Maisha ya Ughaibuni Vis a vis Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya Ughaibuni Vis a vis Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chupaku, May 20, 2009.

 1. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wnanajamii, Salamu!
  Napenda tujadili jambo ambalo kwa muda mrefu nimelitafakari. Kuna kipindi fulani, na hata sasa vijana wengi wa viwango tofauti tofauti vya elimu walikuwa na homa kubwa sana ya kutaka kwenda Majuu, hususan nchi za Marekani na Uingereza, ili kusoma au kutafuta maisha. Wengi walienda, baadhi wamerudi, wapo ambao wanataka kurudi na wengine wameapa kabisa kuwa hawatarudi kamwe.
  Kwenda majuu imekuwa kama suala la Ndoa-wapo wanaotaka kuingia na wapo wanaotaka kutoka. Katika makundi yote hayo mawili, kuna wale ambao hawajui waanzie wapi kurudi, wataonekanaje, na wale amabo hawajui wataendaje. Wanaotaka kwenda na wanaotaka kurudi wote wanajiona wana haki ya kufanya hivyo na ni sahihi.
  MASWALI -
  1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?
  2. Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?
  3. Ni nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
  4. Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
  KARIBUNI TUELIMISHANE!
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii topic ni sensitive sana kwa maana kila mtu anatafuta maisha anapoona panamfaa bila kujali nani anasema nini. Isitoshe hakuna nchi iliyoendelea bila ya watu wake kutoka kwenda kutafuta na kuleta.Ndiyo maana kuna akina Vasco da Gama, Christopher Columbus,Magellan,Diego Cao, na wengine waliothubutu kutoka na kusafiri umbali mrefu kwa kutumia usafiri wenye kutisha na kupambana na shida, mikasa na dhoruba mbalimbali.Maswali uliyouliza hayana majibu rahisi.
  1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?

  Kwani ni nani anapima huo utendaji haki? Haki ya nani dhidi ya nani? Kuna watu wameenda ng'ambo kwe fedha zao wenyewe bila sponsorship ya serikali. Wako waliouza mali zao ili wapate fedha za kuwapeleka huko waliko.Wasiporudi sidhani watakuwa wamemkosea mtu. Kuna wale waliosaini bond na serikali kwamba watapelekwa kusoma na wakimaliza watarudi kujenga taifa. Hawa wasiporudi labda kunaweza kuzua maswali.Lakini mwisho wa yote ni kwamba KILA MTU ANA HAKI KUTAFUTA MAISHA POPOTE.NI UAMUZI BINAFSI KWA MAANA HATA WATU WAKIRUDI, HIYOHIYO SERIKALI HAIJALI WATAENDESHA VIPI MAISHA YAO.

  2.Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?

  WOTE HAWAWEZI KURUDI THATS FOR SURE. ISITOSHE KIWANJA KILICHOPO HAKITUTOSHI WOTE KWA MAANA, MAFISADI WALISHAJINYAKULIA KARIBU KILA KILICHOPO- KWA MAANA YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO. UWEKEZAJI HATA KWA WALIO NDANI YA NCHI TAYARI NI KITENDAWILI - UFISADI KUUTOKOMOMEZA NI KAMA NDOTO KWA MAANA NI LIJISARATANI LILILOKWISHA SAMBAA KILA MAHALI.UTAKATA NINI UACHE NINI.
  UMASKINI WA NCHI HII UMEKUWA CREATED NA WACHACHE - WANAOJILIMBIKIZIA MALI KWA KUNYAKUA KILA KILICHOKO MBELE YA MACHO YAO - MAPORI,MADINI/MACHIMBO,MISITU,NYADHIFA,RASILIMALI FEDHA,N.K.ISINGEKUWA HIVYO BASI WANANCHI WANGEKUWA NA NAFUU YA MAISHA.

  3. Ni nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
  MAISHA NI POPOTE - NA CHANGAMOTO HAZIKOSEKANI.KINACHOJALISHA NI JINSI YA KUPAMBANA NAZO

  4.Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
  HUWEZI KUUJUA UTAMU WA NGOMA HADI UMEICHEZA.USHAURI - ANAYEWEZA AJARIBU ASINGOJE KUSIMULIWA.
   
  Last edited: May 20, 2009
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,425
  Likes Received: 81,472
  Trophy Points: 280
  Jirani, habari za masiku tele jirani. Naona ulipotea mtaani maana nilikuwa nikiangaza angaza huku na kule labda nitaiona ile MB 450 SE Metallic in Colour ikiingia au kutoka kwenye crib yako lakini kwa siku kadhaa sasa sikufanikiwa kuiona. Karibu tena jamvini kwetu J. Hii topic kama ulivyosema ni very sensitive, nafasi ikiniruhusu leo baadaye nitachangia kwa kirefu. Haya jirani baadaye basi.
   
 4. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  WoS,
  Hata kabla ya kushamiri kwa Ufisadi, watu walikua wana hamu ya kwenda majuu..... wakayaacha hayo mapori na rasilimali wajanja wajitwalie.....
   
 5. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Asante!
  Mi nipo hapa siku zote.
  I am a Silent Observer, remember?
   
 6. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  :) Majibu-

  1-Inategemea mana ardhi ni ya mwenyezi mungu-na kila ndege anakula alipo andikiwa...ndo mana unasikia kelele nyingi sana time ya magharibu ndege wanalia-kwa kufurahia siku imeenda salama....

  2-Tanzania si nchi masikini lakini viongozi walio pita ndo wameisambaratisha.....kuna kipindi raisi wa zamani wa Iran-alienda mbeya akasema hivi na nyie mtaomba msaada mpaka lini? Akawaeleza angekuwa na ardhi kama hio ya mbeya basi angelisha dunia nzima......sasa kwanza viogozi waanze kupiga vita ufisadi ndo wengine wataweza....

  3-Kitu kizuri kuishi ughaibuni unapata akili....unaona vipi warabu nchi zao hazina hata majani ya kulisha wanyama-wanaishi na wana saidia nchi kama Tanzania kimsaada...ukiishi nje unapata akili.......dogo.

  4- Wanao taka kurudi warudi wasio taka waendelee na zao mana kurudi au kuto kurudi hakutawasaidia kitu-Mungu ndo kisha waandikia wakaishe kule-wakijidai kuja huku na Mungu hataki wataishia kuuza makaroboi hapo barabarani na mayai na chips.....kwa kupewa shilings bora huko wanapta $...lol...:):cool:
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Chupaki, ni kweli uko sahihi kabisa kuhusu hamu hiyo ... nadhani katika hatua fulani ya maisha watu wengi wanakuwa na hamu na shauku kuonja ladha ya majuu na kuna ndoto nyingi sana zinaotwa kila siku kuhusu ughaibuni - wengine wakidhania ati kweli majuu ni kuku kwa mrija 24/7.Wengine wakifikiri majuu ni raha tupu bila jasho.To the contrary majuu ni kuku kama unaweza kuji-establish na kuweza kumudu maisha ya haraka yasiyo ya kudenguadengua kama yalivyozoeleka bongo.
  Kuhusu kwenda majuu na kuacha mapori - kweli waliyaacha lakini haina maana kuwa kama wangebakia bado wangejitwalia kiulaini.Hata walioko bongo wanakitendawili cha jinsi gani kujipatia hata kiwanja cha high density kujijengea makazi achilia mbali pori la ekari 1000 kwa ajili ya kuwekeza.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tanzania inahitaji watu zaidi wasafiri kwenda nje, siyo wale wachache walio nje kurudi nyumbani.

  Uchumi wenyewe mdogo, tutabanana wapi?
   
 9. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Anhaa, I get the point, unasema jirani yako kumbe anapigia tarumbeta kuishi ughaibuni kwa sababu huko ana mi neema, nha? Si ahame na vyake tu? But then again makorongo ya bongo hayatamtendea haki Mzee Daimler B.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,425
  Likes Received: 81,472
  Trophy Points: 280
  Kama una elimu ambayo ina soko kubwa katika nchi za magharibi basi kufanya kazi nchi za nje kunalipa sana kutokana na mishahara minono na kuthaminiwa kwa elimu yako na mchango wako hapo mahali ulipoajiriwa. Haya yote pia yatawezekana kama ni mchapa kazi mzuri na Watanzania wengi walio nje wana sifa nzuri kwenye kuchapa kazi na pia wasio walalamishi, sifa ambayo kwetu hatuna tunaambiwa ni WAVIVU!!!! L. Kuhusu kurudi au kutorudi hiyo ni mapenzi ya mtu au familia na kamwe sioni ubaya wowote ule kama wataamua kurudi Tanzania au kutorudi


  Baada ya kuishi miaka kadha nje ya nchi, leo hii kama tungeweza kurudisha nyuma time na kupewa nafasi nyingine ya kuendelea kuishi Tanzania na kwenda kuishi nje basi nisingesita hata kidogo kwenda kuishi nje

  Katiba ya Tanzania inasema kwamba Mtanzania yuko huru kwenda mahali popote duniani ili mradi havunji sheria za nchi. Kwa hiyo hapa sioni ni kivipi Watanzania waliomua kwenda nje hawatendei haki nchi yetu. Kwanza wanatuma pesa ili kusaidia ndugu, jamaa na hata marafiki katika nyanja mbali mbali zikiwamo biashara, kujiendeleza kielimu, n.k shughuli ambazo zinachangia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ambalo linarudishwa nyuma na mafisadi na watetezi wao

  Kwa maoni yangu isingesaidia chochote maana tuna viongozi ambao wao wenyewe ni mafisadi na wameingia madarakani kwa njia za kifisadi. Sidhani kama hata huwa wanatafakari gharama za ufisadi kwa nchi yetu au gharama za kusaini mikataba mbali mbali ikiwemo ya uchimbaji wa madini yetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Wanachojali wao ni kuendelea kuwapo madarakani na kuhakikisha chama chao cha mafisadi kinaendelea kubaki madarakani kwa gharama zozote zile hata kama kuwepo kwao madarakani kunachangia nchi kudumaa kimaendeleo.

  Kuishi nje mazuri yake ni kwamba pamoja na kuwa wengi wanalalamika kuhusu kodi, lakini matunda ya kodi hizo unayaona. Maji belele, umeme belele, hospitali ukiugua hutalala chini au kukosa dawa au kuombwa rushwa na Dr ambaye analaliwa mshahara. Kwa kweli quality ya maisha ni ya juu sana ukilinganisha na nyumbani. Miji ni safi, sheria za nchi au miji zinafuatwa na wale wavunjaji wanashughulikiwa ipasavyo tofauti na nyumbani ambapo Mafisadi kama akina Mkapa, Chenge, Idrissa Rashid, Yona, Mramba, mapapa mafisadi kama akina Rostam, Manji, Jeetu, Subhash, Chavda wanaendelea kupeta tu uraiani pamoja na ushahidi wa kutosha dhidi yao kuhusu ufisadi mbali mbali walioufanya dhidi ya nchi yetu ambayo unaifanya ishindwe kupata maendeleo ya kweli na kusababisha asilimia kubwa ya Watanzania kuendelea kuishi maisha yaliyojaa ufukara wa kutisha.

  Ukiangalia Dar kwa mfano, madaladala yanavunja sheria za jiji kila siku, watu wanatupa uchafu hovyo hovyo na kuchangia miji yetu mingi kuwa na uchafu wa kutisha ambao unachangia sana katika magonjwa kama malaria, kipindupindu na magonjwa mengine ya matumbo. Lakini vyombo husika havichukui hatua zozote muhimu kubadilisha hali hiyo ili kuifanya miji yetu iwe misafi na katika hali ya kupendeza. Dar ambayo kwa maoni yangu ni capital city ya Tanzania matatizo ya maji na umeme ni miaka nenda miaka rudi lakini hakuna ahueni yoyote hili linaudhi na kusikitisha sana. Kuhusu drainage system ya Dar, mvua kubwa ya nusu saa tu basi barabara chungu nzima hazipitiki kwa watembea kwa miguu au hata wenye magari na hakuna dalili zozote kama matatizo hayo niliyoyataja yanatafutiwa ufumbuzi. Kwa maana nyingine hali itazidi kuwa mbaya zaidi miaka michache ijayo

  Ni kweli unayamiss mazuri ya Tanzania ambayo yapo mengi tu hasa katika nyanja za social life.  Kama wana elimu nzuri na ambayo ina soko kubwa katika nchi za magharibi au hata katika nchi za Afrika, Uarabuni n.k. ambako mishahara ni mizuri ukilinganisha na Tanzania, basi wasisite kutafuta nafasi za kufanya kazi huko kwani kuchangia maendeleo ya Tanzani si lazima ufanye kazi Tanzania. Hata wale wasio na elimu nzuri lakini wanataka kutumia nafasi hiyo kujiendeleza kielimu basin a wao pia wachangamke tu.

  Unaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu popote pale ulipo duniani na mara nyingi kama wewe ni mfanya kazi basi uwezo huo huongezeka zaidi kama unafanya kazi yenye kipato kikubwa ukilinganisha na kile cha Tanzania. Tukumbuke nchi za Mexico na China mapato yao makubwa katika fedha za kigeni yanatokana na remittances zinazotumwa na wananchi wa nchi hizo ambao wamehamia nchi nyingine duniani. Kenya miaka michache iliyopita ilipokea remittances iliyokaribia $500 miiloni kwa mwaka mmoja tu kutoka kwa Wakenya waliohamia kufanya kazi au biashara katika nchi mbali mbali duniani. Kiasi hicho kilikuwa ni kikubwa kuliko hata misaada na mikopo ikijumlishwa pamoja katika mwaka ule. Kwa hiyo kwa kumalizia kuna mazuri mengi kwa wananchi wa Tanzania hasa wenye elimu ya juu kufanya kazi nchi za nje kwao binafsi kama individuals na pia kwa nchi yetu kutokana na remittances wanazozituma kufanyia mambo mbali mbali ikiwemo kusaidia ndugu, jamaa na marafiki. Mkipata nafasi hizo wala msizilazie damu.
   
 11. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Na kweli Bubu ulitaka kusema na umesema! Points zako ziko sawa kabisa.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  BAK umesema kweli kabisa.....angalia waPakistan na waPhilipinos wanaofanya kazi hasa UAE wanavyopeleka remittances kwenye nchi zao.Hata Tanzania, walio mijini wana uwezo zaidi kuendeleza kwao kuliko kama wangeng'ang'ania tu kubakia vijijini.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  May 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Linganisha haya:

  Mtu mwenye high school diploma nyamwezi na mtu mwenye high school diploma bongo

  Mtu mwenye digrii moja, mbili, au tatu nyamwezi na mtu mwenye digrii moja, mbili, au tatu bongo

  Homeless wa nyamwezi na homeless wa bongo

  Raisi wa nyamwezi na raisi wa bongo

  Mbunge wa nyamwezi na mbunge wa bongo

  Welfare recipient wa nyamwezi na welfare recipient wa bongo (wait a minute najua hakuna hii bongo)

  Mbeba boksi wa nyamwezi na mbeba boksi wa bongo

  Yupi mwenye nafuu zaidi?
   
 14. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280

  hapo umekosea ndugu,source kubwa ya FOREX for china sio remitance!!ni exports!!
  back in 1930s remitance used to be the highest source but,down the way they discovered that money was not going to take them out of the hole!!instead they sent their students overseas..,worldwide..,for better dams management wakaenda netherlands,satelite-rusia,uchumi UK,US etc,textile,italy etc,they sent students worldwide..,the result all miracles(of course chinese are very displined).
  the result was influx of technology and new minds from early 80's,everything the transformed from the backward china to a giant economy superpower people see today.
  the details of the process are very complicated and almost unimaginable to succeed but they pulled it up
  BUT one thing was clear..,remittance influx wasn't gonna help them...,it caused great social divides in china(lords and serfs) back in 1920's and just before 1950's.those with no access to forex had almost no way to develop.they were always takers.I understand that Tz is taking paths that asia took a century ago and they didn't work(why?)

  Fundamentaly ili tuendelee hatuhitaji pesa za remittance!!since they just recycle back buying expensive imports.(westerners are clever!!)
  we need to industrialise,we need strong education,strong IT capabilities(the future).
  pesa za remittance zitasaidia kununua magari mabovu ya japani,mafriji yanayolipuka ya dubai,!!we see it now!haazitasaidia kuweka X-ray mahositalini hazitasaidia kujenga barabara.

  this is a very close call to make,sikatai remittance kuja,BUT tusilemae nazo!!same as misaada.money do no good!!

  ndio maana BUSH yuko tayari kutoa $684million kufadhili ukimwi na malaria BUT i doubt he can do the same to build a hightech drug factories!!wanajua 70% zitarudi!tutanunua ford za miradi US,dawa zitatoka US,hata wataalam wa ngazi za juu watatoka US!!lol..,

  Kama wachina waliligundua hili na kutafuta njia mbadala why not us?look at the results!!USA is funding IRAQ and Afghanistan fundamentally from Chinese CASH!!

  trade deficit is approaching a trillion US dollars and still counting..,CHINA has changed from a remitance country to a manufacturing one..,
  of course they have other problems like access to extremely hightech semiconductor technology(core of the tech industry as of now and the future).BUT simple technologies like car manufauring,mobile phones,computers,are no longer an issue to them..,
  and they are growing in other tech demanding areas like satelite navigation,missiles,biotech,nano-tech...,

  so we don't neccesarily need to caopy china or any other countries BUT atleast lets not rely on what failed in 1920's!!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Obvious wa majuu anakuwa juu.... Tunachoomba tu basi walio majuu wajitahidi kutuma maendeleo nyumbani, inasikitisha unakutana na tu US/Uk ana maisha mazuri ajabu halafu ukija home kwa baba yake anatia huruma kabisa mpaka unashangaa

  Lets follow tiger countries ambao ku-remitt nyhumbani ni kama dini, sie tukishatuma dollar 1000 inakuwa simulizi,

  KWa sasa kuna plenty of land huku nyumbani, nunueni na mbaki huko wakati mkituma vitendea kazi sie tulime, at least ukinunua ardhi haihamishiki tofauti na magari
   
Loading...