Majambazi wajeruhi na kupora Ngara

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Majambazi wameteka eneo la mpaka wa Tanzania na Rwanda kijiji cha Benako Wilaya ya Ngara wamejeruhi mmoja na kupora fedha kwenye maduka.

Chanzo: ITV

==========

Michango ya Wachangiaji wengine....

 
Tanzania bana Askari wanakaa Tu badala ya kuwaweka wakae Doria maeneo hatari Rwanda tembea hata saa 8 ucku Doria IPO ya Kutosha
 
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameteka kijiji cha benako wilayani ngara mkoani kagera na kupora fedha kwa zaidi ya masaa 3.

Taarifa iliokuja kama breaking news kupitia kituo cha ITV kinasema kuwa kuwa majambazi hao wameteka kijiji huku wakiwa na silaha za kivita na kuzunguka kijiji kizima ikiwepo kituo cha polisi kilichopo hapo hapo. kijiji hicho ambacho kina njia tatu za kuingia kilizingirwa na majambazi hao.

Polisi wanaelezwa kuchelewa kufika eneo la tukio ambalo limefanyika usiku wa kuamkia leo na kupelekea mashambulizi kudumu kwa masaa 3. ikumbukwe kuwa kijiji hicho kipo karibu na mpaka na rwanda na Tanzania ambapo magari makubwa ya mizigo na biashara mbalimbali zinafanyika.

Mpaka sasa hakuna taharifa yoyote ya kifo japo wapo watu walio jeruhiwa na tukio hilo,,, mpaka sasa vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la wananchi wa Tanzania, polisi, usalama wa Taifa na uhamiaji wamejaa eneo la tukio,

Taarifa za awali hakuna jambazi yeyote alie kamatwa mpaka sasa,, pia kituo cha polisi cha eneo hilo kilizingirwa na majambazi hao na polisi kutegemea kutoka wilayani.

Waandishi wa habari wamezuiwa kukaribia eneo hilo la karibu kwani kuna msako wa hali ya juu.

SOURCE; ITV BREAKING NEWS
 
unaambiwa ukitoka tu unarushiwa grenade mbili , mtu ana silaha ya kivita na wanatembea nyumba hadi nyumba ssa uyo polisi na kiSMG atafanya nini uku washikaji wamebeba rocket mgongoni
 
Watu wanaozaniwa kuwa majambazi wenye siraha wameteka kijiji cha Benako, wilayani Ngara, mkoa wa Kagera kwa takriban saa tatu leo, na kupora fedha kwa wanakijiji na kujeruhi wengne kwa risasi.
source; ITV breaking news.
 
Polis walikua wap?? Masaa matatu du!! Poor my country
kaka hata ungekua wewe ni polisi usingeenda kwa sababu jamaa walikua na grenade za kutosha mifukoni na ukitoa pua tu wanakurushia ufe nalo, hata miki nisingeenda hata iweje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…