Maiti afufuka chumba cha maiti - Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti afufuka chumba cha maiti - Iringa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Nov 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG][​IMG]

  MAITI YAFUFUKA IKIWA MOCHWARI YARUDISHWA KWA MADAKTARI


  Mauaza uza yaibuka mjini Iringa baada ya mgonjwa ambaye alifika kufanyiwa maombi kwa mmoja kati ya wahubiri maarufu mkoani Iringa kukata kauli yake akiwa nje ya ukumbi huo maarufu wa maombi mjini hapa na baada ya kufikishwa chumba cha kuhifadhiwa maiti (Mochwari) katika hospital ya mkoa wa Iringa maiti hiyo iliamuka na kupelekea ndugu kuupeleka mwili huo kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

  Mke wa mgonjwa huyo Amina Ramadhan alisema kuwa mme wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa Boaz Sollo wa kituo cha maombezi cha overcomers .

  Hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla marehemu aliamuka na kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu Bi Amina Ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Tadei Ngusi


  Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.


   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hivi kumbe Kukata kauli ni ishara tosha kuwa kesha fariki... strange!!!!
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyo hakufa bwana, alikata kauli. Mtu akizimia wewe kama sio mtaalamu unaweza kujua kesha kufa tayari.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Maiti haipokelewi mortuary mpaka dr a_certify! Stori haijatulia hii
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Soma habari yote kabla ya kutoa comment. Madaktari walithibitisha kuwa ameshakufana na kuruhusu kwamba maiti apelekwe mortuary kama ifuatavyo hapa chini:
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Soma kwanza story yote tangu mwanzo hadi mwisho kabla ya kutoa comment. Paragraph ya hapo chnini ambayo ni ya mwisho wa habari inahitimisha kwamba maiti ilikuwa certified by the doctor.

   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni madaktari wetu si werefu wa kutumia vema utaalamu wao. Huyu mgonjwa alikufa nusu kaputi, mapigo ya moyo yalikuwa chini sana, na hivyo kuna vyombo kadhaa vinavyotumika kupima kuhakiki uhai wa mgonjwa au umetoweka kabisa. Hii ni aibu sana kwa taaluma ya waganga.
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Wakati ndugu yangu alipofariki recently how l wished muujiza kama huo ungetokea! Yaani hata siku ya pili tunavalisha Nguo ready kwa safari kuelekea kwetu bado nilikuwa nawish pamoja na kwamba mwili wake ulikuwa na baridi ya kutoka kwenye jokofu!

  Mungu ampe miaka zaidi huyo mkaka; ni relief kubwa kwa familia! Haijalishi ni muujiza au alikuwa kwenye coma kikubwa ni mzima sasa!
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  tuchukue lipi, amefariki au amerudiwa na uhai? Kama amerudiwa na uhai, mke wake anaitwa mjane, na aliyerudiwa na uhai anaitwa marehemu? Unajichanganya mwenyewe, kifupi hueleweki. Jipange vizuri ndugu
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mke wa mfufuka

  Kwa vyo vyote Mungu anatoa funzo fulani kwetu, si jambo la kawaida maana hata mke wake ni kama haamini vile.
   
 11. u

  utantambua JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapana mkuu, jinsi ulivyoiripoti tafsiri yangu (nadhani na ya king'asti) ni kuwa huyo bwana hakuthibitishwa kama ameshafariki. Ila baada ya "kufufuka" ndipo alipotolewa mochware na kupelekea madaktari kuthibitisha sasa kuwa kweli ameshafariki (ambapo supposedly ndio muda source wa habari hii alipotoka hospitalini hapo)

  Kwangu mimi hakuna kufufuka hapo katika habari hii. Ni kwamba ndugu huyo alikuwa amekata tu kauli (si kufa) hadi pale madaktari walipothibitisha kuwa amefariki. Labda kama kuna maelezo tofauti ya story hii.
   
 12. u

  utantambua JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Alikufa nusu kaputi?
   
 13. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hata ku certify kifo kunahitaji utaalamu gani? Je, una uhakika alionwa na daktari? Au hata hao auxiliary nurses unaowaona hapo juu wewe wawaita madaktari? Siamini kama huyo jamaa alionwa na daktari MD.
   
 14. u

  utantambua JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakuna la kuchukua hapa mkuu. Utata wa story huu unalazimishwa na masimulizi yenye controversy. So ni better kusema hii story iko na confusion zaidi kuliko maajabu ya "kufufuka" ambayo allegedly inasema yametokea
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,008
  Trophy Points: 280
  Pumbavu kabisa, yaani mtu anapelekwa mochwari kabla daktari hajathibitisha kuwa amekufa? Midomo kunuka zao
   
 16. l

  lasix JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  na mimi nimeelewa kama wewe mkuu,labda wengine mtueleweshe vzr kwamba mwisho wa siku jamaa ni mzima au ni marehemu?naona mnajichanganya tu
   
 17. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Kama amefufuka inakuaje mumbatize jina la "Marehemu" na mkewe mumuite "Mjane"?.
   
 18. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Iringa inakuwa kama mbeya sasa,kila siku vituko
   
 19. B

  BABYG.X New Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaaaa, duuhizi si habari za kweli haiwezekani mtu kukatakauli halafu akaoneka bado ni mzima hayo ni maajabu ya dunia hivi dunia hiii inakwenda wapi mungu atunusuru na haya majanga
   
 20. B

  BABYG.X New Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni madaktari wetu si wataalam wa kutumia vema utaalamu wao. Huyu mgonjwa alikufa nusu kaputi, mapigo ya moyo yalikuwa chini sana, na hivyo kuna vyombo kadhaa vinavyotumika kupima kuhakiki uhai wa mgonjwa au umetoweka kabisa. Hii ni aibu sana kwa taaluma ya waganga.
   
Loading...