Maisha ya vyuoni vs Maisha ya mtaani

rusesa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
538
233
Maisha ya mtaani na yale ya vyuoni ni tofauti sana. wanachuo wengi wakiwa wako chuo huwa kama wamefunikwa blanketi nzito. starehe kibaooo, matanuzi kibaoo, anasakibaoo!

Usipojiwekea akiba na kutumia akiri yako ku plan vitu mhimu vitakavyo kusaidia baadae mtaishia kulalama ati AJIRA AJIRA AJIRA. SASA AJIRA ZA SERIKALI ZIMESITISHWA ZOTE!

Jamani maisha ya vyuoni na mtaani ni tofauti mno! SASA WALIMU WANALIA ATI AJIRA AJIRA BLANKETI NDO LIMETOKA MACHONI KWENU. TOO LATE.

USICHAGUE KAZI TAFADHALI: NAOMBA MSHIKE MASHAMBA MLIME: KUJIAJIRI KUNALIPA MNO KULIKO KUAJIRIWA.

Serikali kwa sasa inawaza kujenga viwanda walau 50. sasa mtakumbukwa lini? naomba mjiajiri mapema! mlioko vyuoni na nyie jifunzeni kwa wenzenu wanao lalama ajira ajira ajira!
 
da sawa .ila tatizo ni kwamba mtu kama mimi nmejiajili ila nataka hata niende chuo sasa naofia kutoka alafu biashara zangu zikakwama sahizi niko dillema nisome kwanza au nifanye biashara kwanza?
 
wewe kasome. ila hakikisha mradi wako uliojiajiri haufi. andaa mkakati utakao kuwezesha kufanya yote! maisha ni mapambano! usipofanya maamzi ya busara kimoja wapo utakipoteza. tumia akili yako vizuri kuandaa mkakati wa kufanikisha yote! Tumia elimu dunia na elimu ya darasani utafanikiwa tu.
 
da sawa .ila tatizo ni kwamba mtu kama mimi nmejiajili ila nataka hata niende chuo sasa naofia kutoka alafu biashara zangu zikakwama sahizi niko dillema nisome kwanza au nifanye biashara kwanza?
Maisha ni mapambano. Ukiwa dhaifu inakula kwako. fanya maamzi ya kiume!
 
Mimi mwenyew mmoja wao nilitegemea sana ajira naona hata malengo yangu hayatafanikiw kabisa. Kipindi nasoma nimeuza kila kitu (kiwanja, ng'ombe, mashamba) ili niende kusoma maana hata ndugu waliamini nitavirudisha nikipata elimu. Siamini leo mwalimu wa sayansi napigwa danadana, poleni na walimu wa sanaa pia
 
apply elimu ulioipata ili ujikomboe! unaweza hata kuanzisha kilimo cha matikiti na bado ukatusua
 
Ulimbukeni tu kabla ya kwenda chuo si alitokea kwao mtaani au kashushwa toka mbinguni
wanachuo wengi malimbukeni mnooo. hata aliyetokea vijijini haswa akifika chuo anavamia starehe zote za mjin. akimaliza anaanza kulalama ajira ajira ajira. watoto wa masikin tumieni boom vizuri la sivyo huku kitaa hali si shwariii magufuli anajenga viwanda sasa hivi.
 
Back
Top Bottom