Majaliwa hana mamlaka Zanzibar

Majaliwa hana mamlaka Zanzibar

Huu ni wehu, kwenda kwenye boma ya mtu na kumwagiza mke wa mtu asinunue kuku kwa sababu alio nao wanamtosha wakati baba mwenye nyumba ka kaa kwenye kochi anajuangalia tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu 3678 kama sijakosea🙁🙁
Sasa kwa nini mh Tuly anapoteza nguvu kuubwa kugombea huko Mbeya? Si angewanunulia hiyo sukari yote hao wazenj wakagawiwa bure mwaka mzima?? Yeye angeungwa mkono na kiwanda kingeongeza uzalishaji na kula angepewa zoooote Zenj.
Sijui tunakwamia wapi kimawazo. Hadi kwenda katia kadi ya bima huko Mbeya?? Bima hailiwi sukari huliika yakhee
 
Majaliwa ni Waziri Mkuu wa JMT, Zanzibar ni sehemu ya JMT, hivyo ana mamlaka yote kuhusu Zanzibar kwa jambo lolote hata la Zanzibar as far as JMT itahusika.

Biashara sio jambo la muungano, lakini biashara ya sukari ya Zanzibar imekuwa na siasa ambazo serikali ya JMT inahusika direct, hivyo Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa yulo very right kuingilia kati.

Zanzibar inakiwanda cha sukari kinazalisha sukari ya kutosheleza soko la Zanzibar, huku wafanyabiashara ya uagizaji sukari, wakiagiza sukari kutoka nje at cheaper prices kuliko hiyo sukari ya Zanzibar na matokeo yake ni sukari ya Zanzibar imedodea kiwandani wakataka kuiingiza bara, tukawagomea!.
P
Point, na wasome na kuelewa...
 
Mtapokea maagizo ya waziri mkuu kwa sababu moja tu, Zanzibar ni sehemu ya URT.Leo mmesahau pindi mnavyowategemea mabeberu pale serikali inapokunjua makucha dhidi ya wahalifu wa mitandao na utakatishaji wa fedha.Vipeperushi toka ulaya mkiviona mnashashadiaje eti ooh mbinyo wa USA mara EU, ujinga mtupu.Leo Majaliwa ambaye katiba nimempa Malala kaongea tayari mnakuja kinyume. Mipinzani ya bongo hasara kabisa.
Hujui unachoongea, unasikiliza sana ngonjera na propaganda za CCM,..

Katiba ya Tanzania na ya Zanzibar imeweka wazi, kuna mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano sasa shida iko wapi??
 
Waziri mkuu ametoa agizo msiruhusu kuingiza sukari toka nchi za nje.
Ili sukari inayozalishwa Zanzibar ipate soko, mnalalamika.
Masuala ya bandari ,usafiri wa anga posta na mawasiliano ni masuala ya Muungano. Je hiyo sukari toka nje haipitii bandari ya Zanzibar?
Wafungulieni soko la sukari Tanganyika kwanza, nakumbuka wenye viwanda vya sukari pale Mahonda walipigania sana wapate soko la kuuza sukari yao Tanganyika lakini mliwakatalia, sasa kelele za nini?
 
Hata hadhi ya mkoa haina, kati ya Ukerewe na Unguja ipi kubwa?
Ukubwa au udogo wake sio sababu ya kuwa isiwe na hadhi iliyonayo, kuna nchi ndogo kama vile Tuvalu na Nauru zenye raia 11,000 - 13,000 repectively. Zina hadhi na zinatambuliwa kuwa ni nchi. Acha dharau.

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Wafungulieni soko la sukari Tanganyika kwanza, nakumbuka wenye viwanda vya sukari pale Mahonda walipigania sana wapate soko la kuuza sukari yao Tanganyika lakini mliwakatalia, sasa kelele za nini?
Out of point. Issue ni mamlaka ya waziri mkuu.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hana mamlaka ya kuingilia na kutoa maagizo kwa mambo ya #Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984 imeainisha waziwazi mamlaka ya Serikali mbili zilizopo." @MazruiNasso
View attachment 1329197

====
Zbr ni kimkoa tu ndani ya nchi ya Tz. Kupewa hadhi ya kuitwa nchi kusiwachanganye nyie vijana. Ndio maana the so called Rais wa Zbr akiwa kwenye vikao vya Cabinet ya URTZ hadhi yake ni sawa na mawaziri wa kawaida tu kama Mzee Kangi.
 
Hilo jina huwa nalishangaa sana wakati yeye ni escott 4 na Rais wa SMZ ni escott 3..Kiuhalisia vyeo vya serikali kuu vimekaa shaghala baghala tu ilimradi liende. Sasa escott 3 hana mamlaka na Tanganyika wakati escott 4 ana mamlaka na Zanzibar. Pia kwenye cabinet makamu wa Rais na Rais wa SMZ wanakaa next to president wakati waziri mkuu anakaa next to VP.
Acha uongo. Kwenye Cabinet Rais wa Zbr ni mjumbe wa kawaida sana. In short akiwa pale anafuata maagizo ya baba jesca.
 
Biashara za ndani ya Zanzibar si mambo ya Muungano,wafanyabiashara wa Zanzibar wanakatwa KODI mbili TRA na ZRB..

Kwahiyo sijui anaongelea kodi gani??
Na hili wengi nahisi hawalijui, na pia bado bidhaa ziko bei chini Zanzibar.

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Kujeni taratibu tusije kuanza tena mambo ya kupelekana vizuizini, maana kuchezea sharubu za simba siyo jambo jema sana
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hana mamlaka ya kuingilia na kutoa maagizo kwa mambo ya #Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984 imeainisha waziwazi mamlaka ya Serikali mbili zilizopo." @MazruiNasso
View attachment 1329197

====
IMG_20200121_192914.jpg
 
U
Katiba Inatambua vyombo viwili vya utendaji vyenye mamlaka, Serekali ya Jamuhuri na Serekali ya Zanzibar. Mpaka hapa unaamini Serekali ya Zanzibar ina mamlaka na mambo yake? Tena bila kuingiliwa na Jamuhuri (bara!!).

Katiba mpaka hapa ilibidi iweke na Tanganyika kutenganisha na Zanzibar ili kuondoa mkanganyiko. Mfano Waziri wa Michezo wa bara hausiki na Zanzibar, sasa Waziri mkuu wa bara anahusika vipi na Waziri wa michezo wa Zanzibar?

Ndio maana Jissu kaweka kifungu toka katiba ya Zanzibar kinachopinga Majaliwa kumuagiza Waziri wa Zanzibar.

Kifupi huu mjadala hauna majibu sababu tatizo linaanzia kwenye Katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekuwa unajibu unachoulizwa ingependeza sana ili twende na hoja vizuri na ungekuwa una qoute hivyo vifungu
 
Back
Top Bottom