Jamani inakuwaje Tanzania yangu wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi? Majambazi wamevamia hapa Shekilago dukani kwa jamaa na kupora pesa na watu 2 wamejaruhiwa na watu wote tuko ndani tumeogopa kutoka nje . IKisha tulia nitaenda kuwaleta taarifa zaidi . Hali Dar inatisha risasi nje nje .
Mwenye nyeti zaidi tafadhali atumwagie mie nimezima taa naogopa wasiona nachungulie nje . Hali inatisha
Lunyungu
JF Senior Expert Member
Join Date: Tue Dec 2006
Location: Malampaka
Posts: 4,703
Thanks: 1
Thanked 201 Times in 109 Posts
Pole mkuu Lunyungu Tatizo Malampaka napo watu wengi hawana ajira. Kweli malampaka panatisha kama ndiyo style hiyo. Ukitoka tuhabarishe basi je CCTV za Polisi zimewatambua ni kina nani waliofanya uhalifu huo?
Funny!!!! CCTV za polisi zinamwona Jerry Muro pekee, hahahaa!!, so funny 😕! Hata siamini, kila kukicha majambazi yanatamba kama yanavyotaka na hakuna anayekamatwa, na wala hatukuwahi kusikia kama kuna kitu kinaitwa CCTV ambazo zinarekodi matukio kama hayo, lakini Jerry akikaa kwenye meza kwa mazungumzo CCTV zinafanya kazi. inji hii bwana! kaazi kwelikweli!!!Pole mkuu Lunyungu Tatizo Malampaka napo watu wengi hawana ajira. Kweli malampaka panatisha kama ndiyo style hiyo. Ukitoka tuhabarishe basi je CCTV za Polisi zimewatambua ni kina nani waliofanya uhalifu huo?
Wako wanashughulikia swala la J.Muro,hawawezi kuacha kituo wazi kwani kuna wale jamaa waliokuwa kwenye sakata la Muro wako ndani.Lakini asubuhi wataitisha press conference kuelezea hayo yaliyotokea Shekilango.Pole sana mkuu. tuombe Mungu maafa yasiwepo.
polisi mmewapigia simu lakini??
Mkuu usilete utani hali ni ngumu majambazi wamemwaga sana risasi na nia yangu ni kujua nani kapona na wamepora kiasi gani . Haya ya Malampaka yaache tafadhali leo niko Dar .
Jamani inakuwaje Tanzania yangu wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi? Majambazi wamevamia hapa Shekilago dukani kwa jamaa na kupora pesa na watu 2 wamejaruhiwa na watu wote tuko ndani tumeogopa kutoka nje . IKisha tulia nitaenda kuwaleta taarifa zaidi . Hali Dar inatisha risasi nje nje .
Mwenye nyeti zaidi tafadhali atumwagie mie nimezima taa naogopa wasiona nachungulie nje . Hali inatisha
Ujambazi huchochewa sana na (a) umaskini wa watu kutokuwa na kazi, (b) tofauti kubwa za viwango vya maisha miongoni mwa raia.
Kukosekana kwa tabaka la kati (middle class) baina ya matajiri wakubwa na mafukara wakubwa katika jamii huchochea baadhi ya raia kufanya ujambazi ili waweze kupata kipato cha kuwawezesha kuishi kwa kiwango cha matajri wa jamii.
bongo kweli ni shida tupu...wezi nao wanachukua advantage ya ubize wa polisi mmmh