bila mikakati wala hatua zozote madhubuti? Majambazi hayasikilizi hotuba za Rais za kuwaapisha wakuu wa mikoa.
 
Kazi ya Doria isifanywe na Polisi tu ....hali ni mbaya sana ...doria iwe shirikishi na JKT, JWTZ ili msaada uwe karibu ....
 
Nimepita muda si mrefu maeneo ya central bakery Tanga nimekuta watu na gari la polisi wanatoa maiti tu ndani ya hiyo super market.

Nimesimama nikaona maiti tatu na taarifa niliyopewa ni kuwa majambazi walivamia na kuua waliokuwa wateja na mhudumu.

Kwa aliyeko eneo la tukio atujuze, mi nimeondoka.

Kuna umati mkubwa sana wa watu hakuna hata nafas ya kupiga picha maana polisi wapo busy wanatoa maiti na kupakia katika gari lao na wengine wameingia ndani inasemekana kuna waloingia ndani nao wameumia ndo polisi kwanza wanafanya kazi ya kudhibiti watu wasijibinafsishie vitu maana wamejaa sana
Huyo RPC wa Tanga achunguzwe kwa kina. Alipokuwa Morogoro migogoro ya wakulima na wafugaji ilikuwa haiishi, mambo ambayo yalimwondoa Dr. Rutengwe kutoka katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa. Sasa Makao makuu ya Polisi badala ya kugundua udhaifu huo na kumwajibisha pia RPC, akahamishiwa Tanga matokeo yake Tanga ambayo ni katika miji michache sana Tanzania yenye utulivu, majambazi yanajitokeza kwa kasi.
 
Me ctaki kuamini kuwa polisi wameshindwa kabisa kuuondoa ujambazi, haya matukio yamekuwa mengi sana watu wanakufa na wanaendelea tu kufa, kwa nini hata wasifanye operation wajiunge na wanajeshi? kazi namba moja ya kodi ni kulinda roho za wananchi sio kununua ma VX mauwaji ya aina yoyote ya raia viongozi wanapaswa kuya feel ndani ya mioyo yao ni bora hii nchi iendelee kuwa ya ufisadi lakin watu wasiuawawe kwa jasho lao wenyewe. Hivi inawezekanaje majambazi wazidi akili watu wote, vyombo vyote vya usalama, kama mmeshindwa mu import utaalamu intelligencia hata kutoka marekani au ulaya lazima wana mbinu ambazo hamjui.
Mkuu umeongea point kaka. Inashangaza sana kuona viongozi wala hawalipi hili swala kipaumbele. Watu wanahadaa watu na watumishi hewa wakati roho za binadamu zinaondolewa kirahisi rahisi hivi. Hii inauma sana na chaajabu huyo waziri wa mambo ya ndani na IGP wala haya hayaonekani kuwagusa. Inauma kwakweli
 
Nimepita muda si mrefu maeneo ya central bakery Tanga nimekuta watu na gari la polisi wanatoa maiti tu ndani ya hiyo super market.

Nimesimama nikaona maiti tatu na taarifa niliyopewa ni kuwa majambazi walivamia na kuua waliokuwa wateja na mhudumu.

Kwa aliyeko eneo la tukio atujuze, mi nimeondoka.

Kuna umati mkubwa sana wa watu hakuna hata nafas ya kupiga picha maana polisi wapo busy wanatoa maiti na kupakia katika gari lao na wengine wameingia ndani inasemekana kuna waloingia ndani nao wameumia ndo polisi kwanza wanafanya kazi ya kudhibiti watu wasijibinafsishie vitu maana wamejaa sana

Poleni sana wafiwa na waliopata majeraha. Mungu awaponye na marehemu MUNGU awapokee kwenye ufalme wake. Tupo wote katika majonzi haya.

WITO KWA RPC: vijana wako WA PIKIPIKI wanakomalia kukimbizana na bodaboda kupata rushwa. Uwe na utaratibu, jamani wao wafanye doria ya kawaida na si kuwinda bodaboda. Utakataa lakini ndiyo wanalolikazania KUWINDA BODABODA kupata rushwa. Wakataze kuwa hiyo siyo kazi yao, wafanye doria na si kukamata makosa ya bodaboda. Hiyo waachiwe traffic police. TUIMARISHE ULINZI
 
Back
Top Bottom