ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,462
- 4,794
Habari wandugu
Mimi ni mwanamume mwenye Umri wa miaka 35 Nina mke na watoto wanne.Tatizo langu ni kwamba ninahisi ninatatizo kubwa la kiakili ingawa sina uhakika.
Nilikuwa mwajiriwa na mara ghafla nikajikuta sitaki kazi bila sababu yoyote ya msingi,morale ikashuka,mahudhurio yakashuka,performance ikashuka na mwishowe nikasimamishwa kazi.Katika kipindi hicho pia nilipoteza upendo kwa familia yangu,watoto wangu,rafiki zangu na hata ndugu.Sikutaka ukaribu na mtu wala sikutaka kusaidiwa wala kusaidia mtu.Nilikuwa namiliko nyumba nikaiuza na kwenda kupanga,nilikuwa na gari nalo nikaliuza.Pesa nikazitapanya tapanya tu mpaka zikaisha.
Mke wangu baada ya kusumbuana naye kwa muda mrefu aliamua kuondoka ila mama yangu alimchukua na kukaa naye pamoja na watoto wangu.Mimi kwa sasa naishi na mwanamke mwingine ambaye nimezaa naye mtoto mmoja lakini si kwamba nampenda bali niko nae tu kama msichana wa kunifulia nguo na kunipikia,Nimehama kwenye nyuma tuliyopanga na mke wangu proper na hata sijui vitu vyangu viko katika hali gani na wala sijui kodi inalipwaje yaani i do not care
NIlikuwa namiliki ofisi tatu za biashara na zote nilizitelekeza sijua hata zina ali gani naisi kila kitu kitakuwa kimepotea ingawa hata sifuatilii wala kujali chochote.
Mimi sisi mlevi ingawa ninakunywa.Mimi sio mjinga kwa sababu nina uelewa wa mambo mengi.Sasa hivi ninakaanga chipsi tena ni siku nikijisikia kufanya hivyo.Mara nyingi huyu mwanamke ninayekaa naye ndia anahangaika kutafuta hela ya kula na kufungua kijiwe chetu cha chipsi.Yaani nimekuwa na tabia na mtazamo wa ajabu kuhusu maisha.Sijali chochote wala yoyote.Nilijiandikisha chuo kuongeza elimu anagalau nitulize kichwa lakini nako nimeshindwa kuendelea mwaka huu kutokana na kukosa Pesa.Nimelipa ada kidogo lakini nimejikuta sina interest bali naona kama napoteza tu muda.
Hapo nilipo sina interest na jambo lolote wala mtu yoyote.Hata marafiki zangu wala ndugu zangu.Niko Niko tu.
Ukiniona huwezi fikiri kwamba nimepoteza muelekeo wala huwezi hisi kwamba nina mambo magumu lakini nahisi kabisa ninachanganyikiwa na ninajizuia kwa nguvu sana.
Sijui kwa nini nimekuwa hivi.Kila nikitulia najiuliza lakini sipati majibu nikijaribu kubadilika najikuta narudi kulekule.
Ni mambo mengi sana mabaya ambayo yanaendelea kwenye maisa yangu ila haya ni kwa uchache.Tafadhali mnisaidie tatizo langu ni nini?
Jambo pekee ambalo limebaki kwenye kichwa changu ni kutafakari mustakabali wa nchi yetu.Nimejikuta natumia muda mwingi na nguvu nyingi kufuatilia siasa za nchi yetu ingawa hata sina interest na siasa kivile
Tafadhali kama kuna anayeweza kunisaidia kutambua tatizo langu hili au kunishauri aniambie kitu cha kufanya maana kwa sasa kichwa changu kimechoka sana.
Please help if you can.
Shida yangu,sio pesa nahitaji mtu atakeyeweza kunipa muongoza upya katika maisha yangu kabla sijapotea kabisa.Nimeboreka sana na maisha sina interest yoyote na maisha.Sijawahi kufikiria suicide,wala sihisi kukata tamaa bali nahisi kwamba interest yangu na maisha imeshuka sana bila sababu ya kueleweka