---maisha ya "njozi za kutisha"--

lol! given a chance i am afraid i wont go for hypnosis. i guess i am afraid of my own demons. the nightmares i get in my conscious mind ar far much worse,lol
hivi hapa bongo kuna mahali wanafanya hypnosis? is it legal?

The subconscious mind attempts to process these emotions and to resolve any hidden and unconscious conflicts
 
Kuna watu hawali vizuri, hawafanyi chochote hata kidogo cha kuwafurahisha wao au waliowazunguka kinachohitaji kutumia pesa (japo kidogo) wakisema wanawekeza kujengea mtoto/watoto future......

Hili nalo limekaaje?
Gaijin ndio maana nasema binadamu tungekuwa na uwezo wa kufahamu mwenzako anafikiria nini at that time sijui ingekuwaje
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
lol! given a chance i am afraid i wont go for hypnosis. i guess i am afraid of my own demons. the nightmares i get in my conscious mind ar far much worse,lol
hivi hapa bongo kuna mahali wanafanya hypnosis? is it legal?
Mhh!!! King'asti sijasikia kabisa hata kama yupo labda ni mmoja tu, hata mimi given a chance ssidhani kama nitaenda kwenye hiyo Hypnosis maana i guess it will be worse lol
 
mi nadhani imefika wakati tuishi kidhungu sasa! kuna binamu yangu,she was nt involving herself kwenye mambo ya kijamii na kila mtu alimpania ikifika wakati wa kuolewa! alitukomeshaje? manake nadhani alipata jamaa yuko kama yeye. kulikua hakuna kitchen party wala sendoff! walifanya harusi ya kama 30 pple, wawakilishi wa familia wawili na hakuna mchango! ukiangalia cost ya kuchangia harusi ya kila mtu si ofisini,majirani, ndugu, ndugu wa ndugu, majirani wa ndugu!!! si bora ujikatie health insurance, na bima ya elimu ya wanao (ili ukifa wasiwasuse). kama nikifa wasipozika manispaa itatafuta pa kutupa mzoga! too much sasa! na tatizo la bongo mafanikio wanaangalia mashavu (wengine hata mchicha wenye pilipili na ugali tunanona) na kabajaj (hawajui unaweka wese la buku 3, taa imewaka hadi imekufa!)

....umesema kweli tupu....hizi extended family hizi.....pasua kichwa kabisa!
kuna mheshimiwa mmoja majuzi alianzisha unyuzi kukemea vibaya sana michango ya harusi na aliyeianzisha...
---kizazi cha kudaiwa michango--- na usipotoa jamii inakutenga...! ---hata ukisema huna madhali jamii inaku judge kwa 'mafanikio' yako, imekula kwako hiyo!
 
Mbu

Hii "kuishi kwa watoto wetu" nadhani ni mentality ya Tanzania zaidi. Mtu ukimuuliza katika maisha yako umefanya nini kwa ajili ya furaha yako au maisha yako, atakuambia alipambana vikali ili mwanawe aende shule nzuri na maisha bora.

Nadhani inachangiwa na mfumo wa kijamii (serikali) uliopo. Kutokana na kutokuwepo kwa fursa sawa kwa watu wa matabaka yote. Bila ya shaka hata nchi za nje ukisoma Elite universities upataji kazi kwako utakuwa rahisi, lakini kwa vile kazi zipo za kutosha, wazazi hawalazimiki kuchanga pesa maisha yao yote kuhakikisha watoto wanasoma hizo elite universities.

Ukiangalia watu wanaoishi kwa ajili ya watoto wao wengi ni watu wanaotoka kwenye umaskini mkubwa, watu waliotoka tabaka la kati au la juu, wanaishi kwa ajili yao zaidi labda kutokana na kuwa wanaotoka kwenye umaskini huwa wanauogopa kiasi cha kuwa hawataki watoto wao waje wakutane nao
 
mwalimu,japokua mi nakubaliana kwa kiasi kuhusu kuwekeza kwenye kusomesha watoto. aisee, huku africa mwanao asipoona shule anakua mzigo kwako maisha yake yote. manake akikwama si atarudi tu? nadhani ni muhimu kwa mzazi kuhakikisha mwanae anakua na a brighter future. niliwahi kumuambia binti mmoja 'hiyo passion yako wont put food on the table. soma kwanza, utapata kazi na pa kuanzia. then u can start following ur passion kama subsidiary'. sijutii coz majuzi hapa nilimkumbusha kuhusu hiyo dream yake na naona ana opportunity za kutosha kuifanyia kazi manake elimu na kazi imemjengea network ya maana!

nakubaliana na kumpatia mtoto elimu, lakini ukitizama ama system inaforce watu au watu wenyewe wanajiforce kupeleka watoto shule ambazo kimsingi hawana uwezo nazo. Mtu anaishi nyumba ya kupanga lakini mtoto anataka asome Feza au St. Marian

Ulaya, Asia hakuna kitu kama hicho. Watu wameridhika na elimu za public schools. Utakuta familia Ulaya zinaenda vacation kila winter lakini watoto wote wanasoma shule za public. Wazazi wana-enjoy maisha yao pia.
 
Gaijin bora hata hizi public schools za huku kwetu zingekuwa zinatoa elimu nzuri basi mtu usingekuwa unafikiria kujipinda na mawazo kulipa ada ya laki saba, unajua we shape our own reality in many ways, not least in the sense that some of us just let life happen and react to whatever comes our way wakati wengine they direct themselves towards particular experiences
 
Gaijin ndio maana nasema binadamu tungekuwa na uwezo wa kufahamu mwenzako anafikiria nini at that time sijui ingekuwaje

the finest, tunaogopa sana laana bana...hiyo ni ishara tayari ya uweza wetu mkubwa wa kusoma mawazo ya watu au?

nakubaliana na kumpatia mtoto elimu, lakini ukitizama ama system inaforce watu au watu wenyewe wanajiforce kupeleka watoto shule ambazo kimsingi hawana uwezo nazo. Mtu anaishi nyumba ya kupanga lakini mtoto anataka asome Feza au St. Marian

Ulaya, Asia hakuna kitu kama hicho. Watu wameridhika na elimu za public schools. Utakuta familia Ulaya zinaenda vacation kila winter lakini watoto wote wanasoma shule za public. Wazazi wana-enjoy maisha yao pia.

...lol, Gaijin....shule za aina hii ...
MSOGA.jpg
...zinahesabika....hata kwa rangi tu yajionyesha

majority ni;
1.jpg
...hapana, serikali hailaumiki, ni mfumo tuliourithi...
....kila mtu anaanzia mfumo wa maisha ya kijamii nyumbani kwake kisha anausambaza kwa jinsi anavyoutafsiri kwa jamii yake...
 
Mbu hivi uliishawahi kukaa na kila unachofikiria ni NEGATIVE tu, yaani wewe kwako hata kile kidogo ulichoweza ku-achive na chenyewe unakisahau kabisa halafu Mbu hii topic unanitafuta ubaya lol!!!

...lol....haya bana,..pata commercial break hapa;

tumblr_le79zwatPB1qfnfzjo1_500.jpg
 
dahhhh

Mbu umenikumbusha kuna bibi mmoja alikuwa nesi kipindi hicho cha miaka ya nyuma..
Huyo bibi alibahatika kuwa na maisha mazuri sana , alipata kila alicho kitaka maishani
nikimaanisha "VITU" nyumba, gari na vingine vingi.. kuolewa hakukuwa muhimu sana kwake
lakini alipanga kuwa na watoto. nakama akimpata wa kumuoa na mwenye mapenzi ya kweli angependa zaidi.

Alikuwa na juhudi sana kazini.. Baada ya muda alienda kuongeza kisomo zaidi na akawa doctor.
wakati wa likizo alipenda ku travel nchi mbali mbali.. Kwa kweli aliishi maisha aliyofurahia sana.
aliendelee kuwaza siku moja anataka kuwa na mtoto labda "mume" lakini hakuchukua wala
kutilia maanani sana hilo .. kwao walizaliwa wawili . kwa bahati mbaya dada ake alifariki udogoni.

Kitu kimoja ambacho hatuwezi kukishika nyuma ni muda.. Muda uliendelea ku kimbiaa ..
mpaka alipo staafu akiwa na miaka 60. Ndo hapo alipogundua ya kwamba hakutilia maanani
kitu kimoja alichokita maishani "mototo/watoto" alipo kuwa na miaka 62 akagundulia na
breast cancer ..

alikuwa mwenyewe nyumbani , ukimya na majonzi yaka mzidi . Ndipo alipoa amua
kuhamia kwenye rest home. Na hapo pia uchungu ulimwingia zaidi alipo ona watoto
na wajukuu wanakuja kusalimia babu na bibi zao. yeye hana mtu hata mmoja aliejitokeza.
Na mbaya kabisa hakuwa na marafiki wengi sababu muda wake wote aliupendekeza kwake..

p.s hii story ni nje kidogo ya topic yako ila inaonyesha ya kwamba saa nyingine ni
vizuri kuwa tegemeo la familia ni vema kuwa na watu wanaokuangalia kuliko maisha
ya upweke hapo baadaye.....
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...lol....haya bana,..pata commercial break hapa;

tumblr_le79zwatPB1qfnfzjo1_500.jpg
Mbu hii commercial break imenimaliza kabisa na ndio maana hata kama mtaalamu wa Hypnosis akiwepo sitodhubutu kwenda kumuona maana inakuwa ishu zaidi kama alivyosema King'asti
 
....dahhh, afrodenzi kisa chako nacho kinasikitisha...

upatikanaji wa pesa kwa kiasi kikubwa inaendelea kuwa 'nightmare kubwa kwenye
jamii yetu, pesa zinajenga au kubomoa jamii....lawama zote hizi zinachangiwa sababu ya wingi au upungufu wa
fedha....

kuna msemo; " if you live within your means, you lack imaginations!"---(usiibe tu!)...
hebu tafakari msemo huu unaweza wiana
vipi na topiki hii,...

baaadae...
 
guys,public skuls zilikua wakati huooo! siku hizi unakuta shule haina walimu,ni wazi mtoto kufanikiwa ni ngumu. kama unafundisha udsm,na mwanao anaweza kwenda mlimani primary tena kwa miguu hii inakua imetulia. lakini kama ndo machokoroni, walimu hakuna,dawati hakuna! hata hiyo holiday ukipeleka wanao unakuwa unawaonea! na vitoto vya siku hizi mkiwa holiday vinasoma menu,havikawii kuuliza 'papaa, how much do u earn per month?'. ndo mwanzo wa kupanga bajeti ya familia pamoja,lol
 
Mheshimiwa Moskwito......respect!

Babu yangu Mzee Mtuweta aliwahi kuniambia hivi, namnukuu. "Hakuna anayeijua kesho, usiwazie ya kesho wakati ya leo hayajakutosha. Ukitaka kuwa na furaha maishani, fanyia kazi yale unayoyaona na si unayodhani utayaona kwa kuwa Mungu hajakuandikia barua kukuhakikishia utayaona hayo unayodhani utayaona".......... Endelea kulala mahali pema babu yangu mpendwa. AMEN!

Sikuwa nimemwelewa babu yangu huyu.......... siku moja nikataka anifafanulie alimaanisha nini.....

Maisha ni leo:........... Ukiishi vema leo, ukipunguza mawazo ya kuifikiria kesho utakuwa na furaha maishani.......
Akiba......... hakikisha unachokipata leo unakitumia vizuri, ili ikiwezekana ubakie na akiba ya kuanzia kesho.......... lakini kikiisha usiwaze wala kusikitika sana kwa kuwa nani alikuambia kesho utakuwa hai? Na kama leo umepata cha leo, ni kitu gani kinakufanya uhisi kesho hutapata cha kesho mpaka ukonde kwa mawazo?
Lawama ........ Usiogope lawama, eti ujitese kwa ajili ya wengine....... usingekuwepo wewe wao wasingeishi? Tumia ulichonacho kwa kadiri ya uwezo wako na si kwa shinikizo la kukwepa lawama
Majukumu.......... Timiza wajibu wako.......... kama umeamua kuwa na familia yako, pigania familia yako. Pambana!
Tuliza moyo wako........ Furahia ulichokipata..........(hapa najua alimaanisha nipige ulabu lol)...... Unatumia muda mwingi kuhangaika na maisha ambayo hujui yataisha lini........... Tafuta pia muda wa kuipumzisha akili yako.(Utaipumzishaje zaidi ya msaada wa alkoholi?)

Mengine hata siyakumbuki bana.......umri ushaenda huu........!
 
...chipilini. respect kwa babu mzee mtuweta..
Are you living the dream?

Fonts zangu zinanigomea huku kariakoo shimoni..
 
Back
Top Bottom