Majambazi sugu watano wauwawa mbeya

Majambazi sugu watano wauwawa mbeya

Hata kama waliuliwa njiani poa tu haina haja ya kuwa na huruma na Majambazi...hata wao hawana huruma

Sent from BlackBerry
 
Mh! Jambazi sugu hata hao polisi hawajui majina yao? Mara nyingi najua waharifu sugu records zao zipo polisi

Eti wamepata taarifa za kiinterijinsia, halafu hawawafahamu! Jamani Police tuache utani, isijekuwa mnawaua watu na kuwapora mali zao then mnawaita majambazi! Mie siwaamini police wetu kabisa, wanaweza kukufanyia kitu chochote ili wachukue ulichonacho.
 
Polisi kuna kila aina ya vizibiti,kuna bunduki pale,kuna magunia ya bange kuna madawa ya kulevya wakiamua kukupandikizia ni swala la kuingia stoo tu na kukubambikia. Wewe au mimi na wengine wowote tuna uhakika gani kama jamaa kweli walikuwa majambazi?tuna uhakika gani kama hawajabambikiwa washkaji na polisi kama tu walivyobambikiwa wafanyabiashara wa mahenge na akina Zombe?Sasa inawezekanaje watuhumiwa wote wafe kama sio kuficha ushahidi kweli?....Tunahalalisha mauaji hapa kwa njia kama hizi. Ndugu zetu kibao wanasota kwa kubambikiwa kesi na kibao tushawapoteza.kuna mchangiaji mmoja kachangia kwa kusema haiwezekani majambazi sugu wasijulikane majina yao.....Wote wafe,wote kabisa na hata mmoja asibakie kweli?........Sio mpaka auwawe ndugu yako ndio ukemee,anza sasa


Yaani mimi ukishanitajia jina jambazi/ mwizi/ mchawi tu huwa sina huruma kabisa natamani kumchinja. Kwani wanarudisha maendeleo ya mtu binafsi nyuma.

Fikiria umenunua mali ndio unaanza maisha na huenda umepata kwa mkopo wa Benki/taasisi ya fedha kisha mtu anakuja anakuibia. Wewe unabaki maskini na bado una deni linakuandama.

ACHENI KUTETEA HAWA WATU.

Kama hatuna uhakika na kusema eti mbona gari haina tundu la risasi!!!!! hii inategemea na mazingira, huenda kama walitelemka usitegemee ikawa na risasi.

KWa ushahidi labda kama kuna waliopo eneo la tukio humu JF watueleze kwani tunaambiwa mambo haya yaifanyika mchana kweupeeeeee


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa uzoefu wangu wa kuishi katika mji wenye ujambazi wa kutisha, kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 90 kuwa hawa waliouawa ni majambazi kweli. Tunaishi n majambazi mitaani na tunafahamu hadi matukio waliyofanya lakini hatuthubutu kunyanyua mdomo kuongea maana taarifa zinarudi kwao wanakuja wanafanyiza. Na wanapouawa tunashukuru. Hao wa huko Mbeya siwajui, lakini wale waliowahi kuuawa katika mji nilioishi niliwafahamu kwa muda mrefu kabla hawajauawa, ni majambazi. Pengine hamjui kuwa hata polisi wanawafahamu sana hao jamaa na matendo yao, na matukio mengine hupangwa kwa makubaliano kabisa! Kuna majambazi wamewahi kuuawa kwa sababu ya kukiuka makubaliano au kwa sababu ya kufanyiza na kuumiza penye maslahi ya mkubwa. Nilikuwa naishi Temeke mwaka ule majambazi walipoua askari pamoja na mbwa wa polisi. Wale majambazi walisakwa na kuuawa wote.
 
Back
Top Bottom