Majambazi wapora Buguruni kwa pikipiki aina ya Boksa!!

Majambazi wapora Buguruni kwa pikipiki aina ya Boksa!!

KAMANDA HANGA

Senior Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
158
Reaction score
58
Dakika tatu zilizopita majambazi wamepola hapa BUguruni sheli kwenye bakery ya kuuza mikate na vitafunwa.

Wamekuja bila woga na pikipiki lao la Boksa na kuchukua mkwanja tena bila woga na kufyatua risasi juu.

Mie niko bar ya jirani hapa junction ilibidi kidogo wateja wa junction tujifiche kwa mda na mpaka sasa hakuna askari alofika wala nini na ni karibu na kituo kikuu cha polisi Buguruni.

Kweli haya majanga.
 
Matukio kama haya yameanza tena .......!!?
au ni watoto wa mbwa wamerudi!?
 
Dakika tatu zilizopita majambazi wamepola hapa BUguruni sheli kwenye bakery ya kuuza mikate na vitafunwa.
Wamekuja bila woga na pikipiki lao la Boksa na kuchukua mkwanja tena bila woga na kufyatua risasi juu.
Mie niko bar ya jirani hapa junction ilibidi kidogo wateja wa junction tujifiche kwa mda na mpaka sasa hakuna askari alofika wala nini na ni karibu na kituo kikuu cha polisi Buguruni. Kweli haya majanga.
wewe si kamanda mboni muoga..
 
Napafahamu sana hapo hata hiyo bar uliopo ni nyumba ya pili toka hapo palipo vamiwa...cha kushanga inamaana hao watu waliojaa buguruni wafanya biashara wapo kibao hapo wameshindwa kabisa kuwashika hao jamaa? Na police now si wapo hapo hapo rozana!!!
 
Hata mie niko hapa kweli hii ilikuwa kama sinema ya kihindi kwani hawa watu kama wamesomea make sie hapa Junction tulisikia mlio na baada ya hapo zilikuja hadithi tu za tukio. Kweli hili ni janga kwani kama waniba karibu na polisi vipi nje! Tanzania is not safe
 
Dakika tatu zilizopita majambazi wamepola hapa BUguruni sheli kwenye bakery ya kuuza mikate na vitafunwa.
Wamekuja bila woga na pikipiki lao la Boksa na kuchukua mkwanja tena bila woga na kufyatua risasi juu.
Mie niko bar ya jirani hapa junction ilibidi kidogo wateja wa junction tujifiche kwa mda na mpaka sasa hakuna askari alofika wala nini na ni karibu na kituo kikuu cha polisi Buguruni. Kweli haya majanga.

sasa nyie mlijificha ili iweje?
Mbavu sana, mnafurahia kuona wenzenu wakiibiwa sio
 
Kituo kiko Rozana kule lakini mnavyosimulia utadhani kipo stendi ya Muhimbili hapo!? Kama hawajauwa au kujeruhi Mungu ni mwema.
 
sasa nyie mlijificha ili iweje?
Mbavu sana, mnafurahia kuona wenzenu wakiibiwa sio

Mkuu kazi ya ulinzi na usalama inawenyewe.
"Do it perfect otherwise don't do it."
"Make safe of the head on your sholders"
rescue ethecs!!!!!!
 
Acha watu wachangamkie fursa!ila fursa zngne noumer sana!
 
Wamekwiba pesa za vitafunwa?jamaa wanatisha sana hawa
 
Kwanza kabisa tumshukuru Mungu kama hakuna aliyefariki katika tukio hilo. Pili hawa askari wa Tanzania huwa hawawezi kuwahi kwenye tukio. Siku zote wanafika ktk eneo la tukio baada ya majambazi kuondoka. Niliwahi kushuhudia #MWANZA mtaani wa mirongo majambazi kurushiana risasi na raia ambapo polisi wa kituo hicho cha Mirongo walijifungia ndani hata majambazi kulipua Transfomer na hatimaye kuondoka baada ya kutofanikiwa. Maaskari wetu waoga sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom