#COVID19 Majaliwa, Jaffo na Vigogo Afya Waachie Ngazi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,862
35,869
Ni jambo la kheri kuwa sera rasmi kuhusiana na Covid-19 hatimaye imebadilika uelekeo kwa nyuzi 180. Kwamba kama uelekeo ulikuwa mashariki, tumegeuka nyuma kuelekea magharibi.

Mwanga mpya wa matumaini unaanza kujitokeza. Chanjo toka kwa wahisani tuliowaanzishia mabeberu zimeanza kutufikia bila malipo.

Utaratibu wa haraka na ufanywe sasa ili chanjo zilizopo zianze kutolewa kwa wanaozihitaji pasipo na muda kupotea tena.

Ikumbukwe tulikuwa tumetanga mbali huku tukijidanganya kuwa tuko vizuri:


Wakati hali kamili mahospitalini ikiendelea kuwa mbaya zaidi:

Your browser is not able to display this video.


Tungali na tatizo kubwa la uelewa lilosababishwa na porojo za awamu ile kuhusiana na huu ugonjwa.

Wasiokubali bado kuwa ugonjwa huu upo na wala si vita vya kiuchumi wangalipo na ni wengi. Wasiokubali chanjo kuwa ni salama, upigwaji na zenye kushutumiwa kuteketeza afya zetu kama njama tu za mabeberu nao wangalipo na si wachache.

Kuwafumbia macho waliotufikisha hapo bila kuwawajibisha, hakuwezi kuwa na manufaa. Ni muhimu sana waliokuwa vinara wa upotoshaji huu wakaachia ngazi wenyewe kwa manufaa ya taifa kwa kujiuzulu au kwa kufurushwa.



Kwamba mawaziri Majaliwa, Jaffo na vigogo wote wizara ya afya wangalipo ofisini kuendelea na mapambano na ugonjwa huu? Bado wana dhima ipi hawa dhidi ya ugonjwa huu?

Kuwa na timu mpya kutaleta msukumo na mwanzo mwingine utakaotuletea kuwa na tija zaidi. Kutambua na kukiri wazi wazi kuwa tulipotoka kutapunguza ukakasi kwenye kuwataka waumuni wa awamu ile nao kubadilisha uelekeo.

Hii pia ingekuwa funzo kwa wote kwenye kusisitiza uwajibikaji katika dhidi ya maslahi yoyote binafsi.

 
Majaliwa, Mwigulu, Ndugai, Ndugulile, Mpango na Gwajima hawa ndiyo wamempora samia Ikulu na hata kukamatwa kwa Mbowe na kubambikiwa kesi mbaya ya kigaidi eti kupanga njama za za kuwaua Viongozi wa juu Serikalini. Ni hawa ndiyo wahusika. Kumbuka ni huyu huyu mhuni Mwigulu ambaye alimbambikia afisa usalama wa Chadema kesi FEKI ya kubambikia na kudai ushahidi alioukusanya utakubaliwa hata mbinguni. Kesi ile ilisikilizwa mara mbili na mara zote ilipigwa chini kwa kutokuwepo ushahidi wa kutosha.

 
Mama anaupiga mwingi sana,
 
Scam...!
 
Hata wale bobby waliotumika kuzima mkutano wa kujadili katiba mpya waombwe radhi.

Kwa hakika hapa ilikuwa kwenye kuwaangazia manguli hawa wa COVID-19 kwanza.

Hakupaswi kuachwa jiwe moja bila kuligeuza.

Angalizo moja baada ya jingine chakula kinapoendelea kutokota.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Hadi wewe umeanza kuokota habari? Uzoefu wako wote hata JF umeshindwa hata kutunga story yako ya uongo na kweli? Tehee
 

Kwa hapa mwanzo mpya ni njia pekee.

Cabinet mpya na system nzima.

Tatizo mama bila kutokea kusafisha hali ya hewa naye haaminiki tena.

Cc: Sky Eclat
 
Reactions: BAK
Waende wapi maskini ya Mungu hata kujiajiri hawawezi
 
Ukimya wake unashangaza sana.

Kulikuwa na uzi hapa kumtaka msimamo:


 
Reactions: BAK
Angalia uongo wa polisiccm kuhusu kukamatwa kwa Mbowe. Hivi yule dhalimu mwendazake kama Mbowe angekutwa na hatia ya kupanga njama ya kuua Viongozi wa juu Serikalini angemwacha huru tangu September mwaka jana?
 
Jamani acheni kubalisha maudhui ya hii Thread
Ni kwamba, tulikuwa tunasema mtanyooka na COVID, na mtakubali sayansi na sio imani mlizopandikizwa na hao hao waliowaletea hizi imani zenu za kidini na waliokuwa wanaambia kuna mdudu COVID, hajui imani wala maombi, ni anaua kwa kwenda mbele.
Na mabeberu hamuwezi na wala hamtaweza kushindana nao, na wanawaletea chanjo mtake au hamtaki, na sio kuwasaidia, ni kwanba hawawezi kuaacha ka inchi ka viroboto kama katanzania kiendelee kusambaza na kutengeneza variants ambazo zitasambaa dunia nzima na kuvuruga taratibu za maisha ya mabeberu
Tanzania sio nchi ni kaanchi masikini na kadogo mno kwenye dunia ya mabeberu.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…