Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Majambazi wameteka eneo la mpaka wa Tanzania na Rwanda kijiji cha Benako Wilaya ya Ngara wamejeruhi mmoja na kupora fedha kwenye maduka.
Chanzo: ITV
==========
Michango ya Wachangiaji wengine....
Chanzo: ITV
==========
Michango ya Wachangiaji wengine....
Si kweli kwamba Majambazi wameteka Kijiji, Wala si kweli kwamba Majambazi walipambana na vyombo vya Usalama.
Usahihi ni;
Benaco ni Centre ya Biashara iliyopo Kijiji cha Kasulo Kata Kasulo baada ya kugawanywa. Zamani ilukuwa ya Rusumo Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. Majambazi Waliovamia walikua Wawili wenye Bunduki. Walivamia Kibanda cha M Pesa cha Mfanyabiashara aitwaye Niko na kufanikiwa Kupora Pesa za wateja waliokuwepo na Mfanya biashara mwenyewe.
Walijeruhi Mtu Mmoja aliyejaribu kukimbia. Dakika kumi Baada ya Majambazi kuondoka, Ndipo Polisi walifika na kuanza kufyatua risaisi Hewani. KUtokea sehemu ya tukio hadi kituo cha Polisi ni umbali wa KM 1 tu, lakini Polisi walichelewa. Majambazi walitumia kama dakika 10 tu wakaondoka.
Pesa iliyoibiwa haijafahamika kwani alikuwa bado hajafunga Mahesabu. Ila Mteja mmoja mwenyeji wa Rusumo alikua katoa Mil 1 ambayo Majambazi waliondoka nayo.