---maisha ya "njozi za kutisha"--

Mkuu nakubaliana na wewe….

Lakini ukiacha wale ambao wanaona majukumu ya kusaidia ni moja ya kulipa fadhila.. Pia kuna wale ambao majukumu hayo ni moja ya sehemu ya maisha yao mfano wale ambao tumetokea kwenye familia zilizopitia misukosuko ya ndoa.. Mkuu, mimi binafsi nikiwa kiumbe wa kwanza, nilisha-crash na kutaka ku-surrender kwa Mola baada ya majukumu kufika shingoni, ila namshukuru sana rafiki yangu wa Kike ambaye alibaini njama zangu na kunipiga stop..Anyway, huyu bint siwezi kumsahau na ndio maana nilikataa kumwoa na kuwa mke kwani niliogopa majaribu ya kuvunja Moyo wake hapo baadaye. Naamini huyu bint alishachukua nafasi ya Mama kunirudisha duniani kwa mara ya pili… Anyway…




Kama nilivyosema hapo juu.. Ukiacha fadhila ambayo unaweza kuipumzisha kwa muda kama Wazazi wana uwezo. Kuna historia ya maisha ya nyuma ambayo inafanya majukumu kuwa automatically part n' parcel ya maisha.. Si unakumbuka hata Baba wa Taifa alisema Tanzania haitakuwa huru hadi Afrika yote iwe huru.. Lakini hapa yataka uangalifu kwani unaweza kumaliza rasilimali kuwasadia wengine wawe huru nawe binafsi kurudi kwenye umasikini kama ilivyotokea kwa Tanzania.. Ndiyo maana nilisema wema usizidi uwezo…



Fadhila hizo Mkuu..lakini angalia pia na utamaduni wetu.. Kwani huko nyumbani Jamii haina sehemu za kutunza wastaafu (Wazee) kama ilivyo kule ulaya ambako Wastaafu wao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatunzwa kwenye viota maalumu ambavyo vinatusaidia sisi wengine kupata vibarua.. Lakini mkuu Je? Utawezaje kupata usingizi wakati umepata ajira ya kubadilisha mboga na unajiandaa kuama chumba kimoja lakini yule mstaafu ambaye alikubali kutukanwa na baniani ili mimi nipate ugali na mlenda anaangaika kuomba ulanzi na Komoni kule Ileje nyanda za juu.. Nadhani utajitahidi kumfungulia ka- baa ka ulanzi na komoni ili kiasi fulani anywe na kingine apate hela ya kutambia wenzake wakati wanakunywa ulanzi..



Ni kweli yataka moyo..hasa ikiwa kati yenu mmoja ameishi maisha ya Magharibi na mwingine ameishi maisha ya Mashariki… Lakini Pia..kuna asilimia chache ya wapenzi ambao wanahisi machungu ya wapenzi wao..



Tutamsaidia kumwambia wengi tumeishi hayo maisha.. Tulishataka kutafuta Shortcut..Lakini tukarudi njiani na kuendelea kupigika na kumwomba Mola aepushe kikombe chake na Majaribu… Mola ametusikiliza lakini sometime Yes..usione tuna smile usoni..Lakini bado tunaugulia moyoni.. Misekule ya dhiki inaendelea kutuandama wakati tunafikiri wenzetu wengi wanaendelea kuteseka na majukumu ambayo hawawezi kuyatua!
halafu tulizo.................
 
Nimeipenda saana ya huyu mzee na hayo maneno... So touching and so true...

Mbu tukizungumzia jamii yetu nafikiri na level ya maisha yetu pia huchangia saana... Mtu toka anakua yaana mambo yalomzunguka yoote yaonesha hali ya kutegemeana. Katika jamii yetu ukiwa masikini ni shida; hapo hata raha hufikirii na the way maisha yamepanda... Ukiwa na uwezo shida pia maana ujue wee ndo utalea familia yenu yoote kama sio ukoo...

Hata hivo nieme observes saana kua nikitolea mfano jamii zetu hapa; Watu wengi hutumia pesa nyingi saana bila wao kujua kua hufanya hivo... acha kwa yalo muhimu na basic kwa maisha yake... yale ya ziada.... kama un-neccessary mahitaji... nguo, viatu, kofia, accessories bila mpangilia... acha michango mtaani, kazini, kundini kwenye clubs... yaani you name it! Pesa ambazo angeweza hata weka akiba ya badae kupunguza the inevitable stresses za badae.... (sijui nimeenda off point hapa??)

safi mbu kwa uzi mzuri,kweli maisha ni kitendawili

Sijui Mbu huwa anapata wapi idea za kutukumbusha zile facts za maisha.. Salute Mkuu!

...ashadii upo ndani ya msitari kabisa, la general....kitendawili chenyewe hakina hata jibu hata umalize miji yote ya bara na pwani...tulizo...haya ngoja nikujibu jibu ambalo litawajibu nyote nilio wa quote....

hivi baada ya mgao wangu wa mwisho wa mwezi kuugawa kwenye wizara zifuatazo;
1. chakula na lishe, 2. usafiri, 3. nishati mkaa, mishumaa, mafuta ya taa na luku, 4. elimu ada, vitabu, etc 5. mawasiliano vocha, etc
hapo hujavaa, hujachangia kitchen party wala harusi, ....mbaya kuliko zote, wizara ya afya na dharura
ulichowekeza ni panadol tu na dawa mseto ya malaria...
--- halafu unalaumiwa eti mbona humalizi ujenzi---....hii ni halali kweli?

watu hao hao wanakwambia 'mwezi huu unatakiwa unisaidie mimi mzee wako milioni moja nikarabati duka langu, ndio kiinua mgongo changu na mama'ko!"...yaani unajua hiyo milioni hata ukiwekeza huna hisa, wala si mkopo tuseme utapata riba!
aisee...acha tu...kuna watu wakihadithia maisha yao utachoka!

na hii haijalishi anapokea 75,000/= , ...au milioni/=
the more you earn the bigger the demand!
 
Back
Top Bottom