Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia.

Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi.

Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya awamu ya tano kwa awamu ya sita.

Haikuwa ajali kwa awamu ya tano kujikita katika kujitanabaisha kwa nguvu zote kuwa ilikuwa ni ya wanyonge. Yaani wapiga debe, machinga, mama lishe, bodaboda na wa namna hiyo. Makundi haya yatoshe kuwakilisha aina ya philosophy iliyokuwa ikizisukuma agenda za serikali ya awamu ya tano.

Aina ya mafikara ya watu hao ndiyo yaliyokuwa yakiichezesha ngoma yote ya kiutawala tokea juu hadi chini. Ndiyo maana hadi leo, hata bungeni kunasikika wazi wazi sauti zenye kuhimiza kutambuliwa ubora wa wahitimu wa darasa la saba dhidi ya maprofesa au wasomi kwa ujumla.

Imani potofu zilizoambatanishwa na Corona zikiwamo upigaji nyungu, maombi, michai chai, malimao nk ni mwendelezo wa mafikara au philosophy ya watu wa makundi hayo.

Kwenye awamu ile, upepo wa mafanikio serikalini ulilihitaji zaidi kundi hilo la wasioelimika. Watendaji wakiwamo Mawaziri na wote wenye njaa zao walilazimika kuukana ukweli na hata kuzikana taaluma zao ili kuweza kukubalika kundini.

Ya akina Gambo leo na wote wanaoitisha kutolaumiwa kama wao binafsi, bali hali nzima ya utawala iliyokuwapo wakati huo ni mwendelezo wa matokeo hayo hayo.

Tulipo leo chanjo ya UVIKO ipo njiani kuja. Bila shaka jambo hili ni la kheri kabisa. Lakini si ajabu kuwa hii nalo litakutana sasa na kundi lile lililokuwa limeaminishwa kuwa ugonjwa haupo, bali ni vita vya kiuchumi tu dhidi ya Tanzania. Tena kuwa chanjo ni biashara na zaidi sana ni sumu dhidi ya Waafrika na hasa Watanzania.

Siyo siri tuko pabaya sana bila ya kuyashughulikia madhara haya yaliyopandikizwa kutokea awamu ya tano wakati ilipokuwa katika kujitafutia uhalali wa kuwepo kwake.

Matatizo tuliyo nayo kuhusiana na kundi hili yanapaswa kufahamika ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kamili. Hii ikiwa ni wa muda mfupi na hatimaye wa kudumu.

Kuuishi ukweli na haki hata kama kwa kufanya hivyo pana machungu yake ni mambo yasiyoepukika.

Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na "the brainwashed to be catered for." Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia. Kunatakikana jitihada kubwa za dhati na za pamoja katika kuyaweka mambo sawa.

Ni vizuri kufahamu kuwa tuna kundi kubwa la watu wasiojua nini wanataka au nini hawataki. Hii ikiwa ni kwa sababu tu ya kukosa elimu kulikokolezwa vilivyo na kupotoshwa kulikofanyika kwa makusudi.

Ya DC na DED Morogoro ni mwendelezo wa yatokanayo na mitizamo ya kundi hili ambayo hayajapatiwa suluhisho.

Kwa pamoja tunaweza kuyaweka mambo sawa hatimaye. Hata hivyo si haba kutambua kuwa pana mlima mkali kweli kweli wa kupanda.

Penye nia pana njia.

Ninawasilisha.
 
Mama yuko Ikulu miezi mitatu pamoja na kuwa si kipindi kirefu lakini kuna mengi ambayo angestahili kuyamaliza ndani ya kipindi hiki cha miezi mitatu. Kuendelea kwake KUDEMKA kunaonyesha hana nia ya kuleta demokrasi ya kweli nchini.

Atagusa gusa hapa na pale na kukutana na makundi ya Watanzania yasiyohusu kitu kwani hayamwambii ukweli husika kisha atachanja mbuga kuelekea 2025 kufanya mwizi mwingine wa kura. Mimi na magufuli ni KITU KIMOJA. Katiba mpya mtasubiri sanaas. I rest my case.
 
Mama yuko Ikulu miezi mitatu pamoja na kuwa si kipindi kirefu lakini kuna mengi ambayo angestahili kuyamaliza ndani ya kipindi hiki cha miezi mitatu. Kuendelea kwake KUDEMKA kunaonyesha hana nia ya kuleta demokrasi ya kweli nchini. Atagusa gusa hapa na pale na kukutana na makundi ya Watanzania yasiyohusu kitu kwani hayamwambii ukweli husika kisha atachanja mbuga kuelekea 2025 kufanya mwizi mwingine wa kura. Mimi na magufuli ni KITU KIMOJA. Katiba mpya mtasubiri sanaas. I rest my case.

Kama ingekuwa kweli kwamba yeye na JPM ni kitu kimoja, kile kitabu cha kurasa 303 ambacho Anko alitembea nacho kwa siku ^see-tea-knee^ za kampeni za uchaguzi, asingekitupa wala kukiacha kichafuke vumbi vile.
 
Alokwambia wamachinga ni watu wenye elimu duni ni nani??

Nimeishia kusoma kwenye paragraph hiyo inayosema wamachinga hawana Elimu!!

Sina haja ya kukutukana maana nami nitafanana nawe. Bila shaka nawe tunayo kazi ya kukutoa kasumba uliyoveshwa.

Kwamba machinga wewe una elimu kuliko madaktari na maprofesa mlioanza wewe na msukuma kuwazodoa tokea awamu ile? Aaah wapi!

Hukumsikia naibu spika akitaka hao hata wakifikisha miaka 65 wasistaafu?

Bandiko hili kama lilivyotarajiwa litakuwa limekuchoma vilivyo wewe chawa wa awamu ile. Usipate taabu sana lakini. Sindano zote ziko hivyo hivyo. Na hiyo ndiyo iliyo dalili kuwa sasa dawa inakuingia.

Tulia tulio!
 
No point proven. Rather plain confession of total blindness with regard to the scope of the thread!

Okay, I get you, now. Pamoja na kutokuwa fair, kumbe wewe ni total blind pia!??? I accept the confession of your own total blindness. Next time, please, be fair and employ insightful ^blindless^ individuals to do the task for you, sawa!???
 
Okay, I get you, now. Pamoja na kutokuwa fair, kumbe wewe ni total blind pia!??? I accept the confession of your own total blindness. Next time, please, be fair and employ insightful ^blindless^ individuals to do the task for you, sawa!???

Hahaahaaa, what's your point exactly? Can you be specific if you like?

To be honest, up to now you have written totally nothing. To be honest, you haven't started to write anything worth any attention!

Would you also mind to stick to one language please? Should it be necessary I have a Sukuma translator by my side to take good care of you as well 😂😂😂😂😂!
 
Hahaahaaa, what's your point exactly? Can you be specific if you like?

To be honest, up to now you have written totally nothing. To be honest, you haven't started to write anything worth any attention!

Would you also mind to stick to one language please? Should it be necessary I have a Sukuma translator by my side to take good care of you as well 😂😂😂😂😂!

How in the world would anyone in their right mind even need someone of your sort as their cognoscente!???
 
How in the world would anyone in their right mind even need someone of your sort as their cognoscente!???

Another reminder: "Once you are ready for a meaningful discussion you may indicate so. You have the entire thread available." This is with a note (though) now marked in red for your convenience:

IMG_20210618_002640_205.jpg
 
Mama yuko Ikulu miezi mitatu pamoja na kuwa si kipindi kirefu lakini kuna mengi ambayo angestahili kuyamaliza ndani ya kipindi hiki cha miezi mitatu. Kuendelea kwake KUDEMKA kunaonyesha hana nia ya kuleta demokrasi ya kweli nchini. Atagusa gusa hapa na pale na kukutana na makundi ya Watanzania yasiyohusu kitu kwani hayamwambii ukweli husika kisha atachanja mbuga kuelekea 2025 kufanya mwizi mwingine wa kura. Mimi na magufuli ni KITU KIMOJA. Katiba mpya mtasubiri sanaas. I rest my case.

Mkuu BAK heshima kwako.

Ninakuelewa mtazamo wako na nia yako njema ya kuyahitaji mema yote kutokea leo. Ni kweli kwa nini liwezekanalo leo lingoje kesho?

Binafsi ningependelea waliotupotosha wote na popote wasiwemo ofisini kufikia sasa. Lakini yote hayo ni nadharia. Mama ni yeye na sisi ni sisi kumpa benefit of doubt ndiyo mwendo. Hawezi kufanya kila kitu kwa kasi ambayo tungependa sisi. Huo ni ukweli mchungu.

Mama karithi nchi iliyokuwa ikiendeshwa kama ilivyoonyeshwa kwenye mada ambapo katika mashabiki wake wakuu walikuwa ni wale sungusungu kama ulivyowaona pale Mwanza.

Kundi hilo haliamini kuna Corona. Kundi hilo linadhani lina mawazo bora kuliko hata kina Einstein. Kwenye mazingira hayo kutompa mama muda itakuwa ni kutomtendea haki.

Hapa tulipo tayari masheikh wa uamsho wako nje, kesi 147 za bambikizi TAKUKURU zimefutwa, kina Mdude wako njiani kutoka, watu hawapotei tena, kina SABAYA wako mikono salama, kina bashiri, chaku nk nk waliokuwa waasisi wa mengi ya awamu ile hawana ushawishi tena.

Mama kasema yeye = JPM. Kwani kuna taabu? Wanasema mwana wacha kupiga mayowe waache waone wenyewe!

Leo nyungu, michai chai, malimao nk hakuna anayeyakumbuka kasoro ya hao sungusungu na ndugu zao wakiwamo wapiga debe na vibaka. Tulipo COVAX i njiani kuja. Tunataka nini kwa Mungu sisi? Maneno?

Tuweni na subira Mama anahubiri haki. Kwa maneno yake kathubutu kutamka "haki huinua taifa." Inshallah atatupa katiba mpya ambayo ndiyo ulio mzizi wa fitina yote tunayoiona.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Heshima kwako pia Mkuu 🙏🏾. Ngoja tusubiri lakini alipokula kiapo huku akiwa ameshika kitabu kitakatifu cha dini yake na kutamka atailinda na kuitetea Katiba ya nchi halafu huu mwezi wa tatu sasa anajua fika kwamba kuwepo Bungeni kwa COVID-19 ni uvunjwaji wa katiba kwa Wabunge FAKE kuendelea kulipwa billions of taxpayers money na yeye yuko kimya ni UNAFIKI wa hali ya juu kuhusu kwenda kinyume na kiapo chake.
Na wahenga walisema siku njema huonekana asubuhi na asubuhi inazidi kuyoyoma ni 11:00am now she is fast approaching 12 noon.
Tusubiri ila mimi machale YAMESHANICHEZA pamoja na kuwa baadhi ya mambo aliyoyafanya hadi sasa nayafurahia na kuyaunga mkono.


Mkuu BAK heshima kwako.


Ninakuelewa mtazamo wako na nia yako njema ya kuyahitaji mema yote kutokea leo. Ni kweli kwa nini liwezekanalo leo lingoje kesho?

Binafsi ningependelea waliotupotosha wote na popote wasiwemo ofisini kufikia sasa. Lakini yote hayo ni nadharia. Mama ni yeye na sisi ni sisi kumpa benefit of doubt ndiyo mwendo. Hawezi kufanya kila kitu kwa kasi ambayo tungependa sisi. Huo ni ukweli mchungu.

Mama karithi nchi iliyokuwa ikiendeshwa kama ilivyoonyeshwa kwenye mada na katika mashabiki wake wakuu ni wale sungusungu kama uliowaona pale Mwanza.

Kundi hilo haliamini kuna Corona. Kundi hilo linadhani lina mawazo bora kuliko hata kina Einstein. Kwenye mazingira hayo kutompa mama muda itakuwa si kutomtendea haki.

Hapa tulipo tayari masheikh wa uamsho wako nje, kesi 147 za bambikizi TAKUKURU zimetufutwa, kina Mdude wako njiani kutoka, watu hawapotei tena, kina SABAYA wako mikono salama, kina bashiri, chaku nk nk waasisi wa mengi ya awamu ya tano hawana ushawishi tena.

Mama kasema yeye = JPM. Kwani kuna taabu? Wanasema mwana acha kupigana mayowe waache waone wenyewe.

Leo nyungu, michai chai, malimao nk hakuna anayeyakumbuka kasoro ya sungusungu na ndugu zao wakiwamo wapiga debe na vibaka. Tulipo COVAX i njiani kuja. Tunataka nini kwa Mungu sisu? Maneno?

Tuweni na subira Mama anahubiri haki. Kwa maneno yake kathubutu kutamka "haki huinua taifa." Inshallah atatupa katiba mpya ambayo ndiyo mzizi wa fitina yote tuionayo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom