Majambazi yaua watu wanne Tanga

nanawoo

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
1,300
1,252
Nimepita muda si mrefu maeneo ya central bakery Tanga nimekuta watu na gari la polisi wanatoa maiti tu ndani ya hiyo super market.

Nimesimama nikaona maiti tatu na taarifa niliyopewa ni kuwa majambazi walivamia na kuua waliokuwa wateja na mhudumu.

Kwa aliyeko eneo la tukio atujuze, mi nimeondoka.

Kuna umati mkubwa sana wa watu hakuna hata nafas ya kupiga picha maana polisi wapo busy wanatoa maiti na kupakia katika gari lao na wengine wameingia ndani inasemekana kuna waloingia ndani nao wameumia ndo polisi kwanza wanafanya kazi ya kudhibiti watu wasijibinafsishie vitu maana wamejaa sana.

-----------------------------------------

Wakazi wanne wa jijini Tanga wamekufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa kwa risasi na majambazi .

Majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG , walivamia juzi duka kuu (supermarket) la mfanyabiashara Hamoud Ali lililopo Mtaa wa Swahili katika kata ya Central jijini Tanga .

Waliokufa katika tukio hilo ni Ahmed John, Vitus Manfred ambaye ni dereva wa gari la Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Athumani Seya pamoja na Ali Mpemba ambaye ni mfanyakazi kwenye duka hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paul tukio hilo ni la juzi saa 1.30 usiku.

‘’Wakati biashara inaendelea ndani ya hilo duka kuu , ghafla waliingia watu wengine zaidi kama wateja ambao baada ya muda mfupi walibadilika na kutoa silaha za moto”, alisema.

Aliongeza “Kitendo chao hicho kilienda sambamba na amri ya kuwataka watu wote waliokuwa humo dukani kulala chini ambapo inadaiwa walitii na kisha wakaamua kuwapiga risasi maeneo ya kichwani wateja wanne waliokuwemo.”

Kamanda alisema majambazi hao walipora Sh milioni 2.7 na kukimbilia kusikojulikana.
 
Nimepata habari wameua watu wa nne mmoja ni kijana wa pale pale muuza gas nje na mgine ni driver wa gari la mahakama nissan hardbody na hao wawili bado hawajatambuliwa coz wamevimba uso
 
Habari za usiku wakuu km kichwa cha habari kinavojieleza,

Kumetokea tukio la kuvamiwa na majambazi katika duka au supermarket ndogo iliyopo tanga mjini maarufu kwa central bakery na kuuwawa watu wanne usiku huu.

Mpk jeshi la polisi tayari tukio lishatokea.poleni kwa msiba na wenye taarifa kamili au waliokuepo eneo la tukio mtupe habari kamili.

Nipo tanga lkn mbali na eneo la tukio.
 
Nadhani utakua haukuepo na hata kama ulikuepo pengine na wenyewe umeuwawa manake mpk dakika hii sijapata taarifa ya nani na nani waliuwawa.
Dah noma sana!
majambazi wana staili zao kali sana... yawezekana walivaa mabaibui full ninja kumbe viunoni wana manati za kizungu!!
Usiombe ukutane na hii dhahma...
Ilinitokea mtoni kwa aziz waliingia kwa style hiyo kwenye supermarket.. sitasahau maishani kamwe!
 
Dah noma sana!
majambazi wana staili zao kali sana... yawezekana walivaa mabaibui full ninja kumbe viunoni wana manati za kizungu!!
Usiombe ukutane na hii dhahma...
Ilinitokea mtoni kwa aziz waliingia kwa style hiyo kwenye supermarket.. sitasahau maishani kamwe!
Aise pole sana
 
Dah noma sana!
majambazi wana staili zao kali sana... yawezekana walivaa mabaibui full ninja kumbe viunoni wana manati za kizungu!!
Usiombe ukutane na hii dhahma...
Ilinitokea mtoni kwa aziz waliingia kwa style hiyo kwenye supermarket.. sitasahau maishani kamwe!
Wakiwa kazini huwa hawana masihara maana wajua kuwa ukiwawahi wameumia wao
 
Back
Top Bottom