Maisha ya mwanadamu ni safari yenye vituo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Safari ya mwanadamu inaanzia tumboni mwa mama yake. Hakuna anaeomba mama atakaemzaa, unajikuta uko kwenye familia. Inaweza kuwa duni au tajiri. Kituo cha kwanza cha maisha kinaanzia kwenye kuzaliwa. Unavyokua mkubwa, kuna wanaotaka kukufahamu vizuri, watauliza wewe ni mtoto wa nani? Wazazi ndiyo utambulisho wako katika jamii. Kuna watakao kupa heshima kutokana na hadhi ya wazazi wako na wengine watadharauliwa kutokana na hadhi ya wazazi wao.

Kituo cha pili cha safari ya mwanadamu ni ndoa. Kuna watakao penda kujua uko kwenye ndoa? Una watoto wangapi. Hiki ni kipengele cha muhimu hata kwenye CV. Uwepo wako kwenye ndoa ni dalili ya uwezo wa kubeba majukumu. Ndoa inaweza kukuongezea heshima katika jamii au inaweza kukufedhehesha katika jamii. Tabia na maadili ya mwenza wako itaakisi maisha yako. Ndoa imegharimu watu wengi utu wao na wengine imewapaisha kimaisha.

Kabla hujafika kituo cha tatu, kuna wanaopitia uzee. Hapa nguvu zinaanza kupunguza. Watu watapenda kufahamu watoto wako ni wakina nani. Katika kipindi hiki, familia ni ya muhimu sana. Hata ukiwa na hela za kutosha kama huna watu wenye kujali maslahi yako unaweza kuibiwa. Unapoumwa hospitali wakikuuliza nani afahamishwe hali yako ikibadilika utataja jina la mtoto au mjukuu wako.

Safari ya mwisho ni kifo. Mazishi yako yataakisi maisha uliyoishi na watu.
 
Screenshot_20210320-221800_Swahili%20Bible%20Offline.jpg
 
Safari ya mwanadamu inaanzia tumboni mwa mama yake. Hakuna anaeomba mama atakaemzaa, unajikuta uko kwenye familia. Inaweza kuwa duni au tajiri. Kituo cha kwanza cha maisha kinaanzia kwenye kuzaliwa. Unavyokua mkubwa, kuna wanaotaka kukufahamu vizuri, watauliza wewe ni mtoto wa nani? Wazazi ndiyo utambulisho wako katika jamii. Kuna watakao kupa heshima kutokana na hadhi ya wazazi wako na wengine watadharauliwa kutokana na hadhi ya wazazi wao.

Kituo cha pili cha safari ya mwanadamu ni ndoa. Kuna watakao penda kujua uko kwenye ndoa? Una watoto wangapi. Hiki ni kipengele cha muhimu hata kwenye CV. Uwepo wako kwenye ndoa ni dalili ya uwezo wa kubeba majukumu. Ndoa inaweza kukuongezea heshima katika jamii au inaweza kukufedhehesha katika jamii. Tabia na maadili ya mwenza wako itaakisi maisha yako. Ndoa imegharimu watu wengi utu wao na wengine imewapaisha kimaisha.

Kabla hujafika kituo cha tatu, kuna wanaopitia uzee. Hapa nguvu zinaanza kupunguza. Watu watapenda kufahamu watoto wako ni wakina nani. Katika kipindi hiki, familia ni ya muhimu sana. Hata ukiwa na hela za kutosha kama huna watu wenye kujali maslahi yako unaweza kuibiwa. Unapoumwa hospitali wakikuuliza nani afahamishwe hali yako ikibadilika utataja jina la mtoto au mjukuu wako.

Safari ya mwisho ni kifo. Mazishi yako yataakisi maisha uliyoishi na watu. Kama itabidi watu walipwe pesa kujaa kwenye mazishi nayo hiyo ni shughuli.
"Kabla hujafika kituo cha tatu, kuna wanaopitia uzee. Hapa nguvu zinaanza kupunguza. Watu watapenda kufahamu watoto wako ni wakina nani. Katika kipindi hiki, familia ni ya muhimu sana. Hata ukiwa na hela za kutosha kama huna watu wenye kujali maslahi yako unaweza kuibiwa. Unapoumwa hospitali wakikuuliza nani afahamishwe hali yako ikibadilika utataja jina la mtoto au mjukuu wako"

Hapo 👆👆👆 ndipo watu wanapoona umuhimu wa ndoa,kwani wawili ni wawili plus na watoto mixer wajukuu lazima utafurahia maisha ya uzeeni.

Upweke mbaya sana kwani unaweza ukakuua na mihela yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom