Majambazi sugu watano wauwawa mbeya

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923

Majambazi.JPG

MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.

Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.

Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.

Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.

Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

CHANZO: Mbeya yetu
 
Du! Wanaume tumeumbwaei,, matesooo mateso kuangaika.
Afu demu anakuuliza umeingiza shi ngapi? Au yani umeshindwa kuninunulia blackbery tu!
 
Isijekuwa ndo yale "ririkuwa rikipambana na porisi tukarishinda"!
 
[h=3]MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO JANA MCHANA[/h]

DSC00199.JPG

Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha
DSC00203.JPG

DSC00219.JPG

DSC00231.JPG

Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
DSC00233.JPG

Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo
DSC00236.JPG

DSC00265.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

DSC00291.JPG

DSC00294.JPG

MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodhahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio.....

Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.

Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.

Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.

Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

Mbeya yetu

MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO MCHANA - MPEKUZI HURU
 
...Huyu RPC anajitahidi sana, taratibu Mbeya inaanza kusafishika...
 
MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodaiwa kuwa ni majambazi kuuawa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

Alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.

"Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamefariki dunia"alisema kamanda Diwani nakuongeza:.

"Walipofaniwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba, taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya".

Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja na miili yao imeifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi huku akitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
 
niwakumbushe tu watanzania wenzangu na wapenda haki popote mlipo,ni polisi hawa hawa chini ya kamanda Zombe waliwaua wafanyabiashara wa madini miaka kadhaa iliyopita na kuwapora fedha na kisha kusingizia kuwa walikuwa ni majambazi na waliuwawa katika kujibizana risasi..............uchunguzi ukafanyika ikaonekana ni kinyume kabisa,walikuwa raia wema waliuwawa ili waporwe mali zao. Ukiwaangalia polisi hao kama ndio hao walihusika hakuna hata mmoja alikuwa na vifaa maalumu kama bulet proofs kofia ngumu na kadhalika lakini katika majibizano hayo majambazi yote yameuwawa na hakuna hata askari kajeruhiwa?ina maana majibizano hayo yalikuwa ya namna gani!?ina maana majambazi risasi zao walikuwa wanazielekeza upande gani?.....NI MPAKA NDUGU YAKO AUWAWE KWA STAILI KAMA HII NDIO UNAWEZA KUDIG A LITTLE BIT DEEPER ABOUT IT.Kazi ya POLISI ni kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria na sio KUUA hata kama ni majambazi kazi yao ni kuhakikisha wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Nani zaidi ya POLISI hawa anajua kama kweli walikuwa majambazi au lah!?..vipi kama wamepakaziwa tu huu msala na polisi?......vipi kama palikuwa hakuna hata majibizano yoyote yale?........
Nawachukia sana Polisi katika kuingilia kazi za mahakama

MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO JANA MCHANA

DSC00199.JPG

Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha
DSC00203.JPG

DSC00219.JPG

DSC00231.JPG

Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
DSC00233.JPG

Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo
DSC00236.JPG

DSC00265.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

DSC00291.JPG

DSC00294.JPG

MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodhahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

Alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio.....

Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.

Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.

Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.

Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

Mbeya yetu

MAJAMBAZI MATANO YAUAWA NA POLISI JIJINI MBEYA LEO MCHANA - MPEKUZI HURU
 
kama ni majambazi kweli ni swala jingine lakini Hakuna hata mmoja mwenye hatia mpaka adhibitishwe hivyo na mahakama,ndio utawala wa sheria unavyotaka. Au ni kwa sababu ni akina kajamba nani watoto wa walalahoi tu?wapo majambazi wa ukweli ambao hawatumii bunduki wanatumia kalamu na athari za ujambazi wao ni kwa kizazi kwa vizazi na tumewakaushia au tunawakamata kistaarabu wanafungwa miaka miwili mitatu wanaachiwa kama kina LYUMBA tu. Mambo kama haya ndio niliambiwa yanaitwa double standards.
Ni dhahiri tuwapongeze polisi kwa kazi nzuri, hatuna huruma na majambazi....wafe tu...
 
niwakumbushe tu watanzania wenzangu na wapenda haki popote mlipo,ni polisi hawa hawa chini ya kamanda Zombe waliwaua wafanyabiashara wa madini miaka kadhaa iliyopita na kuwapora fedha na kisha kusingizia kuwa walikuwa ni majambazi na waliuwawa katika kujibizana risasi..............uchunguzi ukafanyika ikaonekana ni kinyume kabisa,walikuwa raia wema waliuwawa ili waporwe mali zao. Ukiwaangalia polisi hao kama ndio hao walihusika hakuna hata mmoja alikuwa na vifaa maalumu kama bulet proofs kofia ngumu na kadhalika lakini katika majibizano hayo majambazi yote yameuwawa na hakuna hata askari kajeruhiwa?ina maana majibizano hayo yalikuwa ya namna gani!?ina maana majambazi risasi zao walikuwa wanazielekeza upande gani?.....NI MPAKA NDUGU YAKO AUWAWE KWA STAILI KAMA HII NDIO UNAWEZA KUDIG A LITTLE BIT DEEPER ABOUT IT.Kazi ya POLISI ni kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria na sio KUUA hata kama ni majambazi kazi yao ni kuhakikisha wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Nani zaidi ya POLISI hawa anajua kama kweli walikuwa majambazi au lah!?..vipi kama wamepakaziwa tu huu msala na polisi?......vipi kama palikuwa hakuna hata majibizano yoyote yale?........
Nawachukia sana Polisi katika kuingilia kazi za mahakama

Ndugu uangu endapo kama ulishafanya kazi ya Upolisi hata Polisi Jamii, au umeshafanya kazi na askari wa Defenda, sidhani kama ungelisema maneno haya.

Mimi binafsi siyo Polisi wala Askari / Polisi jamii lakini ni raia wa kawaida. Nilishafanya kazi na askari waa defenda ya Central Polisi DSM kupambana na wahalifu kama hawa (siwezi kusema kwa namna gani) na nilikuwa nao bega kwa bega mitaani. Hivyo najua jinsi wanavyopata shida na kuhatarisha maisha yao wakati wanapambana na hawa jamaa. Na huwa wanachukia sana kunapotokea tukio kisha Jambazi akaachiwa mahakamani.

POLE SANA NDUGU HUENDA UMEPOTEZA DUGU AU JAMAA KATIKA TUKIO HILI la MBEYA AU LINGINE.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mh! Jambazi sugu hata hao polisi hawajui majina yao? Mara nyingi najua waharifu sugu records zao zipo polisi

Hao wamechinjwa tu. Naona vigumu kuamini kuwa waliwajeruhi watu watano na halafu wote wakafia njiani au hospitalini.
 
Isijekuwa ndo yale "ririkuwa rikipambana na porisi tukarishinda"!

Same story everyday. Angalia picha zinazofuata majeraha ya risasi kichwani at very close range. Theory ya kufukuzana tena wakitumia gari haipo kabisa nayo gari haina tundu la risasi hata moja. NO PLEASE EXCUSE US MR OFFICER.
 
Polisi kuna kila aina ya vizibiti,kuna bunduki pale,kuna magunia ya bange kuna madawa ya kulevya wakiamua kukupandikizia ni swala la kuingia stoo tu na kukubambikia. Wewe au mimi na wengine wowote tuna uhakika gani kama jamaa kweli walikuwa majambazi?tuna uhakika gani kama hawajabambikiwa washkaji na polisi kama tu walivyobambikiwa wafanyabiashara wa mahenge na akina Zombe?Sasa inawezekanaje watuhumiwa wote wafe kama sio kuficha ushahidi kweli?....Tunahalalisha mauaji hapa kwa njia kama hizi. Ndugu zetu kibao wanasota kwa kubambikiwa kesi na kibao tushawapoteza.kuna mchangiaji mmoja kachangia kwa kusema haiwezekani majambazi sugu wasijulikane majina yao.....Wote wafe,wote kabisa na hata mmoja asibakie kweli?........Sio mpaka auwawe ndugu yako ndio ukemee,anza sasa

Je, yawezekana kuwa na hata hizo silaha alizoshika Kamanda ni uongo hawakukutwa nazo watuhumiwa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kwa waliowahi kuvamiwa na kudhurika na majambazi wakiona hili tukio nadhani itakuwa faragha kwao
ila upande mwingine ni uonevu mkubwa sana,kuna majambazi wa mabilioni ya fedha za kodi ya wananchi na wanajulikana vizuri sana lakini wanachekelewa na kupendwa sana tena mwaka 2015 wanajiandaa kugombea uraisi,ubunge na vinginevyo na sisi baadhi yetu tuliowengi watanzania tumetoa ahadi ya kuwapa support,sasa hawa vibaka wakihisiwa tu kwamba ni wezi basi ni risasi tu bila huruma
KWELI NI HAKI HAKI HII?
 
Back
Top Bottom