Maisha yangu yamekwisha?

Maisha yangu yamekwisha?

Napitia hali kama yako, ila nipo makini vibaya sana, mambo mengi namuuliza mke wangu na nikihisi nitaharibu basi huwa natoa maagizo kwa mke wangu afanye, nimejikuta napenda kukaa peke yangu mda wote, sipendi kwenda kanisanai tena kama zamani, ila mm shida ni kuwa tuna mtoto mmoja na kila wife akizaa wanakufa, siwezi kumfukuza coz bado nampenda na hana kosa, ila nimejikuta nachepuka sana.
Pole mkuu ila kuchepuka sio suluhu. Mlijaribu kuhusisha wataalam wa afya labda kujua nini tatizo
 
Anti depressant ziko nyingi,unfortunately nyingi zina side effects,ila hii sio sababu ya kutokunywa dawa,because benefits outweigh hizi side effects hasa kwa mtu symptoms ziko deep km mtoa Mada...
Huyu anaumwa sana na anazihitaji kama ni hivyo
 
Muda ukifika chukua form ugombee urais wa Tandhania.!
Habari wandugu

Mimi ni mwanamume mwenye Umri wa miaka 35 Nina mke na watoto wanne.Tatizo langu ni kwamba ninahisi ninatatizo kubwa la kiakili ingawa sina uhakika.

Nilikuwa mwajiriwa na mara ghafla nikajikuta sitaki kazi bila sababu yoyote ya msingi,morale ikashuka,mahudhurio yakashuka,performance ikashuka na mwishowe nikasimamishwa kazi.Katika kipindi hicho pia nilipoteza upendo kwa familia yangu,watoto wangu,rafiki zangu na hata ndugu.Sikutaka ukaribu na mtu wala sikutaka kusaidiwa wala kusaidia mtu.Nilikuwa namiliko nyumba nikaiuza na kwenda kupanga,nilikuwa na gari nalo nikaliuza.Pesa nikazitapanya tapanya tu mpaka zikaisha.

Mke wangu baada ya kusumbuana naye kwa muda mrefu aliamua kuondoka ila mama yangu alimchukua na kukaa naye pamoja na watoto wangu.Mimi kwa sasa naishi na mwanamke mwingine ambaye nimezaa naye mtoto mmoja lakini si kwamba nampenda bali niko nae tu kama msichana wa kunifulia nguo na kunipikia,Nimehama kwenye nyuma tuliyopanga na mke wangu proper na hata sijui vitu vyangu viko katika hali gani na wala sijui kodi inalipwaje yaani i do not care

NIlikuwa namiliki ofisi tatu za biashara na zote nilizitelekeza sijua hata zina ali gani naisi kila kitu kitakuwa kimepotea ingawa hata sifuatilii wala kujali chochote.

Mimi sisi mlevi ingawa ninakunywa.Mimi sio mjinga kwa sababu nina uelewa wa mambo mengi.Sasa hivi ninakaanga chipsi tena ni siku nikijisikia kufanya hivyo.Mara nyingi huyu mwanamke ninayekaa naye ndia anahangaika kutafuta hela ya kula na kufungua kijiwe chetu cha chipsi.Yaani nimekuwa na tabia na mtazamo wa ajabu kuhusu maisha.Sijali chochote wala yoyote.Nilijiandikisha chuo kuongeza elimu anagalau nitulize kichwa lakini nako nimeshindwa kuendelea mwaka huu kutokana na kukosa Pesa.Nimelipa ada kidogo lakini nimejikuta sina interest bali naona kama napoteza tu muda.

Hapo nilipo sina interest na jambo lolote wala mtu yoyote.Hata marafiki zangu wala ndugu zangu.Niko Niko tu.

Ukiniona huwezi fikiri kwamba nimepoteza muelekeo wala huwezi hisi kwamba nina mambo magumu lakini nahisi kabisa ninachanganyikiwa na ninajizuia kwa nguvu sana.

Sijui kwa nini nimekuwa hivi.Kila nikitulia najiuliza lakini sipati majibu nikijaribu kubadilika najikuta narudi kulekule.

Ni mambo mengi sana mabaya ambayo yanaendelea kwenye maisa yangu ila haya ni kwa uchache.Tafadhali mnisaidie tatizo langu ni nini?

Jambo pekee ambalo limebaki kwenye kichwa changu ni kutafakari mustakabali wa nchi yetu.Nimejikuta natumia muda mwingi na nguvu nyingi kufuatilia siasa za nchi yetu ingawa hata sina interest na siasa kivile

Tafadhali kama kuna anayeweza kunisaidia kutambua tatizo langu hili au kunishauri aniambie kitu cha kufanya maana kwa sasa kichwa changu kimechoka sana.

Please help if you can.

Shida yangu,sio pesa nahitaji mtu atakeyeweza kunipa muongoza upya katika maisha yangu kabla sijapotea kabisa.Nimeboreka sana na maisha sina interest yoyote na maisha.Sijawahi kufikiria suicide,wala sihisi kukata tamaa bali nahisi kwamba interest yangu na maisha imeshuka sana bila sababu ya kueleweka
 
Sipendi marafiki,
Sidumu kwenye mahusiano,
Sitaki kuoa,
Sitaki kuishi na mtu,
Sipendi kusaidia,
Sipendi kusaidiwa,
Sipendi kazi yang,
Ni mkali kuliko kawaida,
Sipendi kelele,
Sipend malumbano na ushindani,
Napenda visasi na lawama,
Sipendi kuuliza (mfano naenda sehem naweza nisiulize mpaka gari ikanipitisha)
Sipendi kuulizwa (naweza kuulizwa kitu najua ila nikasema sifaham)
Kisirani moto
Nongwaa
Nakasirika ovyo

Ni mengi yananizonga nilizani ni peke yangu kumbe tupo wengi
Mkuu we utakuwa mad fresh
 
Inabidi utafute viongozi wa dini na wataalamu wa ushauri nasaha waikomboe nafsi kutoka katika umauti mana mda sio mrefu utaidhuru nafsi yako
 
Meza haloperidol haraka sana hilo tatizo ndani ya mwezi m1 litaisha na utarudisha mood yako una psychotic disorders bila kujijua so unaitaji antipsychotics au nenda hospital kitengo cha psychiatry watakusaidia
 
Nakushauri ujenge mazoea ya kusoma vitabu mbalimbali
Anza kijijali mwenyewe.
Taka a vacation somewhere at the beach on weekends
Go to your previous employer try to re connect
Get rid of all women for sometimes
Tafuta marafiki waliofanikiwa jiweke karibu nao
 
1. Kuwa Positive, Usisikilize kitu ambacho ni Negative kwa Nchi yako wala kwa Familia yako na hata kwenye Biashara zako.

2. Ipe nafsi yako thamani inayostahili, Fanya kazi kwa bidii familia iwe ya kwanza katika kila mahamuzi utakayo chukua.

3. Samehe na sahau kwa wote walio kukosea na pia fikiria zaidi kuwa wewe ni nguzo kwa kizazi chako.

4. Sikiliza Music TBC International na Sikiliza TBC taifa kuna Sera za kukujenga na kukupa moyo na kubwa zaidi kujua Taratibu na Sheria za Nchi yako.

5 . Kila jambo unalofikiria kabla ya kufanya jipe nafasi na kisha Sema Mungu ni mkubwa kabla na baada.N.B nimeweka Mungu mwisho kwa sababu Mungu yupo ndani yako na yeye ndio alisimia zoezi mpaka unazaliwa kati ya Mamilioni.
 
Hahahahah [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndio maana jamiiforums nipenda kuliko mitandao yote aise inavituko na inachekesha yaan nikiwa humu unakuta nacheka kwa saut mpaka watu. Wananishangaa nacheka nn
We jamaa upo vizur hongera kwa kuuelewa huu msamiati.[emoji23]
 
Habari wandugu

Mimi ni mwanamume mwenye Umri wa miaka 35 Nina mke na watoto wanne.Tatizo langu ni kwamba ninahisi ninatatizo kubwa la kiakili ingawa sina uhakika.

Nilikuwa mwajiriwa na mara ghafla nikajikuta sitaki kazi bila sababu yoyote ya msingi,morale ikashuka,mahudhurio yakashuka,performance ikashuka na mwishowe nikasimamishwa kazi.Katika kipindi hicho pia nilipoteza upendo kwa familia yangu,watoto wangu,rafiki zangu na hata ndugu.Sikutaka ukaribu na mtu wala sikutaka kusaidiwa wala kusaidia mtu.Nilikuwa namiliko nyumba nikaiuza na kwenda kupanga,nilikuwa na gari nalo nikaliuza.Pesa nikazitapanya tapanya tu mpaka zikaisha.

Mke wangu baada ya kusumbuana naye kwa muda mrefu aliamua kuondoka ila mama yangu alimchukua na kukaa naye pamoja na watoto wangu.Mimi kwa sasa naishi na mwanamke mwingine ambaye nimezaa naye mtoto mmoja lakini si kwamba nampenda bali niko nae tu kama msichana wa kunifulia nguo na kunipikia,Nimehama kwenye nyuma tuliyopanga na mke wangu proper na hata sijui vitu vyangu viko katika hali gani na wala sijui kodi inalipwaje yaani i do not care

NIlikuwa namiliki ofisi tatu za biashara na zote nilizitelekeza sijua hata zina ali gani naisi kila kitu kitakuwa kimepotea ingawa hata sifuatilii wala kujali chochote.

Mimi sisi mlevi ingawa ninakunywa.Mimi sio mjinga kwa sababu nina uelewa wa mambo mengi.Sasa hivi ninakaanga chipsi tena ni siku nikijisikia kufanya hivyo.Mara nyingi huyu mwanamke ninayekaa naye ndia anahangaika kutafuta hela ya kula na kufungua kijiwe chetu cha chipsi.Yaani nimekuwa na tabia na mtazamo wa ajabu kuhusu maisha.Sijali chochote wala yoyote.Nilijiandikisha chuo kuongeza elimu anagalau nitulize kichwa lakini nako nimeshindwa kuendelea mwaka huu kutokana na kukosa Pesa.Nimelipa ada kidogo lakini nimejikuta sina interest bali naona kama napoteza tu muda.

Hapo nilipo sina interest na jambo lolote wala mtu yoyote.Hata marafiki zangu wala ndugu zangu.Niko Niko tu.

Ukiniona huwezi fikiri kwamba nimepoteza muelekeo wala huwezi hisi kwamba nina mambo magumu lakini nahisi kabisa ninachanganyikiwa na ninajizuia kwa nguvu sana.

Sijui kwa nini nimekuwa hivi.Kila nikitulia najiuliza lakini sipati majibu nikijaribu kubadilika najikuta narudi kulekule.

Ni mambo mengi sana mabaya ambayo yanaendelea kwenye maisa yangu ila haya ni kwa uchache.Tafadhali mnisaidie tatizo langu ni nini?

Jambo pekee ambalo limebaki kwenye kichwa changu ni kutafakari mustakabali wa nchi yetu.Nimejikuta natumia muda mwingi na nguvu nyingi kufuatilia siasa za nchi yetu ingawa hata sina interest na siasa kivile

Tafadhali kama kuna anayeweza kunisaidia kutambua tatizo langu hili au kunishauri aniambie kitu cha kufanya maana kwa sasa kichwa changu kimechoka sana.

Please help if you can.

Shida yangu,sio pesa nahitaji mtu atakeyeweza kunipa muongoza upya katika maisha yangu kabla sijapotea kabisa.Nimeboreka sana na maisha sina interest yoyote na maisha.Sijawahi kufikiria suicide,wala sihisi kukata tamaa bali nahisi kwamba interest yangu na maisha imeshuka sana bila sababu ya kueleweka
Pole sana hilo tatizo lako linatibika nenda hospital kwa wanasaikologia watakusaidia
 
Back
Top Bottom