Majambazi yaua watu wanne Tanga

Majambazi yaua watu wanne Tanga

Uchochezi. Hii inaonekna kuwa ni kauli iliyokusudiwa. ...wewe ni miongoni mwa wananjama hao?
Huangalii taarifa za habari?mwaka huu umeshasikia matukio mangapi?mbona unakurupuka tu nakuja kusema uchochezi au kauli iliyokusudiwa hivi kauli zilizokusudiwa na kauli za uchochezi unazifahamu ww?watu wanajadili jinsi ya kuepukana na matukio nini wafanye au nini kifanyike wewe unakuja hapa na kuropoka au pengine hukupenda tujadili haya mambo?unayapenda matukio haya?au ni mmoja wao?!
 
Wakiwa kazini huwa hawana masihara maana wajua kuwa ukiwawahinwameumia wao
Kweli manake wakiwa eneo la tukio wanaweza kuabort mission lakini wakishatoa mabunduki hadharani no turning back nadhani hata wao wanakuwaga na kiwewe vsv ,hofu,taharuki na ndio maana mtukupigwa risasi au hata kuuwawa ni rahisi sana!
 
Hawa majambazi Ni machunusi sio majipu watumbuliwe
 
Mkuu kweli kuna ugumu ktk kudhibiti hilo ila wenye maduka inabidi wajiongeze zaidi kukabiliana na matukio ya ujambazi. Mathalani ikifika mida ya jioni kuwe na mlinzi maalum anaejulikana na mwenye duka tu kazi yake itakuwa ni kulanda landa dukani huku kaficha mguu wa kuku kiunoni then kwenye ambush km hizo inakuwa rahisi kukabiliana na haya majambazi,.. japo ni too risk to attempt that!
Kweli! Mi nadhani kitengo cha intelijensia polisi kiimarishwe ni bora kinga.Mapambano kwenye tukio casualty haziepukiki hata kwa walinzi na polisi wenyewe.
 
Imeniuma sana mmoja kati ya wateja waliouwawa ni Fundi wa magari madogo anaitwa Athumani garage yake iko old korogwe road maarufu kwa Sb jiwa ni mtu wa morogoro maisha yake yote alikuwa Tanga. Inasemekana alichungulia baada ya kukuta mikiki ndani ile kugeuza tu akamiminiwa za shingo ni mmoja kati waliokufa nje ya duka.
 
Kweli manake wakiwa eneo la tukio wanaweza kuabort mission lakini wakishatoa mabunduki hadharani no turning back nadhani hata wao wanakuwaga na kiwewe vsv ,hofu,taharuki na ndio maana mtukupigwa risasi au hata kuuwawa ni rahisi sana!
Kweli kabisa hiyo inaitwa liwalo na liwe,ili mradi kuokoa uhai wa mhusika
 
Hakukua na ulinzi hapo dukani?
Walinzi na gobore au Rungu??..nA MIJAMBAZI YA SIKU HIZI INA MIMACHINE GUN YA UHAKIKA, WANAKUWA WAMEJIPANGA NI POLISI TU KUONGEZA DORIA KILA MITAA.
 
Hawa watu siwapendi, hivi kwanini wasingechukua hizo pesa wakatokomea yani wasiwe na haja ya kumpiga mtu panga au risasi, basi bora wawapige vibao au vitako vya bunduki, Mungu awalaze pema peponi, poleni wafiwa. INAUMA SANA, Serikali tunaomba Doria kwenye mitaa na vituo vya polisi viongezeke.
 
Unashindana na mm jinsi nisivyo wapenda hao watu hawana utu kabisa usiombe ukakutana nao
 
Mbaya sana hii. Sikuwa na jua kama kuna tukio hili limetokea, nilipita eneo hilo saa 2 kasoro asubuhi nikaona hiyo bakery imefungwa nikashangaa kidogo sababu kawaida huwa inafunguliwa mapema asubuhi.
 
‘’Wakati biashara inaendelea ndani ya hilo duka kuu , ghafla waliingia watu wengine zaidi kama wateja ambao baada ya muda mfupi walibadilika na kutoa silaha za moto”,alisema.

Aliongeza “Kitendo chao hicho kilienda sambamba na amri ya kuwataka watu wote waliokuwa humo dukani kulala chini ambapo inadaiwa walitii na kisha wakaamua kuwapiga risasi maeneo ya kichwani wateja wanne waliokuwemo.”

-----------------

Kama washatii amri na kulala sakafuni, kwanini uwapige risasi tena za kichwa? Huu ni unyama kabisa.
 
Very unfair!kuua watu wanne kwa sababu ya tsh milioni mbili na laki saba!Wauaji walaaniwe.
 
Kwa kupata dira hivi hii bakery iko barabara ya ngapi au mtaa gani?
halipo barabara za namba ni huku chini kama unaenda idara ya maji karibu na reli nashindwa kukuelekeza but ni mtaa wa Swahili
 
Imeniuma sana mmoja kati ya wateja waliouwawa ni Fundi wa magari madogo anaitwa Athumani garage yake iko old korogwe road maarufu kwa Sb jiwa ni mtu wa morogoro maisha yake yote alikuwa Tanga. Inasemekana alichungulia baada ya kukuta mikiki ndani ile kugeuza tu akamiminiwa za shingo ni mmoja kati waliokufa nje ya duka.
huyu jamaa ndio ameniuma wallah nakumbuka mara ya mwisho nilikutana nae patwas akiwa na mwanae na akantambulisha kumbe ndio ilikua bye bye ndio basi tena ahadi imefika allah amweke alipopachagua alipokuwa hai
 
Huu ni ungese yani jambazi anaua kisa million.. Halafu tukiwaua huku mtaani matamko mia tano
 
Back
Top Bottom