Satoh Hirosh
JF-Expert Member
- Mar 30, 2021
- 7,145
- 28,845
Hii ni series ya matukio yaliyotokea miaka ya 2010-2013.
Ni mtiririko wa matukio ya ujasiri,kushangaza,kufurahisha na kusikitisha. Maisha ya watoto wa Temeke.
Miaka hii ilikuwa ndiyo mwisho mwisho wa uhuni uliokithiri wa watoto wa Temeke. Bhangi,wizi,mauaji, kukimbizana na defender za polisi na Kila aina ya uovu
Kwa mtanzamo wangu,hii miaka ya 2010 hadi 2013/14 ndiyo usela mavi wa vijana wa temeke ilikuwa unaishia ishia. Japo tabia za hovyo haziishagi lakini angalau miaka hii ya sasa viunga vya Temeke vina unafuu sana.
Hizi ni enzi za mwisho mwisho za Madogo wa Temeke kuzamia Bondeni(south Africa) kwa mafungu ambapo ilikuwa inaonekana ‘mchongo’. Walipozamia South Madogo wengine walichoafanikiwa ni kurudi na macheni ya silver shingoni na Pete kwenye vidole na kuishia kujisifu ujinga na starehe walizofanya wakiwa ‘Dizonga’ kwenye miji ya Durban, Jo'burg na Capetown. Wengine walirudishwa bongo wakiwa wamelala kwenye mabox na kupakiwa ndani ya ndege za cargo na kuishia kuleta vilio kwa familia zao..tukawazika. Wengine walirudi wakiwa mateja.
Kipindi hiko mitaa ya mwembe yanga kukiwa na matamasha yaliyoandaliwa na media maarufu kama clouds na times fme,shoo ilikuwa haifiki mwisho kwa sababu wahuni walijazana kati kupora watu wakati shoo ikiwa inaendelea. Hata uweke ulinzi vipi,wahuni walikuwa wanaharibu na show haiishi salama.
Enzi hizo kulikuwa na askari maarufu wa chang’ombe Polisi aliyefahamika kwa jina la Tyson. Watu wa viunga vya Temeke wanamjua huyu jamaa.
Mitaa ya Last(Tandika), Sheraton ,Maputo ,Devis corner,kaburi Moja,mikoroshini,mtoni kichangani,Mitaa ya pugila pugila,yombo na kote huko wahuni waliisoma namba kwa shoo za huyu Mwamba wa kuitwa Tyson.
Picha linaanza,jamaa alikuwa akiwakamata hawapakii kwenye difenda.
Anawaacha mtembee Huku Mkiimba ule wimbo maarufu “Jua lile literemke” na hakuna anayethubutu kumtoroka Wala kukimbia. wahuni wote waliufyata mkia na walifika Chang'ombe police salama chini yake. Jamaa alikuwa mbabe kiasi kwamba mkikamatwa anaweza kuwaambia “ambae anaona ameonewa kwa kukamatwa ajitokeze mbele apigane na Mimi,au kama unahisi unaniweza sogea hapa mbele tuzichape ukinishinda nakuruhusu usepe kiroho safi bila kukufikisha chango'mbe(au kwa lugha ya Aggrey "anayehisi ananiweza afanye kama anajikuna tu kichwani nimwone)”.
Wahuni walitazamana na hakuna aliyethubutu kunyanyuka ili akazinese na Tyson!!
Huyu askari alipowanyoosha sana wahuni wa Temeke. Nasikia baadae alihamishiwa Arusha Kwa Mafwele (enzi hizo Mafwele alikuwa Arusha)akaenda kuparangana na wahuni wa chuga.
Uhuni Temeke ulipokuwa sugu na hakuna dalili ya kuisha nikaona hapa napaswa kufanya jambo ili kuweza kucopy au kuji-camouflage na maisha ya Temeke. Nikasema Rule of the jungle,ili uweze kusurvive lazima nawe uwe mbabe kama wababe wengine,hivyo napaswa kuingia kwenye Sanaa ya mapigano.
Unajua kwa wasioelewa maisha ya mitaa ya Temeke wanaweza kuona naongea vitu visivyo halisi ila haya ndiyo yalikuwa maisha yetu.
Kipindi hiko mtu ilikuwa siyo rahisi kukatiza mitaa ya Sheraton au relini Maputo huku umejiachia unaongea na simu. Wahuni “wanakupokea” simu yako alafu wanakuambia “haya tembea ole wako ugeuke nyuma”. Na haikuwa usiku,ila mchana wa jua Kali.
Nishawahi kushuhudia wahuni wakimpora simu mdada mitaa ya relini alafu wakawa wanampulizia Moshi wa Bhang! Na hakuna kitu alithubutu kuwafanya Wala kupiga kelele maana alijua nini kingetokea endapo angepiga kelele.
Siku zikasonga na maisha ya Temeke ya usela wa kishamba hayana dili. Defender zilikuwa Kila saa kufanya patrol. Kuna muda mtu unashinda kitaani na washikaji lakini roho ikiwa juu. Kikiwaka tu unaamsha mbio,kama swala anamkimbia Chui.
Sasa Ndipo Nikakutana na jamaa mmoja mkufunzi wa Kung Fu,jamaa anapiga mkono kama komando madafu wa Ikulu. Nikasema Wacha nijifunze Kung Fu maana maisha ya Temeke hayahitaji unyonge.
Lakini kulikuwa na kikwazo..ili ujifunze sanaa ya mapigano kwa huyu jamaa lazima uwe muislamu,maana jamaa alikuwa ostadhi na alikuwa na darasa lake la madrassa,alafu Mimi ni mkristo na sielewi chochote kuhusu uislamu ila kung Fu nahitaji kujifunza… Sasa itakuwaje?
Wanasema Ukiishi Dar ni chuo kikuu. Sasa Ukiishi Temeke enzi hizo lazima uwe mjanja na mwenye akili zaidi yenye kufanya kazi kwa speed.
Nikabadili jina,nikajiita jina feki Abdul. Ila nitamshawishi vipi ostaz kuwa Mimi ni muislamu na siyo ‘kafiri' kama Hawa ndugu zetu wanavyotuita?
Ikanibidi nigeuke jasusi.
Kuna jamaa yangu mmoja ni muislamu,alisoma madrassa nikakomaa nae kwa muda Fulani ili anipige msasa kuhusu kusoma juzuu ili nipate gia ya kuingilia Dojo. Jamaa akanifunza vitu basic nikaiva kukariri. Lengo ikuwa nikistukiwa kuwa Mimi siyo miongoni mwao ila nimezamia nijue jinsi ya kujitetea.
Pale chuo(madrassa )asubuhi ilikuwa madrassa ya watoto,usiku kuanzia saa mbili jengo linageuka kuwa dojo ya Kung Fu/karate..Wazee wa kazi tukawa tunapiga mayoko geri,mawashigeri, na staili mbalimbali za mapigano.
Siku zikaenda, upande wa karate nikaiva ila sasa mtaani hakuna ishu,ni kukimbizana na defender za polisi tu,wakipita tunatoka mafichoni tunarudi kijiwe kupiga stori.
Nikahamia Last (Tandika sokoni) kuuza nguo ila Nako hakusomeki, Huku Nako ni uhuni na wizi tu vilitamalaki. Mteja ukizubaa umeisha.
Ajira hakuna,maisha magumu,nikasema Wacha nifanye jambo…!
*********
Pale mtaani kwetu Kuna mabroo watatu walikuwa wanafanya kazi bandarini.
Enzi hizo bandari Kuna Hela na mabroo wanatamba sana.
Ukiangalia chini bro ana kiatu cha maana,walikuwa hawavai viatu “mdosho” wala cheni “goroka”. Ni shati na suruali ya bei ghali,cheni Kali,na kiatu original ,ila vyote wamepiga bandari kwenye mabaro ya nguo kwenye meli. Tena walikuwa wanavizia mabaro ya Australia yenye nguo kali.
Mabroo Walikuwa wana Hela kwa sababu walikuwa wezi balaa,licha ya kufanya kazi bandari ila walikuwa wanaiba sana. Miaka ile bandari ilikuwa inapigwa na Kila mtu. Mabroo ilikuwa Kila wanapoingia kwenye viwanja vya starehe wanatambulika kama wazee wa bandari. Wakitajwa Majina bar wanatunza kama mapapaa-hela za wizi bandarini,hahah. wakimwita mhudumu awahudumie hawamdai chenji. Wakichenji 10k wanaita uchafu-baki nayo.
Shukrani zimwendee Hayati Magufuli mana alipoingia amefanya maboresho makubwa sana bandari. Enzi hizo mabroo wa Temeke wameiba sana,tatizo walikula Bata bila kufanya mambo ya maana. Wengine wamekufa kwa magonjwa.
Kipindi hiko bandarini Redio na power window za magari ziliwakoma watoto wa Temeke.Majamaa walikuwa wanaiba hadi magari mengine yanabaki skeletons. Mtajuana nyie na wateja wenu walioagiza magari japan.
Watoto wa Temeke na kurasini walikuwa siyo watu wazuri!!
Chumbani kwa mabroo kulikuwa Kuna nguo na viatu vya Kila aina. Vyote hivi wamepiga bandari. Mademu walikuwa wakija maghetoni walikuwa wanapagawa. Ndiyo kipindi hiko nikaanza kushuhudia mambo ya three some. Mabroo walifanya uchafu wa Kila aina kisa Wana Hela za bandari.
Leo bandari Ina VAR(camera) Kila mahali,mascanner na takataka kibao za ulinzi
Tusitoke kwenye reli!!
Mabroo wakatupeleka bandari Mimi na ‘mwanangu’ Y-lala.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kuishi maisha ya ustaarabu maana nilitoka kwenye kinywa cha mamba-Mtaani.. maisha ya kuishi na masela na wahuni Kila kona.
Mimi na Ylala Tukaanza kazi bandarini.
Tukawa wazee wa bandari tukiwa Madogo kabisa!!
Nilipoanza kushika vihela nikahamia mtaa mpya mbali na kule nilikokuwa naishi zamani. Nikapanga chumba Mtoni Mtongani.
Hapa ndipo kisa cha kutaka kuuawa kisa mwanamke kinaanza…
Naunganisha part two.